Jaji Mgeta: Niliumizwa na Waziri Mkuu kuchana Hukumu ya kesi niliyotoa kuwa kashindwa

Sildenafil Citrate

JF-Expert Member
Jan 29, 2021
573
2,553
Jaji aliyemaliza muda wake wa kuitumikia Mahakama, Jaji John Mgeta amesema katika kazi yake ya utumishi kama Jaji hatasahau namna ambavyo kigogo wa Serikali alichana hukumu mbele yake.

Jaji Mgeta ameyasema hayo leo Mei 4, 2023 muda mfupi baada ya hafla ya kuagwa yeye na majaji wengine wawili iliyofanyika Mahakama Kuu Kanda Masjala ya Dar es Salaam.

Jaji Mgeta amelitaja tukio hilo kama moja ya changamoto kubwa aliyowahi kukutana nayo katika utendaji wake.

“Miongoni mwa changamoto nilizokutana nazo ni kusimamia kesi ya aliyekuwa kigogo wa Serikali na kushindwa kesi kwa kigogo huyo. Katika shauri hilo kigogo wa serikali alishindwa kesi lakini nilipopeleka maamuzi ya mahakama aliyadharau na kuamua kuchana karatasi ya hukumu, kitendo hiki kiliniumiza sana na nilikosa furaha, lakini nashukuru baadae serikali ilisimama na kutekeleza kile kilichoagizwa na mahakama,”amesema Jaji Mgeta.

Awali, akizungumza katika hafla ya kuwaaga majaji hao, Jaji Kiongozi Mustapha Siyani amesema wananchi hawapaswi kuwa na wasiwasi na mahakama kwani ni huru na inatoa haki.

Jaji Siyani amewataja majaji hao waliomaliza muda wao wa utumishi kuwa ni Jaji Sekela Moshi, Jaji Beatrice Mtungi na Jaji John Mgeta ambapo amesema kuwa kipindi chote cha kazi kwa majaji hao walikuwa wanafanya kazi kwa weledi.

Amesema mbali na kuchapa kazi pia waliomaliza muda wao na wenye utii kwa kila mtu na kwamba kuondoka kwao ni pengo.

“Wananchi wakikosa imani na mahakama kila mtu atachukua sheria mkononi, na nchi yoyote duniani lazima iwe na mahakama, hivyo tuna mahakama nchi nzima zipo kwa ajili ya kuwasikiliza wananchi,” amesema Jaji Siyani.

Amesema kitendo cha kumaliza muda wao wa kazi kisheria ni alama tosha ya kuweza kuigwa kwa watumishi ili kuleta ufanisi katika kazi yao.

“Tunawakumbuka kwa bidii yenu ya kazi lakini na namna bora ya uongozi kwa kutatua kesi mbalimbali bila kujali ukubwa wake,” ameongeza Jaji Siyani.

Aidha, amesoma wasifu wa viongozi hao ambapo amesema wote walikuwa wamejaaliwa ujuzi katika kuandika hukumu pamoja hekima wanapokuwa na watu.

Chanzo: Mtanzania
 
Jaji: Nilumizwa na Waziri Mkuu kuchana Hukumu. Aanika ukakasi vigogo Serikalini kudharau Mahakama.

Chanzo: Kichwa cha Habari cha Gazeti la Nipashe leo Mei 5, 2023

IMG_7052.jpeg
 
Itasaidia Nini kwa sasa? Alitakiwa asema jambo hilo wakati uleule angeonekana jasiri na mwenye msimamo madhubuti kuliko kusema sasa.

Alionyesha udhaifu mkubwa sana kwa kutokuchukua hatua kipindi kile akabaki na maumivu Hadi Leo!!

Anawafumdisha nidhamu ya uoga, kwamba ukifanyiwa jambo baya usiseme usubirie Hadi siku ya kustaafu ndipo uelezee kama stori!
 
halafu umri wa kustaafu majaji ni miaka mingapi? inaonekana majaji wanao staafu wamezeeka sana!!! Kwa Nini umri wa kustaafu majaji usipunguzwe?!!! maana wamechoka sana!!!
Inaonekana wengi wao umri umesonga sana.

Mahakama inahitaji utulivu wa kichwa.

Watu wazima akili zao ziko settled kuliko vijana wenye matamanio ya mambo mengi.

Mgeta alikua poa sana.

Sasa hivi Kuna mahakimu na majaji wadogo ila bado hawajaiva vizuri
 
Itasaidia Nini kwa sasa?!
alitakiwa asema jambo hilo wakati uleule angeonekana jasiri na mwenye msimamo madhubuti kuliko kusema sasa.

alionyesha udhaifu mkubwa sana kwa kutokuchukua hatua kipindi like na akabaki na maumivu Hadi Leo!!!!!!

anawafumdisha nidhamu ya uoga, kwamba ukifanyiwa jambo baya usiseme usubirie Hadi siku ya kustaafu ndipo uelezee kama stori!!!!!!!
Kumbuka aliyefanya hivyo alikuwa kigogo wa serikali🤔aliwaza mafao yake na penshen yake ya uzeen akaamua kutumia busara kuliacha lipite🤣he knows the court system is somehow fu.ck.e.d up🤺
 
Mahakama inahitaji utulivu wa kichwa.

Watu wazima akili zao ziko settled kuliko vijana wenye matamanio ya mambo mengi.

Mgeta alikua poa sana.

Sasa hivi Kuna mahakimu na majaji wadogo ila bado hawajaiva vizuri
Bado nasisitiza kuwa umri wa kustaafu upunguzwe kwa majaji maana wengi wao wamechoka sana!!

Waacheni wazee wapumzike, mnataka waifie kazini?!!!

Naamini pia familia zao zinawahitaji wafanye mambo Yao, waacheni wastaafu wakiwa bado na nguvu ili wafanye mambo Yao nyumbani.
 
Back
Top Bottom