BUSARA ZANGU
JF-Expert Member
- May 5, 2013
- 779
- 1,267
Asalam Aleikhum
Katika Maisha ambayo siwezi kuyasahau ni maisha ya Boarding. Maisha ya Boarding noma aliimba Jay Mo, moja kati ya wasanii waasisi wa Bongo Flavor.
Maisha ya Boarding ni moja kati ya maisha matamu lakini pia yenye changamoto nyingi. Kuna matukio na vimbwanga ambavyo vinatia chachandu katika Maisha ya Boarding.
Kuanzia kuingia shule ukiwa form 1 ni burudani tosha. Kwanza tuliitwa majina mengi sana, nyoka, Salamanda, njuka, soksi ya mlinzi n.k
Tulipigishwa simu chooni, tulichapwa mikanda usiku hasa tulipowasnitch watesaji kwa walimu. Aisee tuliooingia form 2 tukawa eti ma MP, na sisi ndio wababe dhidi ya Form 1...hataree.
Maisha ya Boarding bhana, tulikula ada, home walipojua ikawa msala wengine ilibidi kipindi cha kuchukua cheti tutafute hela kwa udi na uvumba ili tukakomboe ada tuliyokula.
Nakumbuka kipindi tunajiandaa kwenda shule baada ya likizo tulikuwa tunanunua mafuta ya kupikia na dagaa na viungo, tunachemsha huo mchanganyiko na tukifika shule duh.. hatari, kijiko kimoja cha mafuta kwa bakuli moja la maharage, waombaji sasa, weeeeengi, nyama ilikuwa mpaka ng'ombe wa shule augue.
Siku ya wali wengine ndio tulikuwa tunaoga hasa wale Tuliosoma maeneo yenye baridi. Kuna wakati tulikula ugali na sukari, sukari ni mboga wakuu sio mnashanga tena tamu kweli. Tukiandikiana barua na masela wetu wa shule nyingine, lazima ndani ya bahasha tuambatanishe punje mbili tatu za wali, watajuaje huwa tunakula wali.
Ukipoteza sahani usiwaze, kwa wali au uji utatumia ndoo unayoogea, kwa ugali utabeba mkononi na maharage utaweka kwenye kikombe chako cha uji.
Kuna wakati tulikuwa tunaenda jikoni kuiba upper layer au top layer pale msosi unapokaribia kuiva. Upper layer ni yale mafuta yanayoelea juu ya maharage, ukichanganya na maharage utamu wake sio wa nchi hii.
Kuoga haikuwa lazima. Boarding wengi ndipo walioojifunza kupiga Punyeto, a.k.a Puli. Nakumbuka kuna siku washikaji waliifanya mashindano nani atatoa wazungu haraka na mshindi alipatikana.
Kwa wapenda soka kulikuwa hamna namna unaweza kukosa Mechi za UEFA au za ligi za usiku. Kutoroka lazima, tukirudi tuna fegi mfukoni tukifika Shuleni tunampa mlinzi inakuwa sio kesi. Ikiwa zamu ya mlinzi mnoko tunatumia mbinu za kijasusi kuingia na kutoka eneo la shule.
Maisha ya boarding tulilima, tulifyeka, tulicheza. Kulikuwa na wasongo na wanafeli, halafu kulikuwa na wasongo na wanafaulu. Kubaki bwenini wakati wenzako wapo class ilikuwa kawaida sana, ila ukikutwa na bwana Pepsi shauri yako, yaani ni msala. Ila sisi wazoefu hatukukamatwa.
Muda wa prep a.k.a prepo hatukwenda class, tulisubiri usiku wa manane mtu atuamshe ndio tukasome hii ilikuwa sana sana wakati wa mitihani, tuliita msuli pepa.
Dah siku ya kuondoka school baada ya mitihani ya kitaifa kuisha ilikuwa very sad day. Wa mbeya walikwenda, wa Dar walikwenda, wa Morogoro walikwenda, wa Dodoma, wa Arusha. Kweli boarding school inakutanisha watu kutoka kila kona ya nchi.
I bet waliosoma day schools hawakupata hii informal education katika shule walizosoma.
Waliosoma maisha boarding tiririka your experience.