Vincent Nyerere ampa Mkapa vidonge stahiki

Vincent Nyerere ampa Mkapa vidonge stahiki

Hivi, wewe Gembe ungejibuje kama uhalali wa familia yako ungeshukiwa na kiongozi wa taifa?
Siwaelewi kabisa wanaomsakama na kumlaumu Vincent Josephat Kiboko Nyerere. He is a Nyerere for God's sake.
Tukubali kuwa Mkapa ndiye aliyekurupuka. Sasa wanamtafuta Makongoro awasaidie. Too late.
....kama Makongoro au yeyote katka familia atajitokeza kujibu hoja ya Vicent Nyerere namuomba anisaidie kujibu swali hili.
Nyerere alikufa kwa ugonjwa wa kansa ya damu (Chronic lymphocytic leukemia). Nina uhakika Makongoro hawezi kujibu maswali yanayouhusu huu ugonjwa na mgonjwa kufa ndani ya mwezi mmoja baada ya kufika London. - Hivi mwalimu alipelekwa London kufanyiwa check up for the first time? je, kabla ya hapo ni lini alifanyiwa check up? na je hawakuligundua hilo tatizo mapema na prognosis yake? walimpeleka London kufanya nini katika advanced stage ya ugonjwa ambayo prognosis yake inajulikana? (ushauri wa Prof Mwakyusa ulikuwa ni upi?) kwa nini hakufanyiwa mapema katika early stages ambapo prognosis yake ni better kuliko katka advanced stage ya mgonjwa kufa in less than one month.
 
Mkapa ameanzisha vita ya mawe while anaishi kwenye nyumba ya vioo,.
Siku zote muuaji haishii kumuua mtu mmoja hata kama aliua bahati mbaya; naamini hii dhambi ya kuuana ataiendeleza kwa yeyote yule coz alithubutu kuua bila uoga mtu wa karibu na mwenye heshima ya kimataifa.
 
....kama Makongoro au yeyote katka familia atajitokeza kujibu hoja ya Vicent Nyerere namuomba anisaidie kujibu swali hili.
Nyerere alikufa kwa ugonjwa wa kansa ya damu (Chronic lymphocytic leukemia). Nina uhakika Makongoro hawezi kujibu maswali yanayouhusu huu ugonjwa na mgonjwa kufa ndani ya mwezi mmoja baada ya kufika London. - Hivi mwalimu alipelekwa London kufanyiwa check up for the first time? je, kabla ya hapo ni lini alifanyiwa check up? na je hawakuligundua hilo tatizo mapema na prognosis yake? walimpeleka London kufanya nini katika advanced stage ya ugonjwa ambayo prognosis yake inajulikana? (ushauri wa Prof Mwakyusa ulikuwa ni upi?) kwa nini hakufanyiwa mapema katika early stages ambapo prognosis yake ni better kuliko katka advanced stage ya mgonjwa kufa in less than one month.

Mwalimu alikuwa mgonjwa hata kabla ya kwenda london, kutokana na ugonjwa huo ndo makosa ya Mkapa, ni kumwambia aende kutibiwa uingereza. London alienda kutibiwa sio kufanyiwa checkup. Ugonjwa nafikiri walikuwa wameugundua huko marekani mwaka mmoja kabla.
 
Asante sana wana chadema ,Kuna mambo mengi sana .Sasa cha muhimu ni kuwa na katiba mpya yenye kufanya mambo mengi ya siri yawe wazi ,ili tuwahukumu wote wahusika .walifikiri ,na wanaendelea kufanya mchezo sasa ,maji yakukua ya shigo.Tutayafuatilia haya hata kama watakuwa wazee sana ,lazima waende jela ,segadance lazima mkapa afike huko.
 
Mwalimu alikuwa mgonjwa hata kabla ya kwenda london, kutokana na ugonjwa huo ndo makosa ya Mkapa, ni kumwambia aende kutibiwa uingereza. London alienda kutibiwa sio kufanyiwa checkup. Ugonjwa nafikiri walikuwa wameugundua huko marekani mwaka mmoja kabla.
Wewe na familia yake yupi anajua zaidi wenyewe wanasema alienda kwa check up wewe unaleta u much know.
 
MkamaP,

Nimeipenda hii ya rais Mwinyi aliua Azimio la Arusha ambalo lilikuwa mtoto kipenzi cha Nyerere na Nyerere hakusema kitu.

Kuuza mashirika ya umma ndio kungemwogopesha Mkapa mpaka amwue Nyerere kwanza? Watanzania bwana kwa vijambo jambo tumo!
Mtanzania,
Pitia baadhi ya hotuba za Mwalimu baada ya kung'atuka. Kuna ile hotuba anasema walipokwenda Zanzibar wakarudi kimya kimya "watu wenye akili" tukajua kuwa Azimio limekufa. Mwalimu alisema. Lakini mbali ya kusema angefanyaje zaidi? Hii ya NBC na kuuzwa kiholela kwa mashirika ya umma ilimpa "mshtuko mkubwa.' Alijaribu kufanya awezalo kama retired President lakini usukani wa nchi ulikuwa unashikiliwa na mtu mwingine. Mwalimu did his best na nadhani ndiyo maana Watanzania hivi sasa wanaposikiliza hotuba zake wanamwelewa.
 
Mkapa kalikoroga ngoja alinywe mwenyewe, amezoea uropokaji huyo mwizi, haoni wastaafu wenzie wanavyopumuzika na kula mapensheni?

Kipindi kile wananchi wote wakimnyooshea vidole kwamba ni fisadi wa ANBEN na Kiwira, kila waandishi wa habari walipokuwa wakimwuliza kuhusu hizo kashfa za ufisadi, majibu yake yalikuwa ni kwamba AMESTAAFU MAMBO YA SIASA. Mpaka Masoud Kipanya alimchora kwenye katuni zake.

Baada ya kuona serikali ya JK imetuliza mawimbi na kwamba hazomewi tena kwamba ni FISADI, amejisahau na kujiona ni msafi sana. Yote hiyo ni kwa kuwa wanatuona kwamba waTanzania huwa tunasahau haraka sana madudu yao na leo anaenda kutamba na kuomba kura kwa niaba ya mafisadi wenzake!
 
Mshaurini Vicent Nyerere aachane na hizo siasa. Hoja kuu ambayo alitakiwa kuisimamia ni kwamba Vicent Nyerere hajawahi ku-claim mahali popote pale kwamba yeye ni mtoto wa Marehemu Mwalimu Nyerere. Kwa hiyo, claim ya Mkapa ilikuwa baseless na haiwezi ku-hold maji na hizo ndio siasa za maji taka, watu wanaacha hoja halafu wanakijita kwenye kuzua vijambo na vijimambo.

Discussion za chanzo cha kifo cha Mwalimu Nyerere kwa sasa haziwezi kuwasaidia CHADEMA ili washinde huko Arumeru Mashariki. Mjadala huo kwa sasa hauna msaada wowote kwa wananchi wa Arumeru ambao wana matatizo ya Ardhi na Maji, pamoja kukosekana kwa ajira kwa vijana.

Focus ya Kampeni ya CHADEMA iwe ni kwenye kero za wananchi wa Arumeru. Ili kumgonga vilivyo Mkapa na Chama chake, matatizo ya maji na ardhi hayajaanza leo wala juzi, yapo kwa miaka mingi sasa. Je, Mkapa akiwa Rais ina maana hakuyajua hayo matatizo, kama aliyajua, kwanini hakuyashughulikia? Kikwete yuko madarakani mwaka wa 7 sasa, je hajapelekewa hayo matatizo au hajui hayo matatizo? Je, wananchi watakuwaje na imani kwamba Mkapa akienda kumwambia Kikwete matatizo ya maji na adhi atayatatua na ilihali amekuwa madarakani kwa miaka 7 na matatizo yako pale pale?

Iwapo Mzee Sumari (RIP) alishindwa kusaidia kutatua matatizo ya Arumeru Mashariki akiwa Naibu Waziri wa Fedha (sehemu ya serikali ya chama tawala), je leo hii mwanae ndio ataweza kuyatatua? CCM kimebaki kuwa ni chama cha kuweka ahadi hewa bila kutimiza. Hapo ndio CHADEMA inatakiwa kusimamia kwa kuwa ndo ukweli wenyewe na wananchi wanajionea. Wakumbusheni kwamba hata Igunga ambako CCM walishinda uchaguzi mdogo, zile ahadi zote za CCM zilizotolewa kwa wana Igunga ikiwemo ya kujengewa daraja hazijatimizwa hata moja!

Wewe unaandika tu uliisoma hotuba ya Mkapa
 
Mwalimu alikuwa mgonjwa hata kabla ya kwenda london, kutokana na ugonjwa huo ndo makosa ya Mkapa, ni kumwambia aende kutibiwa uingereza. London alienda kutibiwa sio kufanyiwa checkup. Ugonjwa nafikiri walikuwa wameugundua huko marekani mwaka mmoja kabla.
Kwa nini hakumwambia mapema baada ya kuugundua huo ugonjwa Marekani? kwa nini alisubiri mpaka hatua ya kubaki mwezi mmoja kufa na ambapo Prof Mwakyusa alikuwa anajua prognosis?
 
Watoto wote wa tumbo moja na Mwl. majina yao yalikuwa JKN
1.Julius Kambarage Nyerere,
2.Joseph Kizurira Nyerere
3. Josephat Kiboko Nyerere!.

Ila Chifu Burito alikuwa na mke zaidi ya mmoja na mama Nyerere alikuwa mke mdogo. Kwa baba kina Nyerere wako wengi hata mpiganaji Jackson Manyerere ni ukoo huu. Jee watoto wengine wa Chifu Burito ni kina nani?.

Yupo marehemu Mzee William Butiku na Nyangeta.
 
Dear Mkapa,
Kwa nini umezima mshumaa wetu uliokua ukituangazia Nuru njema?
Kwa nini umebaka haki ya kuishi ya Muasisi wetu wa harakati za uhuru wa taifa letu??
Baba Mkapa, kwa mema aliyoyatenda Mwalimu JE! kifo ndo zawadi stahiki uliyoona ni bora kuliko zote duniani???
 
Kwa nini hakumwambia mapema baada ya kuugundua huo ugonjwa Marekani? kwa nini alisubiri mpaka hatua ya kubaki mwezi mmoja kufa na ambapo Prof Mwakyusa alikuwa anajua prognosis?

Kwahiyo una maana Mkapa anafahamu siku ya watu kufa? naomba nikuombe, nenda pale mhimbili ukikuta watu wanalia, wewe waulize kwanini mmesubili mwaka huu kumleta mgonjwa na mpaka amekufa?

Tatizo nafikiri tunajaribu kuhoji ambavyo ktk imani tumeambiwa na fumbo la imani. kama ulishauuguza, mgonjwa hata kama alikuwa haongei akikaribia kuuga dunia, huwa anapatwa na nguvu anaongea, anazurura hapa na pale na wauguzi mnapata faraja kweli lakini kesho yake mnakuta kisha aga dunia.
 
Nimepatwa na kizunguzungu,, hata sielewi tena kabisa... mambo mengine ni afadhali hata usiyafahamu,,
 
Mkapa kayataka mwenyewe, binafsi nilikuwa namheshimu sana. Hivi si apumzike nyumbani kwake kwa heshima badala kutukanana na kudhalilishana na vijana wa kizazi hiki wanaofahamu kila aina ya uovu wake, ni vile walikuwa hawajapata kichokoo ili wayaanike hayo maovu. Namhurumia sana maana siyo wakati wake.
 
Ha ha ha ha

Mkapa alimlazimisha Nyerere kwenda checkup? very silly
This is more than silly! Siasa za Tz. ni kama kucheza kamali...Nani asiyejua Mwl.aliugua na ilipaswa atibiwe na wote twafahamu alikuwa anaenda UK kwa matibabu sasa leo kumnyoshea mtu kidole kweli Watz. tuwe waoga na hizi tuhuma.
Mchafueni Mkapa kwa mambo mengine UFISADI na mapungufu mengine wakati na baada ya utawala wake, lakini hili kwa kweli mnamwonea. Asingempeleka UK kutibiwa lingezuka lingine. Jamani mungu yupo hizi dana dana tutaja jutia baadae.
 
Kwahiyo una maana Mkapa anafahamu siku ya watu kufa? naomba nikuombe, nenda pale mhimbili ukikuta watu wanalia, wewe waulize kwanini mmesubili mwaka huu kumleta mgonjwa na mpaka amekufa?

Tatizo nafikiri tunajaribu kuhoji ambavyo ktk imani tumeambiwa na fumbo la imani. kama ulishauuguza, mgonjwa hata kama alikuwa haongei akikaribia kuuga dunia, huwa anapatwa na nguvu anaongea, anazurura hapa na pale na wauguzi mnapata faraja kweli lakini kesho yake mnakuta kisha aga dunia.
Hujajibu swali. nimekuuliza baada ya kugundua ugonjwa Marekani kwa nini hakumpeleka kutibiwa? na akasubiri mpaka ikafika terminal stage?. Hata kama nikiwa Muhimbili nitahoji sababu za kumchelewesha mgonjwa iwapo ugonjwa ulijulikana mapema na ndugu walikuwa wanajua.
 
Back
Top Bottom