yna12
JF-Expert Member
- Jan 2, 2018
- 1,936
- 2,319
Nakumbuka kipindi flani nilikua nasoma shule moja iko mbeya maeneo ya uyole pale..kuna dada alikua mlokole hatari na alikua ananipenda mno kukawa na tabia watu wanalalamika wanakabwa usiku..mbaya zaidi mchawi mwenyewe alikua ni huyo dada na alikua anakaba kupitia sura za wengine..basi watu wakiamka asubuhi wanadundana matron anaingilia kati..na yule dada alikua mrembo na mpole haumzanii kama ni mchawi na alikua na tabia ya kunipa ndizi nimekula sana ndizi zake siku za ubwabwa..ilivyokuja kugundulika yeye ndio mchawi aisee nikakumbuka zile ndizi alizokua ananipaga..Ile siku sitaisahau nilijitapisha hadi nikaishiwa nguvu maana nilikua nawaza zile hazikua ndizi