tpaul
JF-Expert Member
- Feb 3, 2008
- 21,857
- 18,273
Serikali hii ya CCM ina mambo ya ajabu sana. Ni aibu kwa serikali inayojinasibu kuzingatia usawa kufanya uhuni wa kiwango hiki. Sijawahi kuona serikali yenye ubaguzi mkubwa kwa wananchi wake hapa ulimwenguni kama serikali ya CCM.
Katika uchaguzi wa wanafunzi watakaojiunga kidato cha kwanza mwaka 2024, serikali imeonyesha ubaguzi wa waziwazi kati ya wanafunzi wa shule za kata na shule binafsi. Hii tabia ya kibaguzi haifai hata kidogo. Tukumbuke kwamba kuna wazazi wa watoto wanaosoma shule binafsi ambao wangependa watoto wao waendelee na masomo katika shule za umma. Inasikitisha serikali imeamua kukatisha ndoto hizo kwa makusudi.
Nitatoa mifano hai ili kuthibitisha hili ninalosema hapa. Nimechukua sampuli ya shule mbili kutoka kata moja (moja ya serikali na nyingine ya binafsi) ili kuuonyesha umma wa watanzania jinsi serikali ya CCM ilivyojaa ubaguzi wa kipuuzi uliopindukia. Lengo la kuchukua shule kutoka kata moja ni la kitafiti zaidi…..kwamba wanafunzi wote wanatoka eneo moja lenye mazingira yanayofanana; hivyo hakuna sababu ya kuwabagua.
Tazama matokeo ya shule hii binafsi jinsi wanafunzi wake walivyofanya vizuri: https://matokeo.necta.go.tz/results/2023/psle/results/shl_ps0206131.htm
Linganisha matokeo hayo na haya ya shule ya kata: https://matokeo.necta.go.tz/results/2023/psle/results/shl_ps0206125.htm
Utaona idadi ya A kwenye shule binafsi ni 58 huku shule ya kata wakiambulia 9 tu!
Sasa njoo kwenyye uchaguzi wa wanafunzi waliochaguliwa kwenda shule za sekondari mwaka 2024. Serikali imechagua wanafunzi 2 waliopata A tu kutoka shule binafsi kwenda shule teule. Wengine wote waliosalia wamerundikwa kwenye shule za kata za kutwa kama mnavyoona.
Uchaguzi wa Wanafunzi wa Kidato cha Kwanza, 2024
Na pia wamechaguliwa wanafunzi 2 tu kutoka shule ya serikali iliyofanya vibaya na wanafunzi hao wamepata B mbili katika masomo yao. Haki iko wapi?

Kama serikali ingekuwa inafuata haki, wanafunzi wote 58 kutoka shule binafsi wangechaguliwa kwenda shule teule. Lakini kwa kuwa ubinafsi na upendeleo umetawala ndani ya roho zao za kutu, wameamua kuchagua wanafunzi 2 tu ili kufunika kombe mwanaharamu apite. Serikali hii ina mambo ya kijinga sijapata kuona.