Vituko vya Maisha ya Boarding, Tukumbushane Tuliosoma Huko

Vituko vya Maisha ya Boarding, Tukumbushane Tuliosoma Huko

Kuoga haikuwa lazima. Boarding wengi ndipo walioojifunza kupiga Punyeto, a.k.a Puli. Nakumbuka kuna siku washikaji waliifanya mashindano nani atatoa wazungu haraka na mshindi alipatikana
Hii ni laana
 
Katika matukio yote ya bweni sitosahau la mwanafunzi(kiongozi wa nidhamu) kumtandika fimbo mwanafunzi mwingine mbele ya wanafunzi wote wa bweni.

Mwamba (mchapwa) alikuwa mdokozi
 
Nilivuna sana asali kwenye mizinga ya shule,ikawa ni mwendo wa kunywa asali na uji wenye asali nyingi,
Niliipigia hesabu mizinga ya shule imetundikwa porini ,nikashona suti ya makaratasi Yale meupe yanayotolewa kwenye magodoro mapya yani mikono mirefu ya tisheti nikaishonea kama gloves na shingoni nikashonea kama helment nkatoboa vitundu vidogo vya kupitisha hewa haha, nikitaka niweze kuvuna asali bila kutumia moto kama nnavoonaga kwenye tv, nyuki washenz kweli usiombe wakung'ate wengi Kwa pamoja yani haha,
Basi siku ya tukio nimetegea saa tatu usiku watu wako prepo nikachkua ndoo na tochi nikazamia zangu porini guess what,!
Ile nimefungua tu mzinga nyuki walitoka kibaao apo full najiamini najua nmevaa suti nyuki hapiti, Ile nimegusa Sega moja sijui walipatia wapi upenyo nilistukia nimeng'atwa kama nyuki Tano kwa pamoja daadek ,kufurukuta ni kama walikua wananiona walining'ata wengi ikabidi nirudishie mfuniko upesi nikarukia kugalagala kwenye nyasi daah nilibeba ndoo yangu na sega nusu nkarudi bweni kuuguza maumivu,
Kesho yake mwanang Kaniona na nundu nkamweleza kilichonikuta kanicheka wee ila kanifundisha mbinu ya kuvuna asali iliofanya tusiwai kufikiria kununua au kuomba sukari ya uji,
Tulitengeneza Mwenge wa vijiti vikavu vya porini kisha juu nazungushia majani mabichi ,ukija kuwasha vile vijiti na majani mabichi yakiungua yanatoa Moshi mwingi kama bomu la machozi ,
Tena kwenda kwenye mzinga suruali inakunjwa adi magotini nnavua shati alaf mikono natembea nmeitanua kama wababe wanavyotembeaga,
Tuliivuna mzinga mmoja tkatia kwenye ndoo kesho yake ni burudani, kilichofuata mizinga karibu yote nilipita nayo
Mpaka namaliza shule a2jawai kustukiwa nkarudi mtaani na ujuzi wa kurina asali ila sjawai kudhubutu kuipiga ya uraiani
,iyo ilikua ni mkoa wa songwe uko
 
Back
Top Bottom