Wanawake tujikumbushie vituko vya leba

Hospital za serikali nyingi huduma ni hizo sio huko moro tu mpaka inaonekana kama kuzaa salama ni muujiza kumbe sio



Mimi naona bora ufokewe uwe ngangari kulikoni kudekezwa unazembea na hutoki mapema mle
 
Habari JF,

Tukiwa tunamalizia malizia wiki la wanawake duniani hebu wanawake wa JF tiririkeni kituko ulichofanya leba ulipokuwa na uchungu.

Aisee ile kitu achana nayo uchungu ulipozidi sana niliona bora nife kuliko kuendelea kuumwa namna ile, yani inafika wakati unaona kifo ndo kitu rahisi.

Ashukuriwe Mungu kuna kusahau

Asante mama



MIMI nafikiri huuu UZI mngetiririkia Kwenye group LA wasapts huku Sisi wengine haturuhusiwi Sana kujua nn kinaendelea Leba Ni desturi zetu waungwana huku afrika kujadiri vitu vya Reba ni mwiko
 
Morogoro Hosp nikienda kujifungua pale, ukilia unapigwa kama mtoto, wale waupe mpaka wa napata wekundu kwa makofi. Mi hawakunipiga ila waliniulia mtoto.


Unanyanyaswa mpaka unaona hiki nini,,,sitasahau pale uchungu umekolea naambiwa nenda kafate dawa nje( sikujua kumbe wanataka rushwa) nikaanza kutambaa kwenda( kumbuka sakafu ya leba na serikalini uchafu wake) nilipofika mlangoni nikaskia we vipi wewe rudi,,utaendaje sasa


Aiseee I have a tale to tell
wanawake mna roho mbaya sana then wengi huwa wanazuga wanapendana kumbe unafki tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mara ya kwanza naingia labour ward nlikutana na case (cord prolapse) mtoto alipotea nilitoka pale nkampgia Mamangu mzazi nkamshukuru sana pili nkajua kwenye sekta ya afya to be a doc tu haifanyi kuona wengne hawasave maisha manurse nao watu muhimu sana ingawa wana roho za ujasiri mno Kila napoona mama kja huwa namshukuru Mungu kuumbwa mwanaume hawa knamama sometaim acheni watuvuruge tu kaz wanayofanyaga na manurse labour ni siri baina yao
Aisee bila mwanamke tusingekuepo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi nilivyofika Leba ,nikapelekwa sehemu ya mapumziko walikuwepo wajawazito wengii,sasa uchungu ulikuwa haujanishika kivile nilikuwa natokwa na maji tu, daktari akanipima akasema bado,,sasa mle kwenye ukumbi kulikuwa na wamama wengi mwingine anaruka, mwingine anajivuta vuta chini, si nikaanza kuwacheka nikasema mbona mimi siumwii.

kKumbe bana uchungu unakuja taratibu, nikawa nashangaa kila muda unavyozidi kwenda maumivu yananizidia wale niliokuwa nawacheka wao wanajifungua wananiacha tu, kukakucha asubuhi niliona ni mwaka na nikasema sirudiii ,kama nilikuwa natembea uchungua ukaja ghafla naganda kama sanamu kama kuna mti ntaung'ang'ania kweli, ilifikia muda sitaki kuja kusalimiwa wala kuonwa na mtu yeyote maana watu wanavyozidi kuja kuniona ndivyo uchungu unazidi kuwa mkali nikawazuia.

Niliita majina yote ya Mungu nikawa namshika mama yangu namuambia aniombee haraka uchungu upoe kiuno changu kilikuwa cha moto nauchukua mkono wa mama nauweka kiunoni kwangu namwambia aniombee mama yangu mpaka alilia nilivyokuwa nahangaika nyie acheni jamani.

Usiku ulipofika saa 2 nikasikia kusukuma nikapelekwa chumbani nimefika kule kila nikisukuma hola,,wakaniwekea maji ya uchungu wapiii wakasema huyu anatakiwa kisu tu nikajitahidi kusukuma wakaja madaktari na manesi wamenizunguka mwingine kanishika kichwa ,mwingine tumbo anabinya,mwingine anaangalia njia ya mtoto (sitasahau)mtoto alitoka saa 8 nanusu kuamkia tarehe 8 na mwaka ....8 loo kazi niliipata

Sasa najiuliza wanaozaa watoto 7 au 8 wanawezaje?maana mim toka nizae sina hamu tena halaf sijawah pata maumivu kama yale toka nizaliwe sema na ukweli
Mama Aheshimiwe ,maana wanaume wangepewa huu uchungu hata dakika wangeukataa na wangetuheshimu sana
Kama tungepewa huo uchungu, nasi tungetumia maneno kama yako aya ya mwisho kwakuwa ingekuwa lazima. Kwn unafikiri wanaume hatuna yanayotusibu kama hilo la uchungu? Neno kula kwa jasho lisikie tu mdada, nyie jasho lenu labda kutembeza bidhaa mtaa kwa mtaa. Mnazaa sisi tunatafuta ngoma droo
 
Back
Top Bottom