Uuzwaji wa Viwanja vya Serikali mtandaoni ni Hatua kubwa sana

Jamaa wameniambia eti namba yangu ya Nida na namba yangu ya simu haviendani ,ila nilitaka kujisajili ninunue viwanja..

Hii kitu imenikuta kwenye Leseni ya biashara
Naambiwa namba ya Nida na namba ya Simu haziendani na sijawahi kubadilisha namba ya simu
 
Nimeupitia na kuna baadhi ya viwanja Nimeanza kulipia sema kuna mapungufu

1. Kuna mda mfumo unakua haupatikani

2. Kuna mda unaingia unakua wilaya ime ongezeka ukija baadae hutaiona tena. Mfano Bagamoyo, bahi, iringa hizi inakuja na kupoteza naanza kuhisi hua wanaziweka akiwa na wateja wao. Mfano bahi na iringa viwanja ilikua bei ya mserereko

3. Kwenye kiwanja ukianza kulipia kulikua na gharama za kuandaa hati, nmechukua mm viwanja viwili ila ss kuna kitu inaitwa Premium kimeongezwa na mwanzo hakikuepo kabisa na ni hela ndefu

4. Ni hongera system ukilipa mda huo huo chat inasoma.

Kama kuna mwenye kuongeza karibu
Tuelezee zaidi kuhusu hiyo Premium
 
Mm mwenyewe sjajua ni nn na hakuna Sehem ya mawasiliano na wenye website
Hiyo ni website ya Tamisemi
Ila Kama una ishu unatafuta mawasiliano ya Halmashauri husika ambayo imelaunch project yake kwenye Tausi.

Mfumo bado ni mchanga,na Halmashauri ni chache waliotangaza viwanja kwakua ,inahitaj kupewa mafunzo na wataalamu wa sekta ya Ardhi toka Tamisemi,Dodoma,Mafunzo ambayo mkurugenzi wa Halmashauri husika anapaswa kuyagharamia.

Then wataalamu wa Halmashauri husika, waliopewa mafunzo,wanatengenezewa User I'd za kuwawezesha kuingia kwenye mfumo wa Tausicore ili kucreate project husika(Kama Kuna viwanja ambavyo vimeshapimwa na vinasubiri kuuzwa kwa Umma) na kuilaunch/ kuirusha kwenye mfumo wa Tausi.
 
Utakuta hako ni ka kias tunapigwa na wenye mfumo na hakaendi serikalin
 
Ni kweli ni hatua kubwa na ya kupongezwa.
Ni suruhisho la tunao nunua viwanja na baadaye vina migogoro
Ni suruhisho la tunao nunua viwanja kutoka kwenye makapuni binafsi kampuni hizo kufilisika, na nyingine zina kesi nyingi mahakamani.
Ni rahis baadaye kuomba na kupata hatimiliki kwa urahisi
 
UPDATE
Nmemaliza kulipia kiwanja changu tatizo nililokutana nalo
1. Siwez view bill yangu ili nione gharama za hati
2. Nilitarajia kua baada ya kumaliza kulipa kiwanja ningepata control number mpya kwa ajili ya kulipa hati
3. Sina uwezo wa kuwasiliana na huduma kwa wateja wa tausi, au sina mawasiliano na watu wa kwimba halmashauri. Kwimba namba zao hazipatikani na tausi hakuna jinsi ya kuwapata
4. Tamisemi kwenye website wame weka namba za kuwa tafuta ila hazijalipiwa so hata nilipiga sina jinsi ya kuwapata.
 
Bado mfumo una shida za hapa na pale. Lakini unaweza kupata control no ya kulipia Kwa kuingia kwenye Mfumo; upande wa kushoto Kuna link ya Land sales, click hapo kisha nenda kwenye My Applications, utakikuta kiwanja ulicholipia Application fee. Kuna link pembeni yake kulia, bonyeza then utaona Bill ya Application Na Bill ya Kiwanja. Pembeni mwa Bill ya Kiwanja kuna link ya ku view Bill - bonyesha hapo utaipata Bill kamili ambayo unaweza kui print
 
Back
Top Bottom