Siyo kuwa hatuyajui wengine tunawasaidia kupokea vitoto vyenu cha msingi acheni vituko acheni kabisaMi niliwekewa kidonge cha uchungu siku moja kabla ya due date. Nikawaaga rafiki zangu wale wa karibu kuwa naenda labor. Basi kila mara namuuliza nurse saa ngapi dawa itareact maana nilikua nishachoka nataka tu nimuone mtoto.
Niliwekewa saa saba mchana. Nikala mchana kama kawaida yangu nikawa busy nachat mwenyewe kwenye groups. Mama angu alikuwepo akakaa mpaka saa moja na nusu akasema ngoja arudi nyumbani akaniandalie chakula cha kesho asubuhi kama itakua sijajifungua.
Mama alivyotoka tu kule wodini nikaanza kusikia kama tumbo la period. Nakumbuka nilikua nimevaa wig nimepaka na lipstick mwenyewe. Mara nikawa sielewi elewi. Akaja nurse nikamwambia naumwa tumbo halafu kama najisikia kwenda kujisaidia haja kubwa. Akaniambia vua nguo zako jifunge tenge. Ile kujifunga tenge ndo kama nilimzindua huyu mkurya tumboni. Kutoka ward kwenda labor ni kama hatua kumi tu. Kufika nikakuta mama mtu mzima nae anasubiri kujifungua. Sasa nikaanza kutapika. Nikaanza kulia. Nikatupa wig kule maana niliona linanibana. Nilisali baba yetu mara kumi kumi. Nilikua nashikilia kitanda siachii. Nilijuta majuto yote. Nilijuta kwanini sikutoa mimba tu kuliko shida ninazopata. Nilijuta kuumwa mwanamke. Nilifikia hatua naomba Mungu anichukue tu kuliko maumivu ninayopitia.
Manurse walikoma na mimi mpaka wananiuliza mzigua gani muoga hivyo. Nilikua kiuno kikikaza sana nawaita wakija wanasema njia bado. Yule mama niliemkuta leba nikamuuliza mtoto wake wa ngapi yule anasema eti wa nne. Nikawa namuuliza unawezaje kuzaa watoto wote hao na maumivu yote haya. Ikafikia point wakanihamishia kitanda cha kujifungulia sasa.
Kitendo cha kutoka kitanda nilicholala mwanzo mpaka kitanda cha kujifungulia niliona ni kama natoka Dar Moro kwa miguu japo ilikua ni kitanda cha tatu toka nilipokua. Nikaishiwa nguvu. Nikawekewa dripu. Sasa mkono niliokua nautumia kujisugua kiuno ukawa umewekwa dripu. Nikaambiwa nikae pozi moja tu. Pale ndo nikazidisha sala za Mungu kunichukua duniani.
Hapo nishajaribu kupush kama mara nne hamna kitu. Nurses wakatoka nje wakaniambia nikijisikia haja nijisaidie tu. Sijui nilijuaje muda umefika ila niliita kwa sauti manesi kuja wakasema sasa tayari anza kupush. Hapo nimeshakata tamaa ya kuishi mmoja akawa amekaa anasubiri mtoto atoke mwingine akawa anamsukuma tumboni anamleta chini.
Mungu wa ajabu sana the moment mtoto ametoka maumivu yote yalikata.
Hata wakati wa kushonwa nyuzi wala sikuogopa sana na uoga wangu wote. Huyu mtoto mzuri nilie nae hapa nikimuangalia naona yale maumivu ya leba ni sawa tu kama nilipitia kumpata malaika mzuri hivi. Wanaume wangejua tunachokipitia leba wangetuheshimu sana.
Kama uliweza kupanua mapaja usindweje kupushi tu

