Vituko vya Maisha ya Boarding, Tukumbushane Tuliosoma Huko

Vituko vya Maisha ya Boarding, Tukumbushane Tuliosoma Huko

Bro uliishi luthuli au Lumumba....Enzi za akina Paul Nonga (wa Lipuli) Bwiru iliogopwa kwa kandanda safi....Wadada wa ngaza waliwakubali sana wana wa uboizini afu wale wa Bwiru girls waliwakubali masela wa nsumba. .....Kwenda kuogelea ziwani na kupanda kimlima kuchungulia wadada wa Bwiru Girls..Kula dagaa za kukaangwa za huko mnarani...zimbo tenkin, .....Those days Kisuu akiwa head....Bila kukusahau gari maarufu lilipaki pale karakana ikiitwa CHUNGA MAISHA
nilikua Lumumba mkuu,Nonga nimecheza nae sana mpira timu ya shule
 
kule tulipokua tunaenda kuwachungulia madada wa girls tulipaita mombasa,watu walinunua mpaka binocular ili wa zoom in kwa urahis
Yeah mombasa....Kuna kipindi maji yalikua ya shida ikawa n mwendo wa kwenda beach....wachache walienda hii ya huku chini miembeni (kilipo chuo cha mipango sasa) ila wengi ilikua n kule chini tupate na wasaa wa kwenda mombasa
 
Longido sec.
Nilipofika tu, hata sikumaliza dakika tano ndoo ikawa imeshaibiwa na sikuwahi kuiona tena.
Huko ndiko nilipokutana na maandazi ya chumvi
Shida ya maji usipime.
Vyoo vichafu kinoma watu wanaoga na kutoa haja kubwa maporini.
Yaani tulikuwa tunaoga maporini, wanawake wa kimasai wanapita wanachunga ng'ombe wao sisi hata hatuna time nao. Tunasema mmasai sio mtu kwa hiyo hakuna haja ya kuona aibu. Basi wanaume wao wakaenda kutusthaki kwa mkuu wa shule, eti tunawatega wake zao.
😀😀😀😀
 
Kuna mchizi alikuwa muhuni Sana sijui alifanya kosa gani alipewa adhabu ya kudeki choo cha shule alienda kudeki kwa mikono mwalimu alivyoona vile ilibidi amuambie asifanye tena hiyo adhabu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dah wale wa mbeke mitaa ya rwangwa tukutane hapa

Haielezeki, japo utamu ulikatishwa mwisho kabisa form six wadau tukapigwa paa had paper

LKN kileji nzima walitujua na walitufanya km watoto wao,

Loh bwenini kutamu sanaaa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nakumbuka tulikuwa tunasoma na Mmasai mmoja hivi shule ya sekondari moringe, alikuwa anajifanya mbabe, tukaenda Monduli Mjini tukanunua kufuli aina ya solex moja matata, ile tumepiga mbonji mwenzetu mmoja akachukua kufuli na kulibana kwenye sikio lake, asubuhi bweni zima tukawa wa kwanza kutoka na kumwacha mshikaji akiwa peke yake bwenini, tumekaa kidogo tukaona vumbi tu nje jamaa anakuja mbio huku shingo imekaa upande kwa uzito wa kufuli, kila mmoja akaanza kutafuta upenyo wake maana tukajua damu itamwagika kwa hasira alizokuwa nazo yule Mmasai, basi akashinda na kufuli siku nzima maana hakuna aliyethubutu kusema nani ana funguo wa wa lile kufuli, ile tumepiga mbonji mwenzetu mmoja akachukua funguo akampenyezea kwenye blanketi lake, kufika asubuhi hamadi anakuta funguo, lakini aliyeuweka hakumjua hadi tunamaliza maana angemjua damu ingemwagika kwa hasira alizokuwa nazo yule Mmasai,
hahah..apo apo Moringe pale dox ndo nilikua nakaa...alikuepo masai mwingine nae shamba shamba kweli...tulikua tu aunganisha unganisha sana kwenye lile dom almanusura liunguege....maana kwenye dari tulikua tumeunganisha system za kuwekea chaja...kulikua na ita mbili na pasi mbili...siku wametuotea asee Ndooki na camp yake walitutembezea kichapo sitasaau...nakumbuka niliruka kwata nusu saa baada ya kuwa nishapiga pushapu za kutosha na baadae tukazunguka uwanja mara saba...kesho yake nilishindwa kushuka zile ngazi za nnje...wengi tulishuka kwa mataka...matako yenyew yalikua mekundu kwa stick....basi bhn siku moja tumeweka ita kwenye ndoo tunachemsha maji na tukayaweka juu ya kitanda...yule masai akaja tukamwambia aangalie maji kama yamepata moto....asee jamaa alifurukuta pale..yale maji yalisambaa vitanda vyote vya juu...kitanda akakirusha huko....basi kuanzia hiyo siku akiona maji yamewekwa pale hata kusogelea
 
kagango pale tumefika tu 5 tukajisaau na sim zetu...asee siku wamepiga inspection walizikusanya na mandoo...kwa jinsi walivokua wengi wakashindwa kuwafukuza...tulichimba visiki ivo vya mikaratusi asee...mwishowe zile sim wakasema hawatorudisha mpaka tumalize...imagine tupo 5 alafu unaambiwa sim utarudishiwa siku ukimaliza...kweli bhn sim zilikaa miaka miwili bila kuwashwa...tunamaliza six ndo tunapewa...zingine zishaota kutu zingine ata aziwakagi tena
Hakuna kitu watu walikuwa hawakipendi kama inspection ya kushtukiza tunaiita "shake off" balaa mnatingishwa balaa hadi kwenye matranka sasa ukute labda ulisahau kiroba au una picha za xx kazi unayo
 
mchezo wa kuibiwa ndoo ulikuwa kwa shule nyingi...mimi mwenyew nimeripoti pale Moringe hata siku aikuisha ndoo sikuionaga tena mpaka namaliza
Longido sec.
Nilipofika tu, hata sikumaliza dakika tano ndoo ikawa imeshaibiwa na sikuwahi kuiona tena.
Huko ndiko nilipokutana na maandazi ya chumvi
Shida ya maji usipime.
Vyoo vichafu kinoma watu wanaoga na kutoa haja kubwa maporini.
Yaani tulikuwa tunaoga maporini, wanawake wa kimasai wanapita wanachunga ng'ombe wao sisi hata hatuna time nao. Tunasema mmasai sio mtu kwa hiyo hakuna haja ya kuona aibu. Basi wanaume wao wakaenda kutusthaki kwa mkuu wa shule, eti tunawatega wake zao.
😀😀😀😀
 
wazee wa kagango...muda wa prepo tupo twn mtaani na wasubi tunazunguka kwenye magheto ya wana wa saloon...nakumbuka tulikua tunaingia vijijini nfsni uko kufata tu sherehe...yaani isisikike tu sauti ya mziki unajua hapo lazima kutakuwa na mpunga...ilikua aijalishi ni sherehe au msiba vyote kwetu ilikua sherehe...basi tutatembea huko hadi nyamililo...nakumbuka tulikuq tunatoboa hadi uku karebezo karibu biharamulo sekondari...na hapo ni mtu alituambia kuna.part na tukalikosa...iyo.sku tulilaani basi tu
 
Asalam Aleikhum

Katika Maisha ambayo siwezi kuyasahau ni maisha ya Boarding. Maisha ya Boarding noma aliimba Jay Mo, moja kati ya wasanii waasisi wa Bongo Flavor.

Maisha ya Boarding ni moja kati ya maisha matamu lakini pia yenye changamoto nyingi. Kuna matukio na vimbwanga ambavyo vinatia chachandu katika Maisha ya Boarding.

Kuanzia kuingia shule ukiwa form 1 ni burudani tosha. Kwanza tuliitwa majina mengi sana, nyoka, Salamanda, njuka, soksi ya mlinzi n.k

Tulipigishwa simu chooni, tulichapwa mikanda usiku hasa tulipowasnitch watesaji kwa walimu. Aisee tuliooingia form 2 tukawa eti ma MP, na sisi ndio wababe dhidi ya Form 1...hataree.

Maisha ya Boarding bhana, tulikula ada, home walipojua ikawa msala wengine ilibidi kipindi cha kuchukua cheti tutafute hela kwa udi na uvumba ili tukakomboe ada tuliyokula.

Nakumbuka kipindi tunajiandaa kwenda shule baada ya likizo tulikuwa tunanunua mafuta ya kupikia na dagaa na viungo, tunachemsha huo mchanganyiko na tukifika shule duh.. hatari, kijiko kimoja cha mafuta kwa bakuli moja la maharage, waombaji sasa, weeeeengi, nyama ilikuwa mpaka ng'ombe wa shule augue.

Siku ya wali wengine ndio tulikuwa tunaoga hasa wale Tuliosoma maeneo yenye baridi. Kuna wakati tulikula ugali na sukari, sukari ni mboga wakuu sio mnashanga tena tamu kweli. Tukiandikiana barua na masela wetu wa shule nyingine, lazima ndani ya bahasha tuambatanishe punje mbili tatu za wali, watajuaje huwa tunakula wali.

Ukipoteza sahani usiwaze, kwa wali au uji utatumia ndoo unayoogea, kwa ugali utabeba mkononi na maharage utaweka kwenye kikombe chako cha uji.

Kuna wakati tulikuwa tunaenda jikoni kuiba upper layer au top layer pale msosi unapokaribia kuiva. Upper layer ni yale mafuta yanayoelea juu ya maharage, ukichanganya na maharage utamu wake sio wa nchi hii.

Kuoga haikuwa lazima. Boarding wengi ndipo walioojifunza kupiga Punyeto, a.k.a Puli. Nakumbuka kuna siku washikaji waliifanya mashindano nani atatoa wazungu haraka na mshindi alipatikana.

Kwa wapenda soka kulikuwa hamna namna unaweza kukosa Mechi za UEFA au za ligi za usiku. Kutoroka lazima, tukirudi tuna fegi mfukoni tukifika Shuleni tunampa mlinzi inakuwa sio kesi. Ikiwa zamu ya mlinzi mnoko tunatumia mbinu za kijasusi kuingia na kutoka eneo la shule.

Maisha ya boarding tulilima, tulifyeka, tulicheza. Kulikuwa na wasongo na wanafeli, halafu kulikuwa na wasongo na wanafaulu. Kubaki bwenini wakati wenzako wapo class ilikuwa kawaida sana, ila ukikutwa na bwana Pepsi shauri yako, yaani ni msala. Ila sisi wazoefu hatukukamatwa.

Muda wa prep a.k.a prepo hatukwenda class, tulisubiri usiku wa manane mtu atuamshe ndio tukasome hii ilikuwa sana sana wakati wa mitihani, tuliita msuli pepa.

Dah siku ya kuondoka school baada ya mitihani ya kitaifa kuisha ilikuwa very sad day. Wa mbeya walikwenda, wa Dar walikwenda, wa Morogoro walikwenda, wa Dodoma, wa Arusha. Kweli boarding school inakutanisha watu kutoka kila kona ya nchi.

I bet waliosoma day schools hawakupata hii informal education katika shule walizosoma.

Waliosoma maisha boarding tiririka your experience.
mimi nakumbuka matukio mengi sana, siku moja ilipigwa inspection ya ghafla tumetoka prepo tumepiga story wee waliolala wakalala saa saba hivi tuliokua macho tukaona second apatron pamoja na waalimu watatu wamekuja tukaamshwa wote kila mtu asimame kwenye loka lake pamoja na tranka lake, asee vilishikwa vitu vingi sana, simu za kutosha, jamaa mmoja alishikwa na hirizi na kibuyu akapewa suspension, mshkaji wangu mmoja akakutwa na pakti mbili za kondom akaulizwa hizi umetoa wapi, jamaa akasema nimepewa na baba yangu, baba yangu ananipenda sana anajali afya yangu, asee ilikua ni kicheko bweni zima. Akaambiwa aite mzazi, ila alikua anaishi na mzee wake tu hakua na maza, mzee alikua peace msala uliisha
 
Boarding hiyo ilikua teacher anakuja dom kutuamsha na fimbo saa 11 basi kuna mjinga mmoja alikua analala kitanda cha mwanzo karibu na mlango...teacher akiingia kwa kunyata jamaa anamsalimu kwa sauti ili kuamsha watu shikamoo mwalimu...asipojibu anarudia mwalimu nakusalimu,watu wanaamka tulikua tunalala na uniform....

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom