Vincent Nyerere ampa Mkapa vidonge stahiki | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Vincent Nyerere ampa Mkapa vidonge stahiki

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mgeni wenu, Mar 14, 2012.

 1. m

  mgeni wenu JF-Expert Member

  #1
  Mar 14, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 3,669
  Likes Received: 614
  Trophy Points: 280
  Wana JF leo katika viwanja vinne tofauti vya kampeni Mbunge wa Musoma Mjini ambae ndie Meneja Kampeni wa Arumeru Mashariki (Vincent Nyerere) amemjibu Mkapa kuwa.

  Aache unafiki wa siasa kwani ana Siri nzito juu yake ambayo ni muda muafaka sasa kwa Watanzania kuijua,na kudai kuwa yeye si mtoto wa Julius Nyerere kama anavyopotosha Mkapa ila ni wa Josephat Nyerere

  Josephat na Julius ni mtu na Mdogo wake(kama hataki ajinyonge) huku akishangiliwa na umati mkubwa Sana uliohudhuria katika viwanja vya mkuytano uliofanyika Sing'si alimtaka Mkapa ajibu na aweke wazi juu ya Kifo cha baba wa Taifa aliyeondoka Butiama akiwa Mzima aliyekwenda tu kupima Afya na kurudi Mfu, huku umati ukipiga Mayowe kwa kushangilia, alitaka aweke wazi kilichomuua baba wa Taifa huku akimwaga Hadharani tofauti zilizojitokeza na Ugomvi kati yake na Mwalimu kilichopelekea Mkapa kuamua na kulazmisha mwalimu apelekwe London kutibiwa (kuuwawa) huku Nyuma akimyamazisha Daktari wa Mwalimu kwa kumpa Uwaziri ili asiseme kilichotokea.

  Na alisema ilikuwaje Mkapa ataje Ugonjwa wa mwalimu ili hali Daktari wake yupo?alihoji, amemwaga vitu vingi ambavyo kwa kweli vitaleta Maswali Mengi juu ya wananchi wa Tanzania na dunia kwa ujumlaa...

  Nikiripoti kutoka Uwanja wa Mapambano wa Arumeru ni mimi Mgosi Mgeni wenu wa JamiiForums
   
 2. m

  mgeni wenu JF-Expert Member

  #2
  Mar 14, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 3,669
  Likes Received: 614
  Trophy Points: 280
  Hakuna Rangi Mkapa hapa ataacha ona mwaka huu
   
 3. SINA JINA1

  SINA JINA1 JF-Expert Member

  #3
  Mar 14, 2012
  Joined: Feb 24, 2012
  Messages: 392
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Du! Kumbe huyu jamaa (Mkapa) alikuwa ana yake mengi kuliko tuliyoyafahamu.Tutajua mengi zaidi ya haya
  Mungi Ibariki Tanzani na CDM kwa kutufumbua macho
   
 4. SINA JINA1

  SINA JINA1 JF-Expert Member

  #4
  Mar 14, 2012
  Joined: Feb 24, 2012
  Messages: 392
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Du! Kumbe huyu jamaa (Mkapa) alikuwa ana yake mengi kuliko tuliyoyafahamu.Tutajua mengi zaidi ya haya
  Mungi Ibariki Tanzani na CDM kwa kutufumbua macho
   
 5. BONGE BONGE

  BONGE BONGE JF-Expert Member

  #5
  Mar 14, 2012
  Joined: Oct 19, 2011
  Messages: 3,398
  Likes Received: 1,522
  Trophy Points: 280
  ......walitofautiana ubinafsishaji, ndo maana jamaa aliuza nchi baada ya kifo cha mwl, alifanya kinyume na mwl alivyokuwa anamwamini. Wabongo kwani wana mwamana basi?
   
 6. Pasco_jr_ngumi

  Pasco_jr_ngumi JF-Expert Member

  #6
  Mar 14, 2012
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 1,811
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  Amkeni wana jamii..... Mi naelekea mawindoni kusaka meno ya tembooooo
   
 7. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #7
  Mar 14, 2012
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Keil homeboy nakuona hapa, wayasikia haya lakini?

  Hii habari ni mbaya sana sana kwa Mkapa na CCM kwa ujumla.

  Sijui atajiosha vipi huyu Mzee? Kweli hukumu ni hapahapa duniani. Kumbe CCM wamemuuwa Baba wa Taifa?
   
 8. Muke Ya Muzungu

  Muke Ya Muzungu JF-Expert Member

  #8
  Mar 14, 2012
  Joined: Jun 17, 2009
  Messages: 3,451
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 0
  wengi wanajua mkapa alimuua mwalimu. sasa kazi kwake, badala ya kutulia, yeye kaweka kimbelembele. naona Adam Malima anacheka kwani atapumzika wiki hii
   
 9. GodfreyTajiri

  GodfreyTajiri JF-Expert Member

  #9
  Mar 14, 2012
  Joined: Sep 26, 2010
  Messages: 846
  Likes Received: 229
  Trophy Points: 60
  mmmmh, kama wanandugu wa baba wa taifa wanaamini hivyo hii itakuwa noma hasa.
   
 10. TONGONI

  TONGONI JF-Expert Member

  #10
  Mar 14, 2012
  Joined: Feb 18, 2011
  Messages: 1,027
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Huyu Vincent amesema maneno mazito sana,na jambo zuri zaidi ni wenyewe kwa wenyewe....Ngoma bila kulewa Mkapa utaichezaje hiyo?
   
 11. K

  Keil JF-Expert Member

  #11
  Mar 14, 2012
  Joined: Jul 2, 2007
  Messages: 2,214
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Mshaurini Vicent Nyerere aachane na hizo siasa. Hoja kuu ambayo alitakiwa kuisimamia ni kwamba Vicent Nyerere hajawahi ku-claim mahali popote pale kwamba yeye ni mtoto wa Marehemu Mwalimu Nyerere. Kwa hiyo, claim ya Mkapa ilikuwa baseless na haiwezi ku-hold maji na hizo ndio siasa za maji taka, watu wanaacha hoja halafu wanakijita kwenye kuzua vijambo na vijimambo.

  Discussion za chanzo cha kifo cha Mwalimu Nyerere kwa sasa haziwezi kuwasaidia CHADEMA ili washinde huko Arumeru Mashariki. Mjadala huo kwa sasa hauna msaada wowote kwa wananchi wa Arumeru ambao wana matatizo ya Ardhi na Maji, pamoja kukosekana kwa ajira kwa vijana.

  Focus ya Kampeni ya CHADEMA iwe ni kwenye kero za wananchi wa Arumeru. Ili kumgonga vilivyo Mkapa na Chama chake, matatizo ya maji na ardhi hayajaanza leo wala juzi, yapo kwa miaka mingi sasa. Je, Mkapa akiwa Rais ina maana hakuyajua hayo matatizo, kama aliyajua, kwanini hakuyashughulikia? Kikwete yuko madarakani mwaka wa 7 sasa, je hajapelekewa hayo matatizo au hajui hayo matatizo? Je, wananchi watakuwaje na imani kwamba Mkapa akienda kumwambia Kikwete matatizo ya maji na adhi atayatatua na ilihali amekuwa madarakani kwa miaka 7 na matatizo yako pale pale?

  Iwapo Mzee Sumari (RIP) alishindwa kusaidia kutatua matatizo ya Arumeru Mashariki akiwa Naibu Waziri wa Fedha (sehemu ya serikali ya chama tawala), je leo hii mwanae ndio ataweza kuyatatua? CCM kimebaki kuwa ni chama cha kuweka ahadi hewa bila kutimiza. Hapo ndio CHADEMA inatakiwa kusimamia kwa kuwa ndo ukweli wenyewe na wananchi wanajionea. Wakumbusheni kwamba hata Igunga ambako CCM walishinda uchaguzi mdogo, zile ahadi zote za CCM zilizotolewa kwa wana Igunga ikiwemo ya kujengewa daraja hazijatimizwa hata moja!
   
 12. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #12
  Mar 14, 2012
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,944
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Mtu asiyejiheshimu anastahili kujibiwa hiyo, ameyataka mwnyewe badala ya kukaa atulie. Na bado jana nilisema hapa aache kutisha watu kwa kuanza kutukana watu atueleze aliko Balali.

  Hongera sana Chadema tumesema acheni woga Igunga mlimulea sana hadi akawa anatamba wakati tunajua ana madhambi mazito.
   
 13. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #13
  Mar 14, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Ni daktari gani huyo aliyenyamazishwa kwa kupewa uwaziri?
   
 14. m

  mgeni wenu JF-Expert Member

  #14
  Mar 14, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 3,669
  Likes Received: 614
  Trophy Points: 280
  Mkapa alitaka kumyamazisha na dogo kaamua kuziba mdomo,hiyo ndo tamu ya siasa, kamwaga ugali huyu kamwaga Mboga ngoma Draw sasa siasa z-chweze Upyaa,tatrizo Mkapa hakujipanga vizuri maana CHADEMA walijua atafyatuka na atanyazishwa na Mkakati wa wa kumtoa Mkapa kwenye chat ya kupigia debe CCM maana ndo msafi wanaeamini aliyebaki CCM, kama katolewa nishai basi CCM haina tena wa kuwapigia Debe na wastegemee tena ushindi popote
   
 15. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #15
  Mar 14, 2012
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,944
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Na hii ni nzito kuliko angeambiwa yeye fisadi, hii hata akikana hilo doa kulisafisha mioyoni mwa watu itakuwa kazi. Tulikuwa tunasikia pembeni pembeni sasa imetolewa na mtoto wa familia yenyewe, tutajuaje huko kwenye familia wanavyomsema Mkapa.
   
 16. K

  Keil JF-Expert Member

  #16
  Mar 14, 2012
  Joined: Jul 2, 2007
  Messages: 2,214
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Wa Kukaya ninayasikia sana,

  CCM huwa wananishangaza sana, huwezi kuwatenganisha Mkapa, Rostam, Chenge, Mramba na Yona [wote wana sifa kuu moja ni mafisadi]. Sasa hizi tuhuma za kumuua Mwalimu zinazidi kumpaka matope Mkapa, sasa subiri kimya chake au povu litakavyomtoka atakapokuwa anajitetea ili aonekane ni Mr Clean!

  Mtuhumiwa namba moja wa kuivuruga CCM ni Mkapa, halafu leo ndio anaitwa kwenda kupiga kampeni as if yeye ndo msafi kuliko wote. Mwanakijiji juzi alihoji, iweje CCM imvishe jezi namba 10 Bwana Mkapa ilihali anajulikana wazi kwamba ni fisadi mkuu na ushahidi upo kwamba alijigawia Kiwira na kupitisha madudu kibao zama za utawala wake?

  Yale aliyoyasema Vicent Nyerere, yanatosha sana kwa sasa. Wao [CHADEMA] waendelee kujikita kwenye hoja na kero zinazogusa maisha ya kila ya wananchi wa Arumeru Mashariki. Huko Kaskazini ule mtaji wa udini haufanyi kazi na ndio maana Mkapa amekuja na mtaji wa matusi na hoja zisizo na mashiko. CHADEMA wakikaa vizuri wanaweza kushinda kirahisi sana.
   
 17. m

  mgeni wenu JF-Expert Member

  #17
  Mar 14, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 3,669
  Likes Received: 614
  Trophy Points: 280
  Angalau sasa hatusemei tena pembeni tumeujua ukweli na kazi imeanza huu ni mjadala wa karne kwa Tanzania nzima ni jukumu la Mkapa kujisafisha
   
 18. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #18
  Mar 14, 2012
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Keil,

  Hizi habari zimenipita sana mwenzio kushoto. Nafikiri kwa sababu ya kukaa sana Sikonge tangu nilipomaliza JKT. Mengi yanayotokea Dar kwa kweli ni kusoma hapa JF, kwenye mitandao au nikiongea na Mtanzania.

  Hii habari sijawahi kuisikia kabisa na kwa kweli imenishangaza mno. Nakumbuka kuangalia mazishi ya Nyerere kwenye BBC na CNN na kumuona hadi Mama Madeleine K. Albright akija Tanzania. Sikutegemea kuwa Mkapa atakuwa mkatili namna hiyo na mtu aliyeweka pesa mbele hadi kumtanguliza Mwalimu wake na mtu aliyemuweka madarakani.

  Nakubaliana na wewe kuwa Dr. Slaa au Mbowe au Zitto, wampige STOP huyu V. Nyerere na hii habari asiiongelee tena. Kama sumu kashatema na mengine acha yaanze kushuka kwa gravitation force.

  Ngoja nilale na asubuhi ntaamkia hapa kuifuatilia zaidi kama haitafutwa.

  [Lali/dilagi mpola kwenuko ]
   
 19. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #19
  Mar 14, 2012
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Ni nani alikuwa waziri wa afya chini ya utawala wa Kikwete?
   
 20. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #20
  Mar 14, 2012
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Sikonge ndugu yangu,
  Wengine tumenyamaza na hizi habari kifuani mwetu kwa miaka mingi tu. Nilijua kuna siku itamwagika hadharani. Sikutegemea kwamba itamwagika nikiwa bado hai.
   
Loading...