SoC03 Walimu wa shule binafsi wawe na hadhi sawa na wale wa shule za serikali

Stories of Change - 2023 Competition

Colly 7

Member
Jul 27, 2022
88
442
Kimsingi, shule zote (za msingi na za sekondari) zilizosajiliwa, zipo chini ya serikali, na hivyo zinasimamiwa na Ofisi ya Rais, Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, pamoja na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia. Shule zote, ziwe ni za serikali au za binafsi, zinawajibika kufuata taratibu, miongozo, sera na sheria zilizotungwa au zinazotungwa na kusimamiwa na wizara nilizotaja hapo juu. Hii ndio maana mitaala inayotumika shule za serikali ndio hiyohiyo inayotumika shule za binafsi; na mtihani wa taifa ni mmoja kwa shule zote kwa kila ngazi (Darasa la nne, darasa la saba, kidato cha pili, kidato cha nne na kidato cha sita).

Kwa kifupi, shule zote shule zote ni mali ya serikali, isipokuwa zile shule tunaziita za binafsi, zinaendeshwa na sekta binafsi kwa niaba ya serikali. Kwa maneno mengine, tunaweza kusema, serikali imetoa kandarasi kwa sekta binafsi kuendeshwa shule zake (serikali). Jambo ambalo kwa mtizamo wangu naona limesahaulika na serikali katika shule hizi zinazoendeshwa na watu binafsi, ni swala la waalimu, ambao wana mchango mkubwa sana katika utoaji wa taaluma nchini.

Hadhi ya Mwalimu wa Shule ya Serikali ni Tofauti na ile ya Mwalimu wa Shule Binafsi

Kutokana uhaba wa ajira, hasa za serikalini, kumekuwa na waalimu wengi waliomaliza vyuo katika ngazi mbalimbali mitaani, wanaosaka ajira. Waalimu wachache wamebahatika kuajiriwa katika shule binafsi. Cha ajabu, waalimu hawa, huendelea kuomba kazi katika shule za serikali kila mwaka zinapotangazwa.

Kwa nini wanatafuta kazi hiyohiyo serikalini? Waalimu hawa hujiona kama bado hawajaajiriwa, yaani wamejishikiza tu, kwa sababu:

1. Waajiri wengi hawatoi mikataba ya kazi, hata kama mwalimu amefanya kazi miaka mitatu mfululizo;

2. Malipo ni madogo, mara nyingi hayafikii hata kima cha chini cha mshahara kilichowekwa na serikali, bila kujali kiwango cha elimu na uzoefu kazini;

3. Waalimu hawa hawalipiwi bima ya afya;

4. Waalimu hawa hawawekewi akiba katika mifuko ya jamii kama NSSF, PSSF, nk;

5. Waalimu hawa hawana ajira ya uhakika au ya kudumu, unaweza kuachishwa kazi muda wowote kwa utashi wa mwajiri;

6. Waalimu hawa sii wanachama wa Chama cha Waalimu Tanzania (CWT);

7. Waalimu hawa sii wanachama wa chama chochote cha Wafanyakazi;

8. Mara nyingi waalimu hawa wa shule binafsi hawashirikishwi kwenye kazi mbalimbali zinazohusu taaluma; mfano kusimamia mitihani katika ngazi mbalimbali; semina au warsha mbalimbali, na kadhalika, ambavyo ni motisha kwa waalimu;

9. Waalimu hawa hawapandi madaraja kama ilivyo serikalini; na

10. Waalimu hawa hufanya kazi nyingi na kwa muda mrefu bila malipo ya ziada

Waalimu wa Shule za Serikali
Ingawa kila mara waalimu hawa hulalamika kuhusu changamoto mbalimbali za kazi yao, kama viwango vya mshahara kuwa vidogo ukilinganisha ka uzito wa kazi, ucheleweshwaji wa kupanda madaraja, miundombinu mashuleni, na kadhalika; waalimu hawa wananufaika na vifuatavyo:

1. Wana mikataba ya kazi ya kudumu;

2. Mwalimu anayeanza kazi hulipwa kiasi kilichokubalika na serikali kilingana na kiwango cha elimu;

3. Wana bima ya afya;

4. Wamejiunga na mifuko ya jamii na mwajiri huchangia kila mwezi;

5. Ni wanachama wa Chama cha Waalimu Tanzania (CWT), ambapo hunufaika kwa namna mbalimbali;

6. NI wanachama wa Vyama vya Wafanyakazi;

7. Wanashiriki kazi mbalimbali za serikali zinazohusu elimu, kama usimamizi wa mitihani, usahihishaji, semina, warsha mbalimbali, na kadhalika;

8. Hupanda madaraja ya kazi kila mara kwa mujibu wa sheria za kazi;

9. Hufanya kazi kwa masaa na kiasi kilichokubalika kisheria, na endapo watafanya zaidi, hufidiwa kwa namna mbalimbali, ikiwa pamoja na malipo ya fedha;

10. Ana haki ya kupata likizo, yenye malipo;

11. Ana haki ya kujiendeleza kitaaluma, bila kupoteza ajira na malipo; na mengine mengi.

Serikali Inaweza Kuinua Hadhi ya Waalimu wa Shule za Binafsi
Ukiangalia maslahi anayopatiwa Mwalimu wa shule za serikali, ukalinganisha na yale anayopata Mwalimu wa shule za binafsi, utangundua ni kwa nini kuna wimbi kubwa la waalimu wanaoomba ajira za shule za serikali.

Ni ukweli kwamba serikali haiwezi kuajiri waalimu wote wanaoomba ajira, ingawa mashule mengi ya serikali yana upungufu wa waalimu; hii ni kutokana na changamoto ya bajeti ya kila mwaka. Pia serikali hawezi kufanya kila kitu bila kushirikisha sekta binafsi, vinginevyo kama shule binafsi zingekuwa hazipo, watoto wote wangerundikana katika mashule ya serikali.

Kwa muktadha huu, sekta binafsi inasaidia serikali kubeba mzigo wa kutoa elimu kwa Watanzania. Kwa hiyo serikali inapaswa kutoa na kusimamia mwongozo wa ajira kwa waalimu kwa shule zote za binafsi, ili kuhakisha wanapata haki zao sawia na wale wa serikalini.

Hii itakuwa na manufaa kwa serikali, kwani itapunguza wimbi la waalimu kuendelea kuomba kazi serikalini, ambazo ni chache.

Tovuti ya Statistica inaonyesha ya kuwa mpaka mwaka 2021 kuna shule msingi za umma na binafsi zaidi 18,000, ilihali za sekondari zikiwa 5,289. Kwa upande wa sekondari, kati ya jumla ya shule 5289, 1289 ni za binafsi (sawa na karibu asilimia 20). Hii inaonyesha umuhimu wa mchango wa sekta binafsi kwenye elimu.

Mapendekezo
1. Wakati wa usajili wa shule binafsi, pamoja na mambo mengine, wamiliki wapewe mwongozo wa ajira kwa waalimu wake, ili kuhakikisha mazingira ya kazi ni sawa wote (wa binafsi na wa serikali).

2. Kwa kuwa watoto karibu wote wanapata elimu kupitia shule binafsi ni Watanzania, serikali itoe ruzuku kwa shule binafsi, ili pamoja na mambo mengine ziweze kuwalipa waalimu stahiki zao ipasavyo.

Rejea
www.statistica.com
 
Kazi nzuri mkuu✊🏾
 
Ni kweli, maadamu wote hawa wamesoma katika viwango sawa.
 
🤣🤣🤣..shule binafsi hizihizi ninazozijua?..

Nowadays huko private schools hata mishahara hakuna bali kuna posho..

Kuna shule ni mali ya kanisa mkoani tanga - bumbuli na lushoto watumishi hawajalipwa KWA miezi zaidi ya kumi..wanadai madeni makubwa..nwa wakifuata uongozi wa kanisa wanapewa majibu mepesi..

Hilo kanisa sitalitaja...na shule sitaitaja ila ipo halmashauri ya Bumbuli na nyingine ipo lushoto.🤣🤣🤣
 
Back
Top Bottom