chiembe
JF-Expert Member
- May 16, 2015
- 12,003
- 20,681
Wakili Mpale Mpoki alisimamishwa uwakili miezi miwili iliyopita na Jaji Ntemi Kilekamajenga. Mpale Mpoki akaomba nakala ya hukumu, Jaji hajaitoa nakala hiyo mpaka sasa miezi miwili imepita. Na anayefanyiwa hivi ni wakili mkubwa kabisa, vipi kuhusu wananchi wa kawaida? Jaji Kilekamajenga anawatendea vipi? Je mahakama inaweza kufanya intelijensia na kufuatilia uendeshaji wa mashauri wa Jaji huyu?
Jaji Mkuu Prof Juma yeye anahangaika na kujenga majengo tu bila kujali nini kinafanyika ndani ya majengo hayo, na kwa uhakika, wananchi shida yao si majengo, ni haki hata kama itatolewa chini ya mti. Majengo yamejaa viyoyozi, viti vya kuzunguka, suti kwa gharama za watanzania, makompyuta na maelfu ya watumishi, lakini wameshindwa kutoa hukumu yenye kurasa nne, kwa miezi miwili.
ChanzoYouTube Channel