Uteuzi: Rais Samia amteua Nehemia Mchechu kuwa Msajili Hazina

benzemah

JF-Expert Member
Nov 19, 2014
1,503
2,977
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi kama ifuatavyo:-

1. Amemteua Bw. Nehemia Kyando Mchechu, kuwa Msajili wa Hazina. Kabla ya uteuzi huo Bw. Mchechu alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC). Bw. Mchechu anachukua nafasi ya Bw. Mgonya Benedicto ambaye atapangiwa kazi nyingine.

2. Amemteua Bw. Hamad Abdallah, kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC). Kabla ya uteuzi huo, Bw. Abdallah alikuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Gimcoafrica Limited na anachukua nafasi ya Bw. Mchechu ambaye ameteuliwa kuwa Msajili wa Hazina.

3. Amemteua Bw. Mussa Mohammed Makame, kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC). Kabla ya uteuzi huo, Bw. Makame alikuwa Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), na pia ni Mshauri Mwelekezi wa masuala ya mafuta na gesi nchini Tanzania. Bw Makame anachukua nafasi ya Dkt. James Mataragio ambaye atapangiwa kazi nyingine.

Uteuzi huu ni kuanzia tarehe 24 Februari, 2023.

Screenshot 2023-02-24 at 14.32.15.png

=====

MAJUKUMU YA OFISI YA MSAJILI WA HAZINA
Kwa mujibu wa Kifungu cha 10 cha Sheria ya Msajili wa Hazina Sura 370 kama ilivyorekebishwa, Ofisi imepewa majukumu yafuatayo: –

1. Kufanya mapitio ya kudumu ama kuhakikisha kunafanyika mapitio ya kudumu ya shughuli na mwenendo wa watu ama Taasisi ambazo Msajili wa Hazina anamiliki mali ama ana maslahi kwa mujibu wa Sheria.

2. Bila kuathiri Kifungu kidogo cha (1) kwa ujumla wake, Msajili wa Hazina anatakiwa:
  • Kutoa ushauri kwa Serikali kuhusu uanzishaji wa Mashirika ya Umma na kusimamia biashara au mali zilizowekezwa kwenye Mashirika hayo;
  • Kupitia utendaji wa kifedha wa Mashirika kwa lengo la kushauri hatua za kuchukua katika kuunganisha, kuboresha muundo, kufuta au kuboresha utendaji wa Mashirika na Taasisi za Umma;
  • Kuweka malengo ya kifedha na vigezo vingine vya utendaji vitakavyotumiwa na Mashirika na Taasisi za Umma;
  • Kufanya tathmini mara kwa mara ili kupima utendaji wa Bodi au Menejimenti za Mashirika na kutoa mapendekezo kwa Serikali ya hatua za haraka au zilizopo za kuboresha usimamizi wa rasilimali;
  • Kuidhinisha uwekezaji wa hisa unaofanywa na Mashirika ya Umma kwenye Mashirika au Kampuni nyingine;
  • Kuwekeza au kuuza mali za Mashirika ya Umma;
  • Kuhakikisha kuwa kila Shirika la Umma linaingia Mkataba wa Utendaji na Msajili wa Hazina mara moja baada ya kuteuliwa kwa Bodi ya Wakurugenzi;
  • Kufuatilia na kutathmini programu za mafunzo katika Mashirika na Taasisi za Umma;
  • Kuelekeza au kuidhinisha matumizi au marekebisho ya kanuni za fedha ili kuhakikisha usahihi wa taarifa za mapato na matumizi ya Mashirika ya Umma;
  • Kuchambua na kuidhinisha Miundo na Mifumo ya Mishahara, Kanuni za Utumishi na Mpango wa Motisha kwa Mashirika na Taasisi za Umma;
  • Kufuatilia misaada, ruzuku, fedha za mtaji, akiba au malimbikizo ya faida katika Mashirika ya Umma na kwenye uwekezaji mwingine wa Umma;
  • Kupendekeza au kuidhinisha Mipango ya Mwaka ya Mashirika na Taasisi za Umma;
  • Kufuatilia na kutathmini utendaji wa Mashirika na Taasisi za Umma; na
  • Kufanya ufuatiliaji na kuhakikisha gawio, michango na mikopo kutoka katika Mashirika na Taasisi za Umma inalipwa kwa wakati.
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi kama ifuatavyo:-

1. Amemteua Bw. Nehemia Kyando Mchechu, kuwa Msajili wa Hazina. Kabla ya uteuzi huo Bw. Mchechu alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC). Bw. Mchechu anachukua nafasi ya Bw. Mgonya Benedicto ambaye atapangiwa kazi nyingine.

2. Amemteua Bw. Hamad Abdallah, kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC). Kabla ya uteuzi huo, Bw. Abdallah alikuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Gimcoafrica Limited na anachukua nafasi ya Bw. Mchechu ambaye ameteuliwa kuwa Msajili wa Hazina.

3. Amemteua Bw. Mussa Mohammed Makame, kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC). Kabla ya uteuzi huo, Bw. Makame alikuwa Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), na pia ni Mshauri Mwelekezi wa masuala ya mafuta na gesi nchini Tanzania. Bw Makame anachukua nafasi ya Dkt. James Mataragio ambaye atapangiwa kazi nyingine.

Uteuzi huu ni kuanzia tarehe 24 Februari, 2023.

View attachment 2528416
Du sasa huyu mzenj ameamu kufanya ujambazi wa kutisha,
Watumishi wa umma,wanawaibia wananchi,Samia,na wazenj wenzake wanaiibia Tanganyika,maana mambo ya mafuta sio ya Muungano,Zenj Wana mambo yao,na Tanganyika hivyo hivyo,sasa unamuwekaje mzenj jikoni kwa Tanganyika kusimamia mambo ya mafuta?huyu si ataiba Siri na kupeleka kwao Zenj,
 
Fact,zanzibar walipogundua mafuta,unakumbuka ilivyokuwa,mpk kikwete akasema mafuta yenyewe hayajai hata kibaba,
 
16 Reactions
Reply
Back
Top Bottom