Vituko vya Maisha ya Boarding, Tukumbushane Tuliosoma Huko

Vituko vya Maisha ya Boarding, Tukumbushane Tuliosoma Huko

Magodoro ya bwenini yalikusanyika na kuuzwa kijiji cha jirani siku ya kuondoka shule pesa yote heshima baaa kesi waliachiwa njuka wakubwa wamesepa kwi kwi kwi
Dah,,michezo kuuza magodoro kwl ilikuwepo sana,,unakuta fom four wakimaliza watu mnakuwa makini mbaya kulinda magodoro,,haha
 
Nakumbuka Sikh ya mazingira form one Pugu sekondari na Foadi akiwa form two alitutesa sana alitupamdisha kilima cha pond, simsahau. Mmh ukaguzi wa mabweni na mwl Mosha acha Bwana. Halafu kwenye mabanda ya MIFUGO na Majura, amestaafu yupo Mahuta
 
Maisha ya boarding siyo kabisaaa kwanza kula maharagwe jamani......nakumbuka nlipewa adhabu ya kukata kuni mia tatu.....dah ile adhabu sitasahau
Hahaa hyo nakumbuka tumefika fom one,,mi nimezaliwa na kukulia dar af tukakutana na kazi ya kukata kila mmoja kuni 20,,dah,, uzuri nlikutana na mwana wa sanya juu huko kwake haikuwa kazi akanipga tafu chaap
 
Maisha ya boding ukitaka kummega demu mnapeana miadi mkutane darasani asubuhi ya saa 12 wkt watu bdo wako mabwenini,,basi mnabanduana asubuh asubuh na lile barid la kule milimani mkitoka hapo wepesiiii
 
Kuna jamaa alokua anapiga msuli sana alafu yuko vizuri sana kichwani lakini mlevi wa bange. Alikuwa anajiita "marking scheme"

Basi term moja akaishiwa pesa ya bange, akaamua kuuza godoro eti alale wenzake wakiwa prepo alafu wakirudi ile saa nne aamke akakeshe

Kauza godoro. Siku ya kwanza muda wa prepo akalala, kufika saa nne jamaa tukamwamsha aende kukesha
Basi jamaa kasoma weee kasoma weee hakukuchi, akalikumbuka godoro lake lakini hana uwezo wa kulirudisha, hela keshavutia

Basi, jamaa karudi kulalia chaga zake asubuhi tunaamka kajikunja hadi huruma
 
bakora za mwalimu Bengesi
emoji23.png
emoji23.png
emoji23.png
Dah! umenikumbusha Bengesi mzee wa " Waleta obushabi shabi"
huku ana kupiga mabegani na fimbo uliyomletea endapo utamletea fimbo
ndogo ndogo.😀😀😀😀
 
Pengine tunafahamiana. Nilikuwa Ihungo. Ukitoka chooni utanuka harufu ya choo kwa masaa kadhaa hivi...
Hahah,,hyo ilikuwa tukienda chooni si tulipaita jumba kwanza unavua nguo zote ndo unaingia toi asee ukiwa uchi wa mnyama na ukitoka lazima utulie tulie kwnza harufu ikuishe,,watu weng walikuwa wanakunya wakati wa kwenda kuoga
 
Nilisahau Shamba dress.Jamani ila kwa kweli tulisoma boarding za Kayumba we are strong than ever.Shida ya maji sasa acha kabisa.O level nilisoma Rugambwa girls yaani kule maji tulikuwa tunafuata kwenye kijito flani hivi kina mawe makubwa kabisa.Halafu sasa kule vyoo vilikuwa vinaziba,kuzibua sasa.Imagine mavi yanajaa hadi yanatokezea kwenye pavements.O My God sitaki kukumbuka.Ila namkumbuka sana mpishi Kaka hansi na Samaki wa mama nelly,jongwe,blue band.Vyoo vya Ihungo vilikuwa vichafu balaa.
jamaani
 
Umenikumbusha boarding school
Kuanza tu wakavunja sanduku wakaiba kila kitu lakini nilihakikisha bweni zima hakuna kulala.
Ndoo za maji kwenye magodoro ya fisi mpaka kilieleweka.

Asie kuwemo na aliyekuwemo wote kesi moja, kila wakianika wakirudisha namwagia tena.
Mpaka wakarudisha hadi mswaki.

Survival of the fittest
Ingawa ilikuwa miaka kumi baada ya uhuru, utafikiri ni Jana tu
 
Boarding ya seminary haikuwa na makubwa zaidi ya manual work na ukali wa ratiba. Ila ya Forest Hill ilikuwa balaa! Kila hostel inatambia nyingine kwa ku-import mademu, kupiga exile, fuko families, miziki ya usiku n.k
 
Nakumbuka tulikuwa tunasoma na Mmasai mmoja hivi shule ya sekondari moringe, alikuwa anajifanya mbabe, tukaenda Monduli Mjini tukanunua kufuli aina ya solex moja matata, ile tumepiga mbonji mwenzetu mmoja akachukua kufuli na kulibana kwenye sikio lake, asubuhi bweni zima tukawa wa kwanza kutoka na kumwacha mshikaji akiwa peke yake bwenini, tumekaa kidogo tukaona vumbi tu nje jamaa anakuja mbio huku shingo imekaa upande kwa uzito wa kufuli, kila mmoja akaanza kutafuta upenyo wake maana tukajua damu itamwagika kwa hasira alizokuwa nazo yule Mmasai, basi akashinda na kufuli siku nzima maana hakuna aliyethubutu kusema nani ana funguo wa wa lile kufuli, ile tumepiga mbonji mwenzetu mmoja akachukua funguo akampenyezea kwenye blanketi lake, kufika asubuhi hamadi anakuta funguo, lakini aliyeuweka hakumjua hadi tunamaliza maana angemjua damu ingemwagika kwa hasira alizokuwa nazo yule Mmasai,
Nje Mkaona vumbi tu linatimka jamaa anakuja mbio[emoji23] [emoji23] [emoji23] nimecheka aisee hadi kila mtu hapa kashangaa
 
kupiga simu chooni, kuvuta mjani, kugonja walimu wa kikeni waliokuwa wakija field, kuuza biskuti, kuvunja makontena ya vilaza, watu tulikuwa na funguo zaid ya 500 hizi ni za kupampu makufuli, wakati tuko shule, tunamiliki shamba bondeni, la nyanya na miwa, kupiga walimu wanoko mida ya prep, kutoroka usiku tunaenda mlima zinaa, kulala ktk mabweni ya wasichana na wasichana kujichanganya ktk mabweni ya masela, kuingia class na vi bom, kupiga simu chooni, disko vumbi, kuwekeana mafta ya taa ktk chakula, kuchambia godoro, kulamba sahani baada ya kula, kupiga passpot size, njuka mnyonge alibanduliwa au kunyonya rungu, kufunga mawe ktk mataulo kisha taa inazimwa dakika tano, muda wa kufunzana adabu, hii kila siku saa tano usiku, kupakana losheni, au kuvunjiwa yai ukilala kisha wanasingiziwa vibwengo, kuuza magodoro ya walioingia darasani wiki dume, godoro linabadilishwa na sahani ya wali maharage, mchaka mchaka saa kumi za usiku kisha mnafuata maji ya kuoga chini ya mlima..na mwisho tukachoma shule moto kisa hawakutupikia wali wiki mbili mfululizo....nilikuwa waziri wa chakula, kampani yangu walijaziwa kuliko maadui zetu, sisi chakula tulikuwa tukiweka katika ndoo ya lita 20 watu watano, tulikuwa wanafunzi 1200 lakini nyama inapikwa kilo kumi na tano tuu, hapo waziri wa msosi nachoma kilo moja na ikiiva najaza kisado, wengine wanakunywa supu...tulibadilishana wali kwa penzi....pamoja na yoote, darasani tulikuwa vizuri....mvua ikinyesha woote tulitoka nje uchi tukioga...kutokana na utukutu niliokuwa nao, pesa ya matumizi nilipewa buku na panadol tu, lakini nikirudi rikizo nilikuwa na zaidi ya laki tatu...
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Hakuna kitu watu walikuwa hawakipendi kama inspection ya kushtukiza tunaiita "shake off" balaa mnatingishwa balaa hadi kwenye matranka sasa ukute labda ulisahau kiroba au una picha za xx kazi unayo
 
Back
Top Bottom