Utajiri wa kufa na kuoza ndio pesa ije

Utajiri wa kufa na kuoza ndio pesa ije

Ni aina mojawapo ya uchawi wa kupata utajiri ukiacha huu wa ;
Kuua ndugu
Kuwafanya wanafamilia ndondocha
Kuwekwa kidonda mwilini
Kupewa masharti ya chakula nguo na magari nk nk

Huu una mambo yake ya ajabu, unapewa dawa ambayo utamshirikisha mkeo tuu.Ukishakunywa hiyo dawa unakufa na kuoza kabisa mpaka kutoa funza wengi
Sasa mkeo kazi yake kila siku itabidi awafagie hao funza na kuwaweka kwenye ndoo kwa mpaka siku ya saba utakapofufuka.

Utajiri wako utategemea na wingi wa funza watakaokusanywa kwa siku.

Ukishamaliza siku Saba utafufuka na biashara zako zitaanza kuchanganya.

Onyo na tahadhari
-Hutakiwi kuwa na mwanamke mwingine
-Mkeo hapaswi kushtuka mara ya kwanza akiwaona funza utakufa moja kwa moja
-So wewe wala mkeo mnapaswa kutoa siri hii kwa yeyote hata chini ya mtutu wa bunduki
-Ishu ya kufa wiki nzima na kuoza utaifanya kila biashara zinapoyumba

Kama bado unataka utajiri kwa njia za mkato fikiria mara mbili kabla hujamua
 
Nilihadithiwa unaenda kwa mganga then usiku mnatoka na mganga ameshika kuku ww umeshika punje za mahindi katika mikono yako unamwaga uwanjani kuku anakula. Punje atakazo kula ndio urefu wa maisha yako ie akila 10 unakaa miaka 10 ya utajiri wa kutupwa etc
Naskia kwa wakinga iko common sana
Kuku akila mahindi 40 unagawanya kwa mbili 20 ndio miaka yako ya kila bata miaka 20 mingine unamwachia jogoo mnagawana uhai ila ukiwa na kimavi jogoo anakua mahindi 2 ukigawa kwa mbili unamwaka wako wa kula bata hapo hata mademu unapiga kavu tu then RIP
 
% kubwa ya wafanyabiashara wa kiafrika wanapita kwenye short cut hizo hasa hapa kwetu Tanzania ndio wamekithiri.

Zamani ilikuwa ni makabila fulani / kwa sasa imekuwa km fashion' ndio maana ugumu wa maisha unaongezeka kila kukicha maana shetani kaingia kwenye cash flow nchini" hawa wafanyabiashara wa mtindo huu wameharibu kabisa mzunguko wa pesa (how) ...matumizi yao yapo fixed . ....kula/vaa/kunywa/ishi ni shida, mfano tunaona hotpot zinavyoingia kariakoo mchana na ma housegirl as if hakuna migahawa/mamantilie au hotel ' nafikiri ni sharti mojawapo kuwa wasile msosi wowote usiopikwa home.

Hawa ndio wanaonyofoa kingo za noti kwa maana wanaoijua wenyewe/ Mshana naomba tafsiri ya hili.


Ushirikina umekithiri sana Tanzania nafikiri hili nalo ni JIPU ambalo linahitaji kutumbuliwa na limekosa mtumbuaji

"MUNGU TUSAIDIE."
Hii ya msosi kupelekwa kariakoo na ma house girl nimeiona pia
 
Yeye ilikuwa sio kwa ajili ya utajiri,bali ilikuwa ndio mtindo wake kabla hajatoa wimbo/album alikuwa anatambika kwa mizimu ya kwao ambapo alikuwa anajifungia ndani kwenye chumba maalumu hata kwa wiki mbili anakuwa kama kafariki. Kosa lililofanyika ni Mama yake alipokwenda kwake na kuingia humo chumbani ndio akafa moja kwa moja.
Dih, haya mambo ni magumu sana
 
Back
Top Bottom