Raia Fulani
JF-Expert Member
- Mar 12, 2009
- 11,866
- 4,262
yuko wapi mtikila? Kitoweo hicho kimekileta, baba mchungaji.
Ndugu yangu Mtanzania,Mkuu Sikonge,
Ukiamini haya maneno ya Vincent basi utaamini utumbo wowote wa wanasiasa.
Kwanza kafanya makosa makubwa kwenye timeline. Nyerere alifariki 1999 wakati prof. Mwakyusa alipewa uwaziri mwaka 2006 tena na rais Kikwete na wala sio rais Mkapa.
Mkapa kasema hamtambui Vincent kama mtoto wa JKN, ilitosha Vincent kujibu yeye JKN ni babake mdogo/mkubwa. Haya yote ni matokeo ya watu mbalimbali kujifanya walikuwa karibu na JKN wakati ukweli si ajabu ni tofauti sana.
Kwa kuingiza kifo cha Nyerere kwenye siasa za uchaguzi, tayari ameiingiza familia nzima ya Nyerere kwenye hili na hao wengine itabidi waseme.
Tusiwe wajinga kiasi hicho cha kuweza kuamini kila ugonjwa ni mkono wa mtu. Nilikuwa hapa London wakati Nyerere anafariki na siwezi kuamini nchi ina watu wajinga kiasi hicho cha hata kuanza kufikiria kwamba JKN aliuwa na njama.
Nilifikiri Mtikila ni kichaa pekee, kumbe tuna hata wabunge ambao ni wajinga kiasi hiki? Hizi hisia za mkono wa mtu kwenye kila jambo zitatupeleka pabaya. Tutajenga taifa la waabudu Kikombe cha Babu na mwisho wake ni kuangamia maana hatutafanya tahadhari yoyote kwenye mambo yanayotusumbua hapa duniani.
Huyo Vincent inaelekea hata knowledge ya cancer hana.
Nakubaliana na hoja zako ila nakupinga kwa hili kuwa Kifo cha Mwalimu JK hakina umuhimu kwa msemo huu 'Siasa ni uteleze nipate nafuu, dodondoka niinuke'. Mkapa ameteleza anapaswa kutelezeshwa adodondeke akose la kunena; abaki akijitetea au kujisafisha!Mshaurini Vicent Nyerere aachane na hizo siasa. Hoja kuu ambayo alitakiwa kuisimamia ni kwamba Vicent Nyerere hajawahi ku-claim mahali popote pale kwamba yeye ni mtoto wa Marehemu Mwalimu Nyerere. Kwa hiyo, claim ya Mkapa ilikuwa baseless na haiwezi ku-hold maji na hizo ndio siasa za maji taka, watu wanaacha hoja halafu wanakijita kwenye kuzua vijambo na vijimambo.
Discussion za chanzo cha kifo cha Mwalimu Nyerere kwa sasa haziwezi kuwasaidia CHADEMA ili washinde huko Arumeru Mashariki. Mjadala huo kwa sasa hauna msaada wowote kwa wananchi wa Arumeru ambao wana matatizo ya Ardhi na Maji, pamoja kukosekana kwa ajira kwa vijana.
Focus ya Kampeni ya CHADEMA iwe ni kwenye kero za wananchi wa Arumeru. Ili kumgonga vilivyo Mkapa na Chama chake, matatizo ya maji na ardhi hayajaanza leo wala juzi, yapo kwa miaka mingi sasa. Je, Mkapa akiwa Rais ina maana hakuyajua hayo matatizo, kama aliyajua, kwanini hakuyashughulikia? Kikwete yuko madarakani mwaka wa 7 sasa, je hajapelekewa hayo matatizo au hajui hayo matatizo? Je, wananchi watakuwaje na imani kwamba Mkapa akienda kumwambia Kikwete matatizo ya maji na adhi atayatatua na ilihali amekuwa madarakani kwa miaka 7 na matatizo yako pale pale?
Iwapo Mzee Sumari (RIP) alishindwa kusaidia kutatua matatizo ya Arumeru Mashariki akiwa Naibu Waziri wa Fedha (sehemu ya serikali ya chama tawala), je leo hii mwanae ndio ataweza kuyatatua? CCM kimebaki kuwa ni chama cha kuweka ahadi hewa bila kutimiza. Hapo ndio CHADEMA inatakiwa kusimamia kwa kuwa ndo ukweli wenyewe na wananchi wanajionea. Wakumbusheni kwamba hata Igunga ambako CCM walishinda uchaguzi mdogo, zile ahadi zote za CCM zilizotolewa kwa wana Igunga ikiwemo ya kujengewa daraja hazijatimizwa hata moja!
Mtanzania,
Nimefuatilia sana uzi huu na kwa kiasi kikubwa nakubaliana na baadhi ya hoja zako. Lakini swali langu, kwa nini unatetea sana uwezekano kwamba kunawezekana kukawa na jinai katika kifo cha Nyerere? Inaelekea una uhakika kabisa kwamba Nyerere hakuuawa, sasa unaonaje utupe facts na si mtazamo kwamba Nyerere hakuuawa? Kwa kuwa unatumia uelewa wa kawaida tu kwamba Nyerere hakuuawa, basi usiondoe kabisa speclulation kwamba Nyerere aliuawa!
Hoja zote zina mashiko: kwamba Nyerere alikufa kwa kansa ni asilimia 50 lakikini kwamba pia aliuawA ni asilimia 50!
wewe bwana mdogo tumia akili yako! Watu wanakwenda na facts na kuunganganisha dots na sio kusikiliza Makongoro amesema nini. Kwani Makongoro akisema hakuuawa ndio hakuuawa kweli? Hata huyu Vicent watu wanampongeza kwa sababu wameweza kuunganisha tukio la mauaji na maneno yake. Piga huyo Mkapa huyo ...piga mawe.... fisadi huyo... choma moto ... loweka kwenye petrol hilo jambazi la epa hilooooo!!!!!!Vincent joseph kiboko nyerere hujatutendea haki watz, tuthibitishie ushiriki wa mkapa ktk kumuua mwalimu na usimungúnye lolote, hatupendi unafiki wa mwakyembe,,,, kauli nyepesi tu ya mkapa kujiuliza ni nani huyu vincent nyerere imekuwa nongwa mpaka unalihadaa taifa kwa sumu chafu prof. Mwakyusa aliingia bungeni, 2000 uwaziri kapewa na jmk je ni wapi mkapa amemhonga uwaziri daktari wa nyerere..... Ni hatari kwa politician kijana na aina yake kuja na general accusation tena kumhusu muasisi wa taifa hili vs kiongozi mmojawapo wa warithi wake!!!! Sijapendezwa na tabia za ulevi wa sifa kwa gharama ya uzushi wa hatari, itakuwaje makongoro mwenye babake akija arumeru na katofautiana na vincent!!!!! Akija na madaraka na rose nini hatima ya vincent na cdm!!! This is ccm of all wana jf....tusishangilie uchanga wa vincent....
Watoto wote wa tumbo moja na Mwl. majina yao yalikuwa JKNNa Kiboko ndiye Josephat. Baba yake Vincent na Gerald.
Haaa haa haaa loooooooser wa kura ya maoni anajaribu kuripea madonda yake.....bwaa haa haa haaMkuu Nyumbu-,
Lengo ni kuelemishana na wakati huo huo inabidi tukemee hii tabia inayojengeka miongoni mwetu sisi Watanzania kwamba kila kitu ni mkono wa mtu. Madhara yake hatujifunzi na tunaendelea kuangamia hata kwa mambo ambayo ni uzembe wetu tu.
Binafsi sioni fouls zozote juu ya uhai wa JKN kwenye mjadala wote huu, Si umeona hata Jasusi anasema hata Marekani waligundua ugonjwa wa JK miaka miwili kabla ya kulazwa UK? Pia sioni motive ya eti Mkapa aamue kumwua Nyerere?
Kikubwa, pamoja na kutokuwaamini Waingereza wanavyoshughulikia matatizo ya dunia nje na nchini kwao, nina waamini inapokuja kushughulikia haki ya mtu akiwa ndani ya mipaka yao. Wanaweza kufanya madudu mengi sana wakiwa nje ya nchi yao lakini sio wakiwa ndani. Ukiwa ndani haki yako inalindwa na vyombo vingi sana. Nitakuwa wa mwisho kuamini mtu kama Nyerere atalazwa kwenye hospitali ya serikali zaidi ya miezi mitatu na kugundulika kuna fouls na wataficha. Sio rahisi sana mkuu kwasababu ukiwa kazini huwezi kumwamini hata rafiki yako inapokuja masuala ya uhalifu, inabidi ulinde usalama wako, hivyo sio rahisi kufichiana siri kiasi hicho.
Jackson Manyerere hatoki ukoo wa Burito alitunzwa tu na kukulia ikulu kwa Nyerere baadaye kuwa mwandishi wa habari.Watoto wote wa tumbo moja na Mwl. majina yao yalikuwa JKN
1.Julius Kambarage Nyerere,
2.Joseph Kizurira Nyerere
3. Josephat Kiboko Nyerere!.
Ila Chifu Burito alikuwa na mke zaidi ya mmoja na mama Nyerere alikuwa mke mdogo. Kwa baba kina Nyerere wako wengi hata mpiganaji Jackson Manyerere ni ukoo huu. Jee watoto wengine wa Chifu Burito ni kina nani?.
Mkuu Mtanzania, humu jukwaani tuna tabia ya kuwa carried over na cinspiracy theories on almost everything!. Kwenye issue ya Dr. Mwaki nimewaeleza sio vibaya watu wangejua alikuwa anasumbuliwa na nini kabla ya issue ya kitaulo na alitumia dawa gani na kwa muda gani na hizo dawa zina side effects gani!. Watu wamekazania conspiracy theory ya kutiliwa sumu tuu!. Sasa hii cobspiracy theory dhidi ya kifo cha Mwalimu, basi sasa itageuka wimbo!.Mkuu Nyumbu-,
Lengo ni kuelemishana na wakati huo huo inabidi tukemee hii tabia inayojengeka miongoni mwetu sisi Watanzania kwamba kila kitu ni mkono wa mtu. Madhara yake hatujifunzi na tunaendelea kuangamia hata kwa mambo ambayo ni uzembe wetu tu.
Binafsi sioni fouls zozote juu ya uhai wa JKN kwenye mjadala wote huu, Si umeona hata Jasusi anasema hata Marekani waligundua ugonjwa wa JK miaka miwili kabla ya kulazwa UK? Pia sioni motive ya eti Mkapa aamue kumwua Nyerere?
Kikubwa, pamoja na kutokuwaamini Waingereza wanavyoshughulikia matatizo ya dunia nje na nchini kwao, nina waamini inapokuja kushughulikia haki ya mtu akiwa ndani ya mipaka yao. Wanaweza kufanya madudu mengi sana wakiwa nje ya nchi yao lakini sio wakiwa ndani. Ukiwa ndani haki yako inalindwa na vyombo vingi sana. Nitakuwa wa mwisho kuamini mtu kama Nyerere atalazwa kwenye hospitali ya serikali zaidi ya miezi mitatu na kugundulika kuna fouls na wataficha. Sio rahisi sana mkuu kwasababu ukiwa kazini huwezi kumwamini hata rafiki yako inapokuja masuala ya uhalifu, inabidi ulinde usalama wako, hivyo sio rahisi kufichiana siri kiasi hicho.
Ni daktari gani huyo aliyenyamazishwa kwa kupewa uwaziri?
mwalimu hakupenda kutibiwa london (st thomas)....mzee alikataa kabisa na nakumbuka siku hiyo butiama mkapa alipokwenda kumsalimia mwalimu...mwalimu hakupokea mkono wala salamu ya mkapa....mwalimu alimuuliza swali moja mkapa'' leo ndo umejua kuwa ninaumwa?......mkapa akajitetea kuwa alikuwa na kazi nyingi akaongeza kwa kusema nimepanga utaratibu ukatibiwe london...mwalimu akakataa kabisa ..mkapa akasisitiza mwalimu akagoma...ndipo binti zaek mwalimu wakaingilia kati kumshauri mzee...mwalimu alitaka kwenda new york maana mwaka 1998 alikwenda huko na kufanya chek up na afya yake ilikuwa safi ....
siku anakwenda wingereza pale uwanja wa ndege mwalimu alikuwa mwenye nguvu za kutosha na bada ya kuongea na waandishi wa habari alipanda ngazi za ndege akiwa anakimbia na alipofika pale juu aligeuka na kuwapungia mkono watz....
wakati mwalimu anapelekwa wingereza hiyo hosp haikuwa specialized kwenye magonjwa hayo.....halafu ni kwa nini hawakumpeleka hosptila moja kwa moja bada yake wakamuweka hotelini hadi alipozimia ndo wakampeleka hapo st.thomas?......
mkuu ''mtanzania hili swala la ugonjwa wa mwalimu naomba niseme kuwa hulijui kwa undani......kifo cha mwalimu kilijaa utata sana...halafu hivi unajua ni kwa nini kingunge alikwenda london?
Hilo jina la Nyerere kalipata wapi?. Nimeuliza ndugu wa Nyerere kwa baba ni kina nani?.Jackson Manyerere hatoki ukoo wa Burito alitunzwa tu na kukulia ikulu kwa Nyerere baadaye kuwa mwandishi wa habari.
Hivi, wewe Gembe ungejibuje kama uhalali wa familia yako ungeshukiwa na kiongozi wa taifa?-Tatizo lako umeathiriwa na Ujinga,nimehitimisha kwa kusema sijui....sijaeleza sijui nini naona umekurupuka tu...
-Wewe ndiyo hujui ,unalazimisha watu kulishwa ***** kwa faida ya wachache..
-Naungana na Mkuu Mtanzania kuwa vicent amepotoka na alitakiwa kujibu alichokisema Mkapa..
-Kaibua hoja ambayo haiwezi na Hana mamlaka ya kuzungumzia kifo cha JKN!
Asante Jasusi, kuna watu hata ukweli wakikutana nao uso kwa uso wataukana kwani wameifanya migumu mioyo yao. Kifo cha Mwalimu hakikutangazwa mara moja ili watu wa aina hiyo watayarishwe kisaikolojia kuupokea uwongo. Na kweli wakanasa na kuanza kutumiwa na wahusika katika harakati zao za kuuzika ukweli. Kuuzika ukweli? Hiyo nawaambia haitawezekana na haijawahi kuwezekana hata kwa dawa, ukweli hautakubali uzikwe hivi hivi.Ndugu yangu Mtanzania,
Nakupa ushauri kidogo tu. Do not rush to judgement. Sometimes the truth is more stranger than fiction. Waswahili wana msemo usichokijua ni kama giza nene. Ni hayo tu kwa sasa.
Haaa haa haaa loooooooser wa kura ya maoni anajaribu kuripea madonda yake.....bwaa haa haa haa
Mkuu Kingunge alikuja kupelekwa kudhibiti flow of information baada ya mwanafamilia mmoja kuongea na waandishi wa habari kule Uingereza na kusema kutoridhishwa na treatment (sio ya madaktari) nzima aliyofanyiwa Nyerere, ila wakati huo tulikuwa tunaambiwa alikuwa haongei nafikiri ilipita kama wiki hivi wanaficha.Mkuu,,tafadhali acha tu yamwagike,naomba weka wazi sababu ya kile kibabu Kingunge kusafiri tufahamu,,what I know Mwl siku anaondoka kwenda UK alikuwa mzima,nilikuwa mmoja ya waliosindikiza msafara wake hata kabla hajapanda ndege alikaa VIP lounge Terminal One pale akiongea vizuri tu hata akisema msihofu ni "check up" tu ya afya