AirTanzania
JF-Expert Member
- Mar 17, 2011
- 1,139
- 1,040
- Mabasi 5 ya Champion yamebeba Wanajeshi yako njiani yanakuja.
- Serikali yatoa tamko yasema watu 91 wanashikiliwa.
- Bunge laahirishwa tena. Kupisha uchunguzi na kuepusha uchochezi kutoka kwa baadhi ya wabunge. (Kwa mujibu wa Spika)
- Maeneo ya Magomeni, Chikongola, Nkanaledi, Mikindani maaskari wanaingia majumbani mwa watu na kumsomba mtu yeyote ambaye ni mwanaume awe amehusika awe hajahusika na kumkamata. Pia inaripotiwa na uhalifu unafanywa na maaskari hao hao. Jambo linaloamsha hisia kwa wananchi.
- RPC anaongea na vyombo vya habari na kuwasihi wananchi waende makazini. Lakini kiuhalisia hali sio shwari.
- Mahakama ya mwanzo ya Mitengo imechomwa moto
- Mpaka sasa ni vita baina ya wananchi na maaskari. Mabomu yamesikika pamoja na milio ya risasi masaa 24. Na milio ya Risasi na mabomu inaendelea kusikika.
- Raia wapatao 7 wameripotiwa kufariki (wengine walipelekwa hospitali ya Ndanda Ndogo na mmoja ameripotiwa kupokelewa Ligula.
- Nyumba za viongozi zinaendelea kuchomwa moto.
- Majibizano baina ya Polisi na Raia yanaendelea maeneo ya Magomeni, Nkanaledi na Mikindani.
- Maduka yamefungwa na hakuna huduma zozote
- Barabara zimewekwa vizuizi magogo na matairi yamechomwa moto. Hakuna njia ya kupita.
Update: Mabomu yametulia. Hali ya ukimya imetawala.
Update:
- Maduka maeneo ya Magomeni yamechomwa moto ikiwamo pia mali za Askari magereza na uhalifu ukifanyika vidole vinawaelekea Polisi.
- Afisa Usalama wa Taifa ambaye anamiliki nyumba ya wageni naye amevamiwa na kuporwa mali ikiwamo fedha katika gesti yake. Haijajulikana ni kiasi gani cha mali kilichopotea.
- Mwanafunzi wa CHUNO afikishwa hospitali Ligula na majeraha ya risasi mguuni.
Update:
- Mwanamke anayekadiriwa miaka 25 mjamzito auawa kwa kupigwa risasi maiti ipo Ligula.
--Magomeni A hatuna amani, askari POLISI wanaingia nyumbani kwetu, wanatupiga na kutunyang'anya simu, yaani huku Magomeni hatuna amani kabisa, tumepotezana na watoto na hatujui hata wake/waume zetu wako wapi
--Mwanadada mjamzito alibakwa na askari Polisi kisha kupigwa risasi. Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Ligula, Mohamedi Kodi alithibitisha kupokea mwili wa mjamzito ukiwa na tundu tumboni, linaloaminika kuwa linatokana na risasi.
--Umati wa watu wengi wao wakiwa kinamama na watoto umemiminika kwenye Hospitali ya Ligula kukimbia msako wa nyumba kwa nyumba unaofanywa na polisi na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).
--Wakazi wengi wamelalamikia kitendo cha POLISI kuingia katika makazi yao, kuwapiga na kuwapora mali zao. Magomeni A askari wanaingia nyumbani kwetu, wanatupiga na kutunyang'anya simu, yaani huku Magomeni hatuna amani kabisa, tumepotezana na watoto
--Hadi sasa huduma za kijamii zimesimama, hakuna maduka yaliyofunguliwa, hakuna usafiri wa daladala wala pikipiki, mji upo kimya huku sauti za milio ya mabomu na bunduki ikitawala, wanajeshi waliovalia sare wametapakaa sehemu mbalimbali za mji wakiwa katika magari na pikipiki.
--Pamoja na Nchimbi kufika, Pia ndege kubwa ya jeshi nayo ilitua huku na wanajeshi walikuwa wakipakua vitu mbalimbali vilivyoaminika kuwa vifaa.
--Polisi wamechomba nyumba nyingi sana za raia maeneo tofauti baada ya Waziri Nchimbi kuwasili
==========================Kituo cha televisheni cha ITV kimerusha habari usiku huu kuhusu vurugu zilizojitokeza kwa takribani siku mbili huko Mtwara. Taarifa hiyo imelitaja waziwazi jeshi la Polisi kuhusika na uchomaji wa nyumba za raia na kufanya uharibifu wa mali katika kile kile kilichoelezwa kusaka wahalifu.
Mwandishi wa ITV aliyeripoti habari hiyo kutoka Mtwara amesema "...kwa upande mwingine askari Polisi wameonekana wakichoma nyumba katika kusaka wahalifu waliochochea vurugu hizo..."
Nimejaribu kuploud voice clip ya mwandishi huyo lakini naona network inasumbua. Naendelea kujaribu ikikubali nitaweka wakati mjadala unaendelea.
NB: Jeshi la Polisi limeshutumiwa kuendeleza ghasia za Mtwara badala ya kuzituliza. Imeripotiwa katika vyombo mbalimbali kuwa Polisi wameongeza maafa Mtwara. .
Matukio katika Picha
==========================