For two years, I followed very closely what was taking place in this blog, Jamii Forums, as a guest. On May 31st 2008, I decided to register as a member and I am glad I did. The country was going to the dogs and nobody but its true and humble citizens like us could save it.
Mchango wangu wa kwanza ulimhusu Mbunge wa Kyela Dr. Mwakyembe.
Mchango wangu wa pili ulihusu tamko la Mbunge wa Same kutoka CCM, Ana Kilango.
Je wana JF, nilikosea? Msimamo wangu ni huo huo hadi leo na umekuwa hivyo toka mfumo wa vyama vingi ulipoanza na CCM (kikundi cha watu wachache) ikajitwalia kwa wizi mali zote zilizokuwa za Watanzania wote (milioni thelathini)
Nilipojiunga JF niliamini humu kuna kundi la watu huru wasiofungamana na upande wowote na ambao kilichowafanya wajiunge na Jamii Forums ni ule uchungu wa kuona taifa lao linateketea. Hawa niliamini wako tayari kuungana na wazalendo wengine wenye mawazo kama hayo ndani na nje ya Jamii Forums kutafuta njia za kuinusuru Taifa kwa amani. Niliamua kuwa ni muda muafaka kwa kundi hili kuwa tayari kusimama na kuhesabiwa katika hizi harakati za ukombozi, naam kulikomboa taifa letu, Tanzania.
Nachukua fursa hii kuwapongeza wana JF wote ambao wameunga mkono juhudi hizi na kusimama kidete kutetea taifa letu tunalolipenda bila kujali itikadi zao. Kwamba nchi inateketea, ni ukweli ambao haitawezekana kuuzika hata kama tutajaribu kuufukia chini ya itikadi, dini, rangi, jinsia, wadhifa, mali na vishawishi vinavyopofusha macho, masikio na zaidi ya yote akili. Kama kawaida wapo watetezi wa status quo wanaoamini Tanzania haiwezekani bila CCM lakini baada ya miaka hii yote kuendelea kujidanganya hivyo ni upofu.
Asante JF kwa kutupanulia wigo wa mapambano, vita vilivyopo mbele yetu kama taifa ni kubwa na ngumu na si kama nilivyofikiria nilipojiunga JF...sikujua humu nitawakuta watu kama
Ritz,
chama,
zomba na wengineo ila nawapongeza wote ambao kweli wanakerwa na tunakoelekea na wanaona umuhimu wa dereva kupumzishwa. CCM inaingia kwenye rekodi ya Guiness book kama chama kilichokaa madarakani kwa miaka mingi huku bado ikijizatiti kung'ang'ania kwa njia zozote zile iwe ufisadi, ukandamizaji na hata mauaji ikibidi.
A luta continua!