Mkuu Sikonge,
Ukiamini haya maneno ya Vincent basi utaamini utumbo wowote wa wanasiasa.
Kwanza kafanya makosa makubwa kwenye timeline. Nyerere alifariki 1999 wakati prof. Mwakyusa alipewa uwaziri mwaka 2006 tena na rais Kikwete na wala sio rais Mkapa.
Mkapa kasema hamtambui Vincent kama mtoto wa JKN, ilitosha Vincent kujibu yeye JKN ni babake mdogo/mkubwa. Haya yote ni matokeo ya watu mbalimbali kujifanya walikuwa karibu na JKN wakati ukweli si ajabu ni tofauti sana.
Kwa kuingiza kifo cha Nyerere kwenye siasa za uchaguzi, tayari ameiingiza familia nzima ya Nyerere kwenye hili na hao wengine itabidi waseme.
Tusiwe wajinga kiasi hicho cha kuweza kuamini kila ugonjwa ni mkono wa mtu. Nilikuwa hapa London wakati Nyerere anafariki na siwezi kuamini nchi ina watu wajinga kiasi hicho cha hata kuanza kufikiria kwamba JKN aliuwa na njama.
Nilifikiri Mtikila ni kichaa pekee, kumbe tuna hata wabunge ambao ni wajinga kiasi hiki? Hizi hisia za mkono wa mtu kwenye kila jambo zitatupeleka pabaya. Tutajenga taifa la waabudu Kikombe cha Babu na mwisho wake ni kuangamia maana hatutafanya tahadhari yoyote kwenye mambo yanayotusumbua hapa duniani.
Huyo Vincent inaelekea hata knowledge ya cancer hana.
Aliyeanzisha hili zali ni Mkapa mwenyewe ,wananchi wengi tumekuwa tukidadisi hata humu JF kuna thread imetembea sana kuulizia nini haswa kilimuua Mwalimu,Leukemia inaua lakini sio abruptly kama ilivyokuwa kwa mwalimu, Mkapa aeleze wananchi alimfanya nini Mwalimu ni swali halijaanza kwa Vicent magezeti, mitandao na hata watu binafsi tumejiuliza ni wakati wa MKapa kutueleza ,Vicent sio mjinga