Uuzwaji wa Viwanja vya Serikali mtandaoni ni Hatua kubwa sana

Jicho la Tai

JF-Expert Member
Oct 10, 2012
1,449
574
Ukiingia kwenye huu mfumo wa Tausi kupitia tausi.tamisemi.go.tz una vitu vingi sana ndani japo vingine naona havifanyi kazi.
Screenshot (44).png

Nimefurahishwa sana na uuzaji wa viwanja ambapo unanunua kiwanja unakiona kwenye ramani kama ilivyo google map, tofauti na ile ya kwenye karatasi. Wengi tuna viwanja ila hata location hatujui mpaka twende physically.

Screenshot (46).png

Hii inampa uhuru mtu kununua kiwanja popote nchini bila kufika ili mradi anakiona.
Tatizo naloliona hapa ni moja tu, Wilaya nyingi zimepima viwanja ila havipo humu.

Nini unatakiwa kufanya
-> Jisajili kwa kutumia NIDA na TIN yako
-> Nenda land sale module
utaona viwanja vyote vinavyouzwa na Halmshauri nchi nzima
-> Chagua Halmashauri unayotaka kununua kiwanja
-> Chagua kiwanja kutoka kwenye ramani
-> Lipia kupitia control number ya ada ya maombi utakayopewa
-> ukimaliza kulipia utapata control number nyingine ya ada ya kiwanja, ukishalipia kiwanja ni chako!

Unaendelea na hatua za kupata hati.
Screenshot (45).png
 
Ukiingia kwenye huu mfumo wa Tausi kupitia tausi.tamisemi.go.tz una vitu vingi sana ndani japo vingine naona havifanyi kazi.
View attachment 2888384

Nimefurahishwa sana na uuzaji wa viwanja ambapo unanunua kiwanja unakiona kwenye ramani kama ilivyo google map, tofauti na ile ya kwenye karatasi. Wengi tuna viwanja ila hata location hatujui mpaka twende physically.

View attachment 2888388

Hii inampa uhuru mtu kununua kiwanja popote nchini bila kufika ili mradi anakiona.
Tatizo naloliona hapa ni moja tu, Wilaya nyingi zimepima viwanja ila havipo humu.

Nini unatakiwa kufanya
-> Jisajili kwa kutumia NIDA na TIN yako
-> Nenda land sale module
utaona viwanja vyote vinavyouzwa na Halmshauri nchi nzima
-> Chagua Halmashauri unayotaka kununua kiwanja
-> Chagua kiwanja kutoka kwenye ramani
-> Lipia kupitia control number ya ada ya maombi utakayopewa
-> ukimaliza kulipia utapata control number nyingine ya ada ya kiwanja, ukishalipia kiwanja ni chako!

Unaendelea na hatua za kupata hati.
View attachment 2888389
Naona viko vya mikoani tu,
Au halmashauri za Dar hawana viwanja vya kuuza?
 
Jamaa wameniambia eti namba yangu ya Nida na namba yangu ya simu haviendani ,ila nilitaka kujisajili ninunue viwanja..
Lazima namba ya simu uliyoandika iwe inaendana na ile uliyosajili wakati wa usajili wako wa Nida. Na Kama namba uliyotumia wakat unasajili nida ni tofauti, basi hakikisha namba ya sasa unayotumia imesajiliwa kwa namba yako ya ileile ya nida. kama unatumia namba ya mtu lazima utakwama
 
Mbona wameweka halmashauri chache?
Yani ukiona hivyo ujue kuna halmashauri zina ukiritimba, hazitaki kuweka wazi, hivyo zinaona kuweka kwenye mfumo itawakosesha ulaji. Kuna watu maofisi ya Serikali wanapenda kutukuzwa na kufuatwafuatwa, ukiuliza sababu hapo watajifanya wanakupa sababu za kitaalamu kweli kumbe wanachosema tunakijua. Mtu kamaliza chuo 2005 na yupo serikalini, halafu anaelezea kitu ambacho kimemkuta kazini na sisi wengine tuliomaliza 2020 tumekisoma na tuko deep kumzidi, inabidi tu usikilize anavyojikanyaga na umuache.
Hii mifumo ingewekewa sheria nadhan hawa jamaa wa serikalini wangenyooka sema wanachukuliana poa sana.
 
Ni swala la muda tu hatuwezi kukwepa tena mfumo.
 
Mfumo upi unaongelea ?
Tausi.
Umesema hapa kuwa Kuna viwanja vya halmashauri haviingii kwenye mfumo wa Tausi kwa ajili ya kuuzwa kwa wananchi naomba uweke ushahidi ili ijulikane kuwa mfumo wa Tausi unamapungufu na developer wafanyie kazi hayo Mapungufu.
 
Back
Top Bottom