Kwanini waimbaji wa Injili wa kike hapa Bongo hawadumu kwenye ndoa?

Mhaya

JF-Expert Member
Aug 20, 2023
1,658
4,861
Ukitizama waimbaji wa injili wengi wa kike mfano kina Beatrice Mhone, Bahati Bukuku, Angel Bernard, kina Christina Shusho, kina Flora Mbasha na wengineo wamekuwa katika wimbi la kuolewa na kuachika. Huku sisi wafuasi wao ambao tunawaona kama Role Modal wakituacha solemba tukiduwaa.

Waimba Injili tunawachukulia kama watu wema au wanaoishi katika neno la MUNGU kwa namna wanavyoeneza injili katia nyimbo zao, hivyo kwa asilimia kubwa tungetegemea kuona wao wakituongoza katika kuwa na ndoa njema na kuishi maisha ya furaha kwa sababu tunaamini anayeishi kwenye neno basi uishi kwa furaha. Lakini cha kushangaza nao tunawaona wanaolewa na kuaachika.

Shida ni nini hasa kwa hawa ndugu zetu, mwenye ulewa juu ya haya mambo tunaomba ufafanuzi nini kinawakumba hawa dada zetu?
 
Mziki wao wanafanya kibiashara, they don't mean what they sing bro. Jiongeze, kwani wachungaji wangapi wanatembea na waumini wao? Masheikh wangapi wanalawiti waumini wao? Mapadre wangapi wana watoto au kugonga masista?

Dini ni akili yako tu sio mambo ya kuambiwa.
 
Sababu kubwa ni status. Kutokana na kipaji cha uimbaji wanapata umaarufu kuwazidi waume zao. Mwanamke akishamzidi mwanaume katika nyanja flani anakosa kumheshimu mumewe kama kichwa cha familia. Kwa ivo hawezi kuishi na mwanaume aliemzidi. Ili mwanaume awe kichwa cha familia inabid umzidi mwanamke. Mfano yeye ana umaarufu. Wewe una pesa
 
Wengi ukiwachunguza wanaimba wasichokiamini, wanaimbia watu huku wenyewe hawaishi maisha hayo, wamepatwa na kiburi baada ya kupata fedha, wanawaona waume zao ni maboya tu, hawashauriki wala kuambilika. Wachungaji wao wamewashindwa wanajiendea tu. Baada ya kuwa na kiburi huporomoka na kubaki kuimba nyimbo zisizo na upako kama mwanzo. Bora wakafanye collabo na waimba muziki wa kidunia
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom