The Palm Tree
JF-Expert Member
- Apr 13, 2013
- 7,951
- 12,535
Jaji Mustapha Siyani katishwa akatishika na kuamua kuisigina haki hadharani mchana kweupe....
Amejitoa kuisikiliza kesi hii kwa maumivu makali katika nafsi yake kwa kuisigina haki mchana kweupe akidhani kwa kuwa yeye ni JAJI, wengine wote ni "wajinga" hatutaona upuuzi wake. Amekosea sana...!
Huyu kajitoa si kwa sababu eti ya majukumu yake mapya ya ujaji kiongozi, la hasha...!
Ni kwa sababu NAFSI YAKE IMEBEBA HATIA [guilty conscious]. Anaona giza mbele yake. Anamtumikia ibilisi shetani. Na shetani hana mzaha, atamtumikia weeeee lakini mwishoni anammaliza kwa kumchinja yeye. Ndivyo ilivyokuwa kwa Yuda Iskariote aliyemsaliti Yesu Kristo...!!
Hapo awali alijitahidi sana kuonekana ni mtu wa haki lakini mwizi ni mwizi tu japo atajifanya kuvaa ngozi ya mwanakondoo asiye na dhambi lakini mwisho wa siku atajionesha tu kwa ngozi yake halisi ya chui....
Hii ndiyo picha ya Jaji Mustapha Siyani ambayo mtu anaweza kuichora. Hakika, hii haina shaka yoyote kuwa huyu naye ni mshirika wa ile syndicate ya uhalifu wa kidola...
Jaji Siyani amemaliza kipande chake, anakuja Jaji mwingine miongoni mwa syndicate ileile ya waliokwisha kuapa kuwa lazima wampoteze Mbowe na CHADEMA...
Swali ni wataweza? Mpango wao huu muovu utafanikiwa?
Msikilize wakili huyu akichambua makosa ya kisheria ya hukumu ya Jaji Mustapha Siyani...