Uzi Maalumu wa Nyimbo za Injili (Gospel Music Special Thread)

tpaul

JF-Expert Member
Feb 3, 2008
21,838
18,250
Bwana Yesu asifiwe! Nimeanzisha huu uzi maalumu na mahususi kwa wapenzi wa nyimbo za injili. Hapa tutakuwa tunabadilishana nyimbo mbalimbali za injili za sasa na zamani. Huenda kuna mtu anautafuta wimbo fulani wa injili bila mafanikio. Basi ataomba wimbo huo hapa jukwaani na atatumiwa na mwanajukwaa atakayekuwa nao.

Lengo hasa ni kuhakikisha kuwa tunaendelea kuwaenzi waimbaji wetu wa nyimbo za injili kwa kutambua kazi zao na pia kusaidia kueneneza injili kupitia uimbaji. Kuna ushahidi wa watu kuokoka na kuamua kumtumikia Mungu kwa kusikia wimbo fulani wa injili ukipigwa.

Muziki una nguvu sana. Hata wapigania uhuru walihamasishana kupitia nyimbo zilizowapa hamasa kupigana na mkoloni hadi uhuru ukapatikana. Na kupitia nyimbo za injili, tunayo fursa ya kupambana na shetani hadi kuokoka na kuwasaidia wengine kuokoka.

Baada ya kusema hayo, naomba sasa wenye nyimbo mbalimbali za zamani za injili waanze kuzitupia humu jukwaani ili tuburudike kwa pamoja na kumtumikia Mungu kupitia uimbaji. Na pia kama kuna mtu anahitaji wimbo fulani anaoutafuta kwa muda mrefu bila mafanikio, basi ajitokeze na aombe atumiwe na wanajukwaa.

Sio lazima mtu awe askofu au padri ili amtumikie Mungu. Hata wewe utakayetupia wimbo humu utakuwa umemtumikia Mungu pakubwa. Karibuni sana.

View attachment 2840127
Karibuni wadau wa dini zote tuburudike pamoja kwa nyimbo za injili
 
Back
Top Bottom