Wanawake tujikumbushie vituko vya leba

Wanawake tujikumbushie vituko vya leba

Mwanamke uliyefundwa huwezi kusema haya mambo hadharani

Ni eidha ulizaa ukiwa mwanafunzi/mwanachuo au umekuwa mama kabla ya wakati wako.

Vinavyofanyika/kutokea leba ni siri, kuvimwaga hadharani hapa ni kujivua nguo. Ndio maana hata manesi/wakunga hawavitoi nje.
I don't agree with you. Kwani hapo Nani katumia lugha mbovu. It's just an experience. Hebu Wanawake tuache kujinyanyapaa. Tujivunie mbele za dunia shida tunazopitia katika kuleta viumbe duniani. Proud of my scars
 
Sidhani kama kuna kitu kigeni chochote duniani, uchungu na leba ni mambo ya kawaida kabisa uliza wanaosomea udaktari, kwa dunia ya leo iliyoendelea watu watakushangaa kusema jambo kama hilo, ukiingia YouTube kunazo hadi video ya kuzaa.... Sasa sielewi unazungumzia siri katika muktaza gani
Swadakta
 
Lakini si imeandikwa utazaa kwa uchungu pia nani alikuambia ule lile tunda.?
 
Jamani mimi sitaki kukumbuka maana nikikumbuka huwa kwanza nacheka peke yangu maana siku hiyo ilikua sinema, nakumbuka nilivyoenda hospital nikiwa najidai kweli nawaambia manesi nimekuja kujifungua wakawa wanaangaliana hee wanaokujaga kuzaa ndio wanakuwaga hivi? Wakati huo mimi nacheka cheka tuu eti nafuraha ya kwenda kupata mtoto , wakanipima njia ili kujiridhisha kama kweli nina uchungu wakakubali centimita kadhaa tayari nipelekwa Labour huku na chekacheka nikaingia Labour na mama maana ni private basi nikamwambia mama kaniandalie msosi wa maana maana hadi saa 12 nitakua mimeshashusha injini , mama akawa ananiangalia tuu navyojishaua anaondoka nikamwambia nesi yaani na hamu ya kuzaaa nesi akastuka etii mmh akanijibu omba Mungu baadae chupa ikapasuka nikajua ndio tayari kumbe ndio shughuli imeanza jamani niliumwa hadi nilimchukia nesi namuona kama nuksi ikabidi ni mpigie simu mume wangu aje anihamishe hospital eti sina imani na hiyo hospital tena wamenitundikia dripu 2 za uchungu lakini wapi nimeshakuwa kama chizi jinsi navyoumwa ikabidi nikimbizwe govermt wee kufika kule ndio sinema niliwaonyesha yaani sitakaa nisahahu yaani story ni ........ chakumshukuru Nilijifungua salama toto moja imara changamfu hatari kwakweli kila nikimwangalia nafarijika nasahau shida zangu zooote
 
Sasa bila uchungu unazaaje?
Kwani unapodungwa sindano ya ganzi ili kung'oa jino inakuwaje husikii uchungu?

Naelewa ni vitu viwili tofauti lakini vinalingana.

Uchungu wowote mwilini hutokea pale receptors zinapopeleka habari ya uchungu kwenye ubongo na ubongo kutoa jawabu kuwa hakika huu ni uchungu.

Uchungu wa uzazi unatokana na kutanuka kwa cervix ambayo wakati wa mimba inakuwa imefunga kabisa kuzuia hata tone la maji kutoka halafu hutanuka mpaka ukubwa wa sentimeta 10 wakati wa kujifungua.

Ganzi inachofanya ni kuzuia receptors kupeleka habari ubongoni kwa hiyo uchungu hupati.
 
Morogoro Hosp nikienda kujifungua pale, ukilia unapigwa kama mtoto, wale waupe mpaka wa napata wekundu kwa makofi. Mi hawakunipiga ila waliniulia mtoto.

Unanyanyaswa mpaka unaona hiki nini,,,sitasahau pale uchungu umekolea naambiwa nenda kafate dawa nje( sikujua kumbe wanataka rushwa) nikaanza kutambaa kwenda( kumbuka sakafu ya leba na serikalini uchafu wake) nilipofika mlangoni nikaskia we vipi wewe rudi,,utaendaje sasa

Aiseee I have a tale to tell
 
pole sana mkuu....
 
sorry
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom