Mtanzania,
Umesahau kwenye ile press conference ya Nyerere baada ya kuandika kile kitabu chake?
Alimchambua Mwinyi vibaya sana na hata kufikia kusema "Rais gani anaongeza na maamuzi ya nchi yanafanyika kitandani?" Baada ya hapo akamuangukia na Malecela kuwa HAFAI. Mwinyi aliendelea kupewa maneno yake kuwa "Hafai kuwa Rais na ni mdhaifu sana. Ila kuondoa Rais madarakani, inaleta mkosi kwenye nchi na tumvumilie tu amalize muhula wake wa pili."
Nafikiri kwa Mkapa, ninaweza kuanza kuamini kuwa alitaka kumzuia asigombee tena mara ya pili. Mkapa kwa kujua gomvi zao huko mwanzo ambazo unaona kabisa zilikuwepo, akalijua hilo na akaamua KUSAIDIA KIFO kwa kuzembea JKN kutibiwa au kwa kumuwahisha huko mbele ya hukumu.
Sijui ni sababu zipi zilimfanya JKN amuweke Mwinyi kuwa Rais ila kwa Mkapa, kila mtu alikuwa anajua historia ya Mkapa na Nyerere na hadi watu kuja kumwita mtoto wa JKN. Nyerere akamwita Mr. clean atakayekuja kusafisha Tanzania. Alimpamba sana mtoto wake na kila mtu aliamini hivyo kwa muhula wa mwanzo. Ila Mkapa aliponogewa madaraka, akaanza kuvimba kichwa na kuanza kivyake ukichukulia, Nyerere alimpa hadi kofia ya Mwenyekiti wa CCM.
Kama ilifika wakati Nyerere analalamika nje juu ya uuzaji wa Nchi unaofanywa na Mwanae Mkapa, basi kuna sehemu walikuwa wameshakosana vibaya sana. Kumbuka Mtanzania wanasema "there is a very thin line between LOVE and HATE. ukiteleza kidogo tu, love hugeuka kuwa hata uuwaji.
Mwinyi hayo mapenzi na Nyerere sidhani kama yalikuwa makubwa kiasi hicho na ukichukulia kuwajibika kwa Mwinyi miaka ya kuhamisha wananchi kwenye vijiji vya ujamaa huko Shinyanga.
All in all, VN awe kasema kweli au uongo, hii kitu imemuharibia sana Mkapa. Hata ajitetee vipi, kuna sababu nyingi sana zinanzoweza kuwafanya watu wengi waamini kuwa Mkapa alihusika hata kama ni kwa UZEMBE. Na unajua kabisa kuwa kuna nchi, kutokuwa msaada kwa mtu ni kosa. Hata kama umempiga risasi, na kumwacha anakufa, basi watakuhukumu hata kwa kosa la kutokumsaidia mtu aliyeumizwa na risasi.
Mkapa pia ana madudu haya ya EPA, Makampuni ya umeme, kuuza nchi na mengine mengi ambayo inabidi apande kizimbani ayajibu. Sijali sana kama alimuuwa Nyerere au lahh ila nafahamu kuwa aliuza nchi yangu ya Tanzania. Hayo ya Nyerere atajuana na ndugu zake Nyerere akina Vincent Nyerere na wengine kama wataamua kuungana naye au kumkana, shauri lao wana ndugu kwa ujumla.