Njia 8 Za Uhakika Za Kupata Wazo Linalolipa Kupitia Uwekezaji Wa Viwanja/Mashamba/Majengo

Aliko Musa

Senior Member
Aug 25, 2018
156
240
Mwanaidi alipata wazo la kutafuta wateja wa kukodi shamba lake la ekari 10 baada ya kumiliki eneo hilo kwa muda mrefu bila kuingiza kiasi chochote.

Eneo lake (Mwanaidi) lina uwezo wa kuingiza 500,000 kwa msimu wa kilimo. Ikiwa ataweza kupata wafugaji wa ng'ombe au mbuzi au samaki, kipato kinaweza kuwa zaidi ya hapo.

Emmanuel ni mmiliki wa viwanja 2 vilivyopimwa. Kutokana na changamoto za safari ya maisha yake na familia yake ameshindwa kulipia kodi ya ardhi serikalini kwa miaka kadhaa.

Baada ya kuona makala zangu za kukodisha viwanja/mashamba alifanya maamuzi ya kuchukua hatua. Hii ni hatua nzuri sana ambayo itaondoa changamoto kadhaa kuhusu kipato chake.

Nasibu ni mmiliki wa nyumba kuu kuu katikati ya jiji lililoendelea. Nyumba aliipata kwa njia ya urithi. Nasibu ana umri wa miaka 24 tu. Watu wake wa karibu na yeye mwenyewe hawana uwezo wa kujenga aina ya majengo ambayo yanazunguka nyumba yao/yake.

Hivyo, akaamua kumtafuta mwekezaji wa kujenga nyumba ya kupangisha ambayo itakuwa inasaidia kuendesha maisha yeye na wadogo zake.

Alipata mwekezaji ndani ya siku 60. Hii ilikuwa baada ya kumshauri njia kadhaa ambazo zina ufanisi mkubwa katika kupata wawekezaji wa kujenga katika kiwanja chako.

Mwaipopo ni mmiliki wa nyumba iliyojengwa kisasa. Mwaipopo ni mwajiriwa serikalini, alijenga nyumba hiyo kwa kutenga sehemu ya mshahara wake kwa miaka kadhaa.

Baada ya muda alihamishwa kituo cha kazi kutoka Mbeya na kwenda kutumikia Bukoba. Jambo hili lilifanya nyumba yake, ikose matumizi. Alijaribu kushauriana na mkewe kipenzi ili waiuze, wakaona ni maamuzi ya hovyo kwa upande wao.

Baada ya kufahamu njia bora zinazoweza kuingiza kipato endelevu. Mwaipopo na mke wake waliamua kutafuta mpangaji ambaye ataitumia nyumba hiyo kwa ajili ya kulea na kufundisha watoto wa chekechea (Daycare centers).

Ni mwaka wa tatu tangu waanze kukodisha nyumba yao. Nyumba wanakodisha shilingi laki mbili kwa mwezi. Hii si fedha ndogo. Ni kipato ambacho kinaweza kutumika kufungua biashara nyingine, kulipia watoto ada za shule, kununua kiwanja, hata kununua nyumba chakavu na kuiboresha kwa ajili ya kutengeneza kipato.

Leo ninakushirikisha njia 8 ambazo na wewe unaweza kuzitumia kupata wazo zuri la kukufanya uongeze kipato chako.

Njia 8 Za Kupata Wazo La Kuwekeza Kwenye Ardhi Na Majengo.

Moja.

Kumiliki kiwanja au shamba. Kama unamiliki kiwanja/shamba, tafakari kwa kina njia zote za kutengeneza fedha. Kisha chagua njia tatu bora sana. Chukua hatua sasa kwa kufanyia kazi maarifa yako.

Mbili.

Kumiliki jengo katika eneo zuri.

Tatu.

Kumiliki banda la chuma/aluminium ambalo hulitumii kwa sasa.

Nne.

Kumiliki konteina ambalo halina matumizi ya kuingiza fedha.

Tano.

Kupata/kuwepo kwa wapangaji bora sana wa mabanda ya biashara au kontena au nyumba za kuishi au fremu za biashara.

Saba.

Kupata mnunuzi wa jengo au kiwanja ambaye yupo tayari kuingia makubaliano ya kimaandishi.

Nane.

Kiasi cha mtaji fedha ulichonacho mfukoni mwako.

Usikubali kipato chako kiendelee kuwa kidogo wakati una rasilimali za kuongeza kipato chako.

Kama kuna njia za hapo juu zinakuhusu unaweza kunitumia ujumbe na tuanze kufanya kazi pamoja. Njoo tushirikiane na mimi uweze kuongeza kipato chako kupitia viwanja, mashamba, mabanda ya biashara na majengo/nyumba.

Rafiki yako,

Aliko Musa.
Whatsapp; +255 752 413 711
 
Back
Top Bottom