Wanawake tujikumbushie vituko vya leba

Wanawake tujikumbushie vituko vya leba

sitasahau nipo chumba cha labour usiku nilikuwa zamu mrembo mmoja uchungu ukamshika mweee muoga kama nini kapush weee mpaka namuonea huruma haswa pale alipoanza kulia na kutaja idadi ya wanaume aliokula nao ujana mwisho nilishangaa alivyoniomba karatasi asaini kuwa hata beba tena mimba lkn alijifungua vizri.....siku ya siku kasahau saini aloweka kwa sasa nimjamzito tena namsubiria aje
 
nyie nashangaa mnalalamika uchungu mtoto mwenyewe wa kwanza,mi wife kajifungua watoto wa3 kwa mpigo yuko kawaida tu,hongera sana msambaa wangu
 
sitasahau nipo chumba cha labour usiku nilikuwa zamu mrembo mmoja uchungu ukamshika mweee muoga kama nini kapush weee mpaka namuonea huruma haswa pale alipoanza kulia na kutaja idadi ya wanaume aliokula nao ujana mwisho nilishangaa alivyoniomba karatasi asaini kuwa hata beba tena mimba lkn alijifungua vizri.....siku ya siku kasahau saini aloweka kwa sasa nimjamzito tena namsubiria aje
 
Najua kuna kina mama hapa wanatetea artificial painless delivery methods .....lakini tukubaliane tu sacrifice na bond ya kina mama waliopitia painful labor hata mara moja huwezi fananisha na kina mama waliopitia anaesthetisia ....
Inaeleweka pale mama anapokuwa na health issue kwa kuwa hilo tatizo lenyewe litakuwa ni bond tosha ...lakini kama ni buheri wa afya ni muhimu kuwapa moyo wachague njia ya kawaida ....
Wewe fikiria mfano familia ya kifalme kile kibibi [QUEEN ELIZABETH ] wakwe zake kwa watoto na wajukuu wana deliver normal with all riches ...

Kuna ambaye ameongelea kuwa alifanyiwa .....Councelling hiyo ni njia nzuri sana ya kuwapa moyo wazazi vijana ....na hizi hospitali kama Agakhana na nyingine private ambazo zina promote painless delivery ningeshauri zifungue kitengo cha USHAURI NASAHA kwa expectant mothers ili waandaliwe kupata uzazi salama wa kawaida .......hii pengine itaimarisha malezi hasa kwa wazazi wa leo ambao anaweza kuacha mtoto analelewa na housegal bila hata kujali .
 
ILA na nyie mngejua uchungu Tunaopata wanaume,wakati dudu imesimama afu mkojo umebana..vile misuli inasimama,uchungu wake daahhhh hamjui tu..au bahati mbaya ukalie P.U.M.B.U
 
Mimi nilivyofika Leba ,nikapelekwa sehemu ya mapumziko walikuwepo wajawazito wengii,sasa uchungu ulikuwa haujanishika kivile nilikuwa natokwa na maji tu, daktari akanipima akasema bado,,sasa mle kwenye ukumbi kulikuwa na wamama wengi mwingine anaruka, mwingine anajivuta vuta chini, si nikaanza kuwacheka nikasema mbona mimi siumwii.

kKumbe bana uchungu unakuja taratibu, nikawa nashangaa kila muda unavyozidi kwenda maumivu yananizidia wale niliokuwa nawacheka wao wanajifungua wananiacha tu, kukakucha asubuhi niliona ni mwaka na nikasema sirudiii ,kama nilikuwa natembea uchungua ukaja ghafla naganda kama sanamu kama kuna mti ntaung'ang'ania kweli, ilifikia muda sitaki kuja kusalimiwa wala kuonwa na mtu yeyote maana watu wanavyozidi kuja kuniona ndivyo uchungu unazidi kuwa mkali nikawazuia.

Niliita majina yote ya Mungu nikawa namshika mama yangu namuambia aniombee haraka uchungu upoe kiuno changu kilikuwa cha moto nauchukua mkono wa mama nauweka kiunoni kwangu namwambia aniombee mama yangu mpaka alilia nilivyokuwa nahangaika nyie acheni jamani.

Usiku ulipofika saa 2 nikasikia kusukuma nikapelekwa chumbani nimefika kule kila nikisukuma hola,,wakaniwekea maji ya uchungu wapiii wakasema huyu anatakiwa kisu tu nikajitahidi kusukuma wakaja madaktari na manesi wamenizunguka mwingine kanishika kichwa ,mwingine tumbo anabinya,mwingine anaangalia njia ya mtoto (sitasahau)mtoto alitoka saa 8 nanusu kuamkia tarehe 8 na mwaka ....8 loo kazi niliipata

Sasa najiuliza wanaozaa watoto 7 au 8 wanawezaje?maana mim toka nizae sina hamu tena halaf sijawah pata maumivu kama yale toka nizaliwe sema na ukweli
Mama Aheshimiwe ,maana wanaume wangepewa huu uchungu hata dakika wangeukataa na wangetuheshimu sana
Na sisi tuna uchungu wetu wa kutahiriwa
 
Habari JF,

Tukiwa tunamalizia malizia week la wanawake duniani hebu wanawake wa JF tiririkeni kituko ulichofanya Leba ulipokuwa na uchungu.

Aisee ile kitu achana nayo uchungu ulipozidi sana niliona bora nife kuliko kuendelea kuumwa namna ile, yani inafika wakati unaona kifo ndo kitu rahisi.

Ashukuriwe Mungu kuna kusahau

Asante mama
Najua hauta amini lkn ndio nakwambia ukweli

Nimezaa watoto 3 sijui uchungu ni nini kabisaaa

Nikifika nasubiria wakitaka kuniwekea uchungu nakataa nawaambia me ndio nilivyo wanaondoka kwa hasira wakirudi wanakuta tayar toto anatokaa

Mtoto Wangu wa mwisho nimejifungua napiga stori name dokta na mume leba mana alishanizoea

Mtoto wa piling dokta hakuamini kama nazaa bila uchungu akaamua kushuhudia na nilimzaa huku napiga chafya nyingi kwa harufu ya perfume ya dokta haikunipenda

Mtoto wa kwanza nimejifungua nyumbani nimekaa na mama mkwe chupa ikavunjika Sina habari mama mkwe ananiambia we Penny mtoto anaanguka ikabidi amuwahi uzuri Mtoto hakuanguka

Hivyo ndio vituko vyangu hakunaga anaeamini lkn ndio ivyo
 
Pia wababa tuliosusiwa watoto inabd kifanyike kitu
Nyie tatizo mnajifanya vichwa ngumu.
Ndio maana tunawasusia.
Ila idadi ya single parents ni kubwa kwa upande wa wanawake ukilinganisha na upande wa kiumeni.
Ndio maana asasi nyingi sana zinajaribu kuingilia kati upande wetu
 
Najua hauta amini lkn ndio nakwambia ukweli

Nimezaa watoto 3 sijui uchungu ni nini kabisaaa

Nikifika nasubiria wakitaka kuniwekea uchungu nakataa nawaambia me ndio nilivyo wanaondoka kwa hasira wakirudi wanakuta tayar toto anatokaa

Mtoto Wangu wa mwisho nimejifungua napiga stori name dokta na mume leba mana alishanizoea

Mtoto wa piling dokta hakuamini kama nazaa bila uchungu akaamua kushuhudia na nilimzaa huku napiga chafya nyingi kwa harufu ya perfume ya dokta haikunipenda

Mtoto wa kwanza nimejifungua nyumbani nimekaa na mama mkwe chupa ikavunjika Sina habari mama mkwe ananiambia we Penny mtoto anaanguka ikabidi amuwahi uzuri Mtoto hakuanguka

Hivyo ndio vituko vyangu hakunaga anaeamini lkn ndio ivyo
Asee mkuu nakutamania...I wish I culdu be Money Penny
 
Nilikosea wodi siku hiyo nikaingia leba aseee.namskia mdada analia mamaa weee nakunyaaaa nakunyaaaa daaahh ikabidi nihuzunike tu
 
Mimi nilivyofika Leba ,nikapelekwa sehemu ya mapumziko walikuwepo wajawazito wengii,sasa uchungu ulikuwa haujanishika kivile nilikuwa natokwa na maji tu, daktari akanipima akasema bado,,sasa mle kwenye ukumbi kulikuwa na wamama wengi mwingine anaruka, mwingine anajivuta vuta chini, si nikaanza kuwacheka nikasema mbona mimi siumwii.

kKumbe bana uchungu unakuja taratibu, nikawa nashangaa kila muda unavyozidi kwenda maumivu yananizidia wale niliokuwa nawacheka wao wanajifungua wananiacha tu, kukakucha asubuhi niliona ni mwaka na nikasema sirudiii ,kama nilikuwa natembea uchungua ukaja ghafla naganda kama sanamu kama kuna mti ntaung'ang'ania kweli, ilifikia muda sitaki kuja kusalimiwa wala kuonwa na mtu yeyote maana watu wanavyozidi kuja kuniona ndivyo uchungu unazidi kuwa mkali nikawazuia.

Niliita majina yote ya Mungu nikawa namshika mama yangu namuambia aniombee haraka uchungu upoe kiuno changu kilikuwa cha moto nauchukua mkono wa mama nauweka kiunoni kwangu namwambia aniombee mama yangu mpaka alilia nilivyokuwa nahangaika nyie acheni jamani.

Usiku ulipofika saa 2 nikasikia kusukuma nikapelekwa chumbani nimefika kule kila nikisukuma hola,,wakaniwekea maji ya uchungu wapiii wakasema huyu anatakiwa kisu tu nikajitahidi kusukuma wakaja madaktari na manesi wamenizunguka mwingine kanishika kichwa ,mwingine tumbo anabinya,mwingine anaangalia njia ya mtoto (sitasahau)mtoto alitoka saa 8 nanusu kuamkia tarehe 8 na mwaka ....8 loo kazi niliipata

Sasa najiuliza wanaozaa watoto 7 au 8 wanawezaje?maana mim toka nizae sina hamu tena halaf sijawah pata maumivu kama yale toka nizaliwe sema na ukweli
Mama Aheshimiwe ,maana wanaume wangepewa huu uchungu hata dakika wangeukataa na wangetuheshimu sana
Mpaka nimelia mateso uliopitia na mm ndo niliopitia Niliumwa uchungu siku tatu tena wanguvu nilipauka nikawa kama kichaa alieniona alitoa macho kwa jinsi nilivyo kuwa.

Kiukwel nilipitia mateso yote,uchungu niliumwa,drip ya uchungu niliwekewa na ikashindikana kilicho fuata ni kisu siku ya nne tena saa 11 jion. shikamoo mama!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom