Uteuzi: Rais Samia amteua Nehemia Mchechu kuwa Msajili Hazina

Wazanzibari wanakula nchi yetu wanavyojisikia wakati nchi yao waneificha nyuma hawataki mtu aiguse
Huna ujualo kaa kimya. Hakuna Mzanzibari hapo wote ni Wa Tanganyika. Tena Wapogoro kabisa wa Morogoro.
Teuzi zinakwenda kwa Waislamu wa Zanzibar na Wakiristo wa bara.

Waislamu wa bara itafuteni Tanganyika yenu mliyoipigania kwa nguvu sana, haiwezekani Wazanzibari wanakula share yenu kiulaini kwenye mambo ya nchi yenu ya Tanganyika.
 
Kwa hiyo ile mada ya ukosefu wa vituo vya kujazia magari ya gas jana isiyokuwa na kichwa wala miguu ilikuwa kwa sababu ya kupima upepo kabla ya teuzi.

Nchi ina fitna hii sijapata kuona.

Kuna watu hiyo nafasi ya TPDC walikuwa wanaimezea mate kitambo tu, so wala atushangai.

Huko wizara ya fedha kuna Mwigulu, Mafuru na Nehemia; team ya ulipaji bila kuuliza kule TANESCO imekamilika.

Maza amekusudia kufuata nyayo za ‘Isabela Dos Santos’ kuelekea kwenye ile exclusive club ya kina Mohamed Dewji.
 
Ni kweli, Zanzibar ni sehemu ya Tanzania ila Tanzania sio sehemu ya Zanzibar.

Mzanzibari ni mtanzania ila sio kila mtanzania ni Mzanzibari.

Mali ya Tanzania ni mali ya Zanzibar ila mali ya Zanzibar sio mali ya Tanzania.

Muungano wa hovyo toka Dunia imeumbwa.
Hiyo "mali ya Tanzania ni mali ya Zanzibar ila mali ya Zanzibar siyo mali ya Tanzania"yaani inakera basi tu,sijui kwenye kero za muungano haipo.
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi kama ifuatavyo:-

1. Amemteua Bw. Nehemia Kyando Mchechu, kuwa Msajili wa Hazina. Kabla ya uteuzi huo Bw. Mchechu alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC). Bw. Mchechu anachukua nafasi ya Bw. Mgonya Benedicto ambaye atapangiwa kazi nyingine.

2. Amemteua Bw. Hamad Abdallah, kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC). Kabla ya uteuzi huo, Bw. Abdallah alikuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Gimcoafrica Limited na anachukua nafasi ya Bw. Mchechu ambaye ameteuliwa kuwa Msajili wa Hazina.

3. Amemteua Bw. Mussa Mohammed Makame, kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC). Kabla ya uteuzi huo, Bw. Makame alikuwa Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), na pia ni Mshauri Mwelekezi wa masuala ya mafuta na gesi nchini Tanzania. Bw Makame anachukua nafasi ya Dkt. James Mataragio ambaye atapangiwa kazi nyingine.

Uteuzi huu ni kuanzia tarehe 24 Februari, 2023.

View attachment 2528416
Maama huwa anatia kichefuchefu kwa kweli .utafikir hii ni nchi ya watu 10 tu
 
Kabla ya GIMCO alikuwa NHC pamoja na Mchechu kabla Magufuli hajawatimua bila sababu kwa WIVU wake.
Siyo wivu; zilikuwa ni hujuma.
Kilichokuwa kinafanyika ni kwamba alikuwa anashauriwa awatoe wazuri wote aliokuwa amewarithi kutoka kwa JK, halafu aweke wengine wa kwake yeye ambao wengi wao ilikuwa ni team ya kumhujumu vile vile.
Kwa hiyo alikuwa akitoa ni "hujuma"; na akiingiza ni "hujuma" pia huku akiwa ametengenezewa uadui na wale aliokuwa akiwatoa
 
Back
Top Bottom