Wanawake tujikumbushie vituko vya leba

Mamaa Africa

Mamaa Africa

Member
Joined
Mar 1, 2018
Messages
85
Points
150
Mamaa Africa

Mamaa Africa

Member
Joined Mar 1, 2018
85 150
Habari JF,

Tukiwa tunamalizia malizia wiki la wanawake duniani hebu wanawake wa JF tiririkeni kituko ulichofanya leba ulipokuwa na uchungu.

Aisee ile kitu achana nayo uchungu ulipozidi sana niliona bora nife kuliko kuendelea kuumwa namna ile, yani inafika wakati unaona kifo ndo kitu rahisi.

Ashukuriwe Mungu kuna kusahau

Asante mama
 
wiseboy.

wiseboy.

JF-Expert Member
Joined
Aug 11, 2014
Messages
3,777
Points
2,000
wiseboy.

wiseboy.

JF-Expert Member
Joined Aug 11, 2014
3,777 2,000
Habari Jf
Tukiwa tunamalizia malizia week la wanawake duniani hebu wanawake wa Jf tiririkeni kituko ulichofanya leba ulipokuwa na uchungu!!!!!


Mimi niliongea maneno yote kichwAni, mwisho nikasema namchukia ndugu yangu flAni ambaye kiuhalisia nampendaga sana

Aisee ile kitu achana nayo uchungu ulipozidi saana niliona bora nife kuliko kuendelea kuumwA namna ile,yani inafika wakati unaona kifo ndo kitu simple...

Tiririka sasa
Halafu hamkomi kuzaa ,I wish I could be a woman... Nisingezaa ngooooo..
 
Mama Sabrina

Mama Sabrina

JF-Expert Member
Joined
Jul 30, 2016
Messages
16,921
Points
2,000
Mama Sabrina

Mama Sabrina

JF-Expert Member
Joined Jul 30, 2016
16,921 2,000
Mimi nilivyofika Leba ,nikapelekwa sehemu ya mapumziko walikuwepo wajawazito wengii,sasa uchungu ulikuwa haujanishika kivile nilikuwa natokwa na maji tu, daktari akanipima akasema bado,,sasa mle kwenye ukumbi kulikuwa na wamama wengi mwingine anaruka, mwingine anajivuta vuta chini, si nikaanza kuwacheka nikasema mbona mimi siumwii.

kKumbe bana uchungu unakuja taratibu, nikawa nashangaa kila muda unavyozidi kwenda maumivu yananizidia wale niliokuwa nawacheka wao wanajifungua wananiacha tu, kukakucha asubuhi niliona ni mwaka na nikasema sirudiii ,kama nilikuwa natembea uchungua ukaja ghafla naganda kama sanamu kama kuna mti ntaung'ang'ania kweli, ilifikia muda sitaki kuja kusalimiwa wala kuonwa na mtu yeyote maana watu wanavyozidi kuja kuniona ndivyo uchungu unazidi kuwa mkali nikawazuia.

Niliita majina yote ya Mungu nikawa namshika mama yangu namuambia aniombee haraka uchungu upoe kiuno changu kilikuwa cha moto nauchukua mkono wa mama nauweka kiunoni kwangu namwambia aniombee mama yangu mpaka alilia nilivyokuwa nahangaika nyie acheni jamani.

Usiku ulipofika saa 2 nikasikia kusukuma nikapelekwa chumbani nimefika kule kila nikisukuma hola,,wakaniwekea maji ya uchungu wapiii wakasema huyu anatakiwa kisu tu nikajitahidi kusukuma wakaja madaktari na manesi wamenizunguka mwingine kanishika kichwa ,mwingine tumbo anabinya,mwingine anaangalia njia ya mtoto (sitasahau)mtoto alitoka saa 8 nanusu kuamkia tarehe 8 na mwaka ....8 loo kazi niliipata

Sasa najiuliza wanaozaa watoto 7 au 8 wanawezaje?maana mim toka nizae sina hamu tena halaf sijawah pata maumivu kama yale toka nizaliwe sema na ukweli
Mama Aheshimiwe ,maana wanaume wangepewa huu uchungu hata dakika wangeukataa na wangetuheshimu sana
 
Mamaa Africa

Mamaa Africa

Member
Joined
Mar 1, 2018
Messages
85
Points
150
Mamaa Africa

Mamaa Africa

Member
Joined Mar 1, 2018
85 150
Mama Sabrina Mama sabrina looo pole shogangu yani ulivyoelezea yote yalinikuta mimi, mtoto alisukumwa na manesi watatu huku dokta naye anavuta jamani wanaume wangejuaga kwa kweli wasingeletaga dharau, acha mama aitwe mama, toka nitoke leba aisee nimekuwa mgumu balaa hata nipitie kitu gani sijui kama maumivu yake yatafikia ule uchungu.

Shikamoooni wamama jamani
 
owomkyalo

owomkyalo

JF-Expert Member
Joined
Dec 26, 2017
Messages
1,945
Points
2,000
owomkyalo

owomkyalo

JF-Expert Member
Joined Dec 26, 2017
1,945 2,000
mnaogopa kuzaa lakin cha ajabu amuachi kunaniii na akina nanii.

Alafu sahiv amuna wanawake kuna wasanii tu....zamani ndo kulikuepo wanawake wa ukweli kama Mama Yangu
Maana wanawake wasahivi kutwa mnawaza nanii .
 
Mzigua90

Mzigua90

JF-Expert Member
Joined
Sep 23, 2014
Messages
34,386
Points
2,000
Mzigua90

Mzigua90

JF-Expert Member
Joined Sep 23, 2014
34,386 2,000
Mi niliwekewa kidonge cha uchungu siku moja kabla ya due date. Nikawaaga rafiki zangu wale wa karibu kuwa naenda labor. Basi kila mara namuuliza nurse saa ngapi dawa itareact maana nilikua nishachoka nataka tu nimuone mtoto.

Niliwekewa saa saba mchana. Nikala mchana kama kawaida yangu nikawa busy nachat mwenyewe kwenye groups. Mama angu alikuwepo akakaa mpaka saa moja na nusu akasema ngoja arudi nyumbani akaniandalie chakula cha kesho asubuhi kama itakua sijajifungua.

Mama alivyotoka tu kule wodini nikaanza kusikia kama tumbo la period. Nakumbuka nilikua nimevaa wig nimepaka na lipstick mwenyewe. Mara nikawa sielewi elewi. Akaja nurse nikamwambia naumwa tumbo halafu kama najisikia kwenda kujisaidia haja kubwa. Akaniambia vua nguo zako jifunge tenge. Ile kujifunga tenge ndo kama nilimzindua huyu mkurya tumboni. Kutoka ward kwenda labor ni kama hatua kumi tu. Kufika nikakuta mama mtu mzima nae anasubiri kujifungua. Sasa nikaanza kutapika. Nikaanza kulia. Nikatupa wig kule maana niliona linanibana. Nilisali baba yetu mara kumi kumi. Nilikua nashikilia kitanda siachii. Nilijuta majuto yote. Nilijuta kwanini sikutoa mimba tu kuliko shida ninazopata. Nilijuta kuumwa mwanamke. Nilifikia hatua naomba Mungu anichukue tu kuliko maumivu ninayopitia.

Manurse walikoma na mimi mpaka wananiuliza mzigua gani muoga hivyo. Nilikua kiuno kikikaza sana nawaita wakija wanasema njia bado. Yule mama niliemkuta leba nikamuuliza mtoto wake wa ngapi yule anasema eti wa nne. Nikawa namuuliza unawezaje kuzaa watoto wote hao na maumivu yote haya. Ikafikia point wakanihamishia kitanda cha kujifungulia sasa.

Kitendo cha kutoka kitanda nilicholala mwanzo mpaka kitanda cha kujifungulia niliona ni kama natoka Dar Moro kwa miguu japo ilikua ni kitanda cha tatu toka nilipokua. Nikaishiwa nguvu. Nikawekewa dripu. Sasa mkono niliokua nautumia kujisugua kiuno ukawa umewekwa dripu. Nikaambiwa nikae pozi moja tu. Pale ndo nikazidisha sala za Mungu kunichukua duniani.

Hapo nishajaribu kupush kama mara nne hamna kitu. Nurses wakatoka nje wakaniambia nikijisikia haja nijisaidie tu. Sijui nilijuaje muda umefika ila niliita kwa sauti manesi kuja wakasema sasa tayari anza kupush. Hapo nimeshakata tamaa ya kuishi mmoja akawa amekaa anasubiri mtoto atoke mwingine akawa anamsukuma tumboni anamleta chini.
Mungu wa ajabu sana the moment mtoto ametoka maumivu yote yalikata.

Hata wakati wa kushonwa nyuzi wala sikuogopa sana na uoga wangu wote. Huyu mtoto mzuri nilie nae hapa nikimuangalia naona yale maumivu ya leba ni sawa tu kama nilipitia kumpata malaika mzuri hivi. Wanaume wangejua tunachokipitia leba wangetuheshimu sana.
 

Forum statistics

Threads 1,335,546
Members 512,359
Posts 32,509,312
Top