Updates: Yanayojiri Mtwara - hali bado tete (Mei 23/24, 2013)

Updates: Yanayojiri Mtwara - hali bado tete (Mei 23/24, 2013)

Mkuu tatizo hela ya WAHISANI ishaliwa, sasa wakifanya kama wananchi wanavyotaka hawa WAHISANI waliohakikishiwa gesi huku Dar na kwingineko watarudishiwaje chenji yao!!

Of course chanzo cha vurugu kipo hapo kwenye 10%.
Plan ya mwanzo kabisa ya serikali ilikuwa ni kujenga kinu cha kufua umeme kwa kutumia gesi Mtwara, kisha kuusafirissha umeme huo hadi Singida ambako kunajengwa substation kisha kuunganisha na njia kubwa ya umeme (gridi) inayojengwa kutoka Iringa kwenda Shinyanga. Mpaka hapo hakukuwa na mpango mwingine wa kusafirisha gesi kwenda Dar. Mnamo mwaka 2010 wakati wa kampeni, JK aliinadi plan hii niliyofafanua hapo juu. Sasa leo hii mpango huo wa kuweka mifuo Mtwara umekufa, badala yake linajengwa bomba, kinyume na ahadi ya raisi, ndio sababu walioahidiwa wamechachamaa. Ni kwa makusudi kabisa serikali hawasemi kitu hiki kwa raia, si Muhongo wala Mgimwa anaegusia plan hiyo hapo juu ambayo wameiweka kapuni kwa kupendelea 10% ya Wachina ambao ndio waliotengeneza bomba, ndio wanaolilaza kutoka Mtwara hadi Dar na ndio wenye mikataba mingine kibao ya bomba hilo. Huo ndio ukweli wa moja ya vyanzo vya vurugu za Mtwara.
Hutawasikia akina Nchimbi wanagusia suala hili, badala yake wanatafuta mchawi nje ya serikali, ilhali wa'chawi ni wao wenyewe.
 
kuchoma nyumba kunahusika vipi na gesi. acheni kuharibu mtwara jamani , mfano mbaya ni Syria wanateketeza mali zao wenyewe.
 
Mie nimekuwa more dissappointend......

Namshukuru Mungu nimeshuhudia awamu zote za marais katika nchi hii, ila huyu baba ni kiboko, sikuwahi kufikiria hata siku moja Tanzania tutagombana eti kwa sababu ya dini, sikuwahi kufikiria hata siku moja eti Tanzania yatatokea haya yanayotokea mtwara, najua hata awamu zilizopita viongozi walikuwa wanaiba lakini kwa huyu wanaiba mchana kweupe hata aibu hawana. Ninasikitika sana juu ya taifa langu Tanzania lakini nina huzuni kubwa sana juu ya watoto wangu sijui mwisho wao utakuwaje, Please Kikwete ona aibu taifa linaangamia

Kuna Professor wangu mmoja mwaka 2005 nikiwa chuo alinambia "Youngman, I know many Tanzanians will Vote Kikwete in for Presidency out of AD POPULUM (Mob psychology or out of emotions) but I tell you Son, Kikwete is going to be a great disappointment.

Ndo tunayashuhudia sasa. I'm no longer proud of being a Tanzanian, totally disappointed!
 
Taarifa zinaonesha kuwa sasa Polisi wa Mtwara ndio wafanyafujo huko.Wanavamia;wanapora;wanakamata;wanapiga mateke,ngumi na risasi;wanachoma samani za majumbani na kunyanyasa raia.Wana kila aina ya kutamba watakavyo.


Polisi wameshika hatamu Mtwara. Huo ndio udhibiti hasa utakiwao na Serikali kuzima vuguvugu ya Mtwara? Majukumu ya Polisi ndiyo hayo? Hii si kumwagia mafuta kwenye moto uwakao sasa Mtwara? Ndiyo zamu kwa zamu?


Vyanzo vya habari: VoA,BBC,DW na wakazi wa Mtwara.
 
Hivi kweli tunaanza kuuana badala ya kujadiliana,kueleweshana na kukubaliana? Hakika mungu anaona ukatili huo na malipo yake ni humu duniani...imagine mama na kiumbe kinachotarajia kuiona nuru ya dunia? Pia kijana mwanafunzi? Poleni wafiwa.naandika hii comment kwa uchungu na machozi kunilengalenga nikijaribu kuchukua nafasi ya waliofikwa na misiba hii pasi na sababu za msingi
 
unajua kabisa kingereza hukijui sasa kwa nini ulazimishe kwani ungeongea kiswahili tungekuona huna point ....tena ungeeleweka na wengi kuliko ulivyokunya hapo

Umenivunja mbavu ndugu yangu.
 
few examples of STUPID PEOPLE in groups
  1. Wanamtwara wanaodai wasichokijua,
  2. CHADEMA na wafuasi wake wote ukitoa zitto na mnyika

Okey, mimi na wewe tunajua kuwa mikataba ya gas imesainiwa bila kuundwa sera ya gas.
Je, kwasababu watu wa mtwara hawajui wanachodai hawastahili kusikilizwa????

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Huo ndio mtindo wa CCM ndio maana mukikataliwa hamuamini kwamba ulegelege wenu wa kuendesha serikali umewafikisha mulipo

nina mashaka na upeo wa kfikiri wa huyu anayejiita mimi kum...., wakati watu wanajadili mustakabali wa nchi lenyewe linaleta ushabiki wa vyama kama baba yako katibu wa CCM kakae na baba yako mdanganyane ----- wewe!
 
kuchoma nyumba kunahusika vipi na gesi. acheni kuharibu mtwara jamani , mfano mbaya ni Syria wanateketeza mali zao wenyewe.
Kiongozi imara hasubiri mpaka nyumba zichomwe ndo atoe tamko.

Ni nani asiyejua kuwa taarifa za vurugu za mtwara zilishazagaa mapema kufanyika endapo bajeti haitakua na majibu kwa wana mtwara??


Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
  • Thanks
Reactions: ram
Kweli wee ni mburulalaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa... tena ungekuwa karibu yangu ningekuchapa mboge la kofi
Taarifa kutoka maeneo mbalimbali ya mji wa mtwara zinasema, wanaoendesha zoezi la uchomaji wa ofisi za CCM, nyumba za Mawaziri na taasisi za serikali ni kikundi maalum cha vijana wa CHADEMA na ambacho kinaratibiwa na kiongozi mmoj wa CDM ambaye anatokea mikoa ya nyanda za juu kusini. Swali ni je vijana wa CCM wakiamua kujibu mapigo kwa kusaka ofisi za CDM kweli Mtwara kutakalika? Inasemekana CDM viongozi wa CDM katika mji wa Mtwara wameelekezwa kufunga ofisi zao na kuzipa ulinzi wakati vijana wao wanapotekeleza uchomaji wa ofisi za CCM na taasisi za serikali.

Wito kwa serikali: Ichukue hatua za haraka kwani endapo CCM nao wakiamua kujibu kwa kuchoma ofisi za CDM hakika Mtwara hakutakalika na inawezekana kabisa vurugu hizo zikasambaa hata katika mikoa ya jirani.
 
Sasa kwa nini anawatumia mawaziri wake kulinde hisa zake? aende mwenyewe bs akayamalize kiutu uzima,ujue ukiwa mrafi basi usiwe mchoyo,naukiwa mchoyo usiwe mrafi,navyojua gesi haikomei kinyerezi tu inaenda mpaka tegeta,sasa tegeta ni road ya kwenda wapi? na bandari inajengwa wapi?
 
Ngoja na sisi wa ziwa Victoria tuzuie maji yanayoenda shinyanga, maana nasikia eti wanataka wayafikishe hadi dodoma.
Nasikia Iringa nao wanataka kugoma Ulanzi usipelekwe Mbeya.
Nasikia pia Kyela na Mbarali wanataka kugomea Mchele a.k.a Punga usiende kuuzwa DSM.
 
sasa yataanza kuchomwa moto na yenyewe... WATANZANIA SI MABWEGE TENA!!
Watanzania si mabwege tena kwa hiyo unataka kusema hao wanamtwara ambao wameamka kutoka kwenye ubwege walionao kwa kuchoma nyumba za watu kuharibu mali kuua kuharibu miundo mbinu ndio wanafanya sahihi kisa gesi unaona wanafanya sawa. kweli wewe bwe.ge wa fikira. Omba kunyimwa utajiri kuliko kunyimwa hekima na busara japo kiduchu maana ndio unaonekana bwe.ge maradufu. Ushabiki usio na tija.

Sasa walichofanya kimewapa faida gani mpaka sasa kuvunja madaraja n.k huku wanadai mtwara iko nyuma kimaendeleo kwa hiyo wanayoyafanya sasa ndio maendeleo wanayoyataka.
 
Kwa mara ya kwanza nakiri kulichukia Jwtz kama ninavyowachukia polis...

Kitendo cha kuongoza kuchoma nyumba za raia kwa maslai ya wanasiasa kinakera na kuumiza roho.!!!

Jeshi letu limekuwa jeshi la wanasiasa.

Bora waende kongo wakafie mikononi mwa M23.!!
 
Watu waliuawa kwa kupigwa risasi ni wengi wanafika hata 20, na polisi pia wameuawa zaidi ya kumi. Source ni jamaa zangu waliopo huko. mfano jana kuna maiti 4 zimefika masasi kwa ajili ya mazishi. Mungu ibariki mtwara na tz kwa ujumla.
 
MBONA WAMETANGAZA KUWA NI WAWILI TU?.....Mkuu una uhakika?
Hivi kuficha idadi kamili ya wanaofariki katika majanga ni propaganda inayomsaidia nani?
Mpaka umri huu sijajua maana ya kitendo cha aina hiyo!
 
Back
Top Bottom