Updates: Yanayojiri Mtwara - hali bado tete (Mei 23/24, 2013)

Updates: Yanayojiri Mtwara - hali bado tete (Mei 23/24, 2013)

Wanajamvi kunakitu nashindwa kukielewa eti wanajeshi zaid wapelekwa mtwara je hiro ndo sululisho la tatizo hivi kweli rais ameshindwa kutoa Kauli ndogo tu Kua kiwanda kitajengwa mtwara mambo yakaisha? Na kulikua na haja gani hata kupelekwa polis Huko mpaka watu wanauwawa je wanafanya kwa Faida ya nani? Na Kama ya watanzania je hao wanaopigwa mabom na kuuwawa sio watanzania na waliokamatwa na kupelekwa mahakamani wana makosa gani? Je sisi wa mikoa mingine tujifunze nini kwa hii serikari yetu na mpaka Leo ni raia wangapi wameuwawa na serikari wakidai haki zao kweli nimeamini hii ni Hali mpya ya mauaji kasi mpya ya ufisadi na Maisha bora kwa kila fisadi na familia zao mnyonge mnyongeni but haki yake mpeni
 
katiba imewapa haki hiyo au ni ubabe, raia hao wasingekatalia gesi hiyo ila uporaji wa viongozi wetu umewapa mashaka kama wataambulia chochote wakiruhusu gesi kutoka, viongozi wetu ni majambazi wakubwa.wanashirikiana na jeshi la polisi kunyanganya mali za watanzania wote kwa manufaa yao binafsi. ndo maana wanamtwara hawana imani na viongozi waliopo kuwakabidhi mali hiyo kwani wanajua hawatafaidi tena. NAKUOMBEA MH.DR.WILBORD SLAA mungu akubariki ufike 2015 utuongoze kwa busara yako. kwa maana serikali ya ccm haina mbinu tena ya kututoa salama hapa tulipofikia
 
Umefika muda serikali kukaa na wananchi na kusikiliza hoja zao na kuzifanyia kazi maana zina mashiko kuliko kutumia nguvu na ubabe
 
Nadhani ni Wakati sasa Serikali itafakari upya mpango wake wa ujenzi wa bomba la gesi. Ni vyema iyo gesi ivunwe huko mtwara, plant ya kufua umeme ijengwe huko huko na kisha umeme usafirishwe kwa njia ya Nguzo.

Mkuu tatizo hela ya WAHISANI ishaliwa, sasa wakifanya kama wananchi wanavyotaka hawa WAHISANI waliohakikishiwa gesi huku Dar na kwingineko watarudishiwaje chenji yao!!
 
du mtwara nouma, yani hawataki kusikia gesi ikisafirishwa dar hata kwa bomba la peni. naanza kuiona tanzania ambayo sikuitarajia kuchafuka ila ni kutokana na mfumo wetu wa nchi. mungu tusaidie uwape hekima viongozi wetu, waache kujifikiria wao na wawafikilie wananchi.
 
hii shughuli ni nzito kwa serikali. huu sio upepo kama matukio mengine yalikwisha kuitwa ni upepo utapita. Nia thabiti, uwazi na ukweli vinahitajika kusuluhisha hili.
 
Ndugu yangu katafute kiugali chako na wanao ukalale mambo ya kupambana na serikali achana nayo haiwezi kukuwekea chakula mezani ht kama gesi inachimbwa uani kwako
 
Hawa sasa sio polisi wa tz bali ni m23
wanakolelekea utasikia wameanza kubaka raia
 
Nadhani ni Wakati sasa Serikali itafakari upya mpango wake wa ujenzi wa bomba la gesi. Ni vyema iyo gesi ivunwe huko mtwara, plant ya kufua umeme ijengwe huko huko na kisha umeme usafirishwe kwa njia ya Nguzo.

Naamini gharama za kusafirisha gesi kwa bomba kuja Dar na kisha kujenga plant kwa ajili ya kufua umeme ni kubwa kuliko ujenzi wa Plant huko huko Mtwara. Wanamtwara wanataka kufaidi 'Multiplier effect' ya ujenzi wa plant ya kufua umeme huko Mtwara na sio kwamba hawataki Watanzania wengine wafaida matunda ya gesi.

After all, Annual maintanance ya Bomba ni kubwa kuliko Annual maintanance ya nguzo za Umeme. Tutafakari!

Kwa bahati mbaya au nzuri tathmini ya kiuchumi na kifedha iliyofanywa kama msingi wa kuendeleza mradi wa bomba la Gesi Kutoka Mtwara hadi DSM ilibaini kuwa mradi wa bomba unafaida kubwa zaidi za kiuchumi na kifedha kuliko kuzalisha umeme Mtwara na kuusafirisha kuja DSM.
 
Wakuu leo Mtwara hali nI mbaya zaidi kuliko jana kwa vitendo viovu VINAVYOFANYWA na askari wa jeshi la polisi.
Iko hivi;
-Polisi wanafyatua risai za moto kwa raia
-wanavunja mabanda ya biashara ya raia na kupora mali, fedha na chochote kilichopo KISHA KUYACHOMA MOTO
-Wanasachi na kunyang'anya fedha, simu na chochote alichonacho mfukoni kisha wanamjeruhi vibaya yeyote wanayekutana naye bila kujuwa kuwa ni nani
-wanavunja nyumba za raia na kubeba wanachoona kinawafaa

NB: Vijana wengi hasa wa mitaa ya Majengo, Mdenga na Magomeni wameyakimbia makazi yao wako mafichoni nje kdogo ya mji
MapoliCCM ndio zao hizo hawaoni wananchi kama watu,ni bora mara kumi wanajeshi waingie Mtwara kutuliza wana Mtwara!!
Mkuu wa kaya naona mambo yanamshinda, angeliweza kutumia lugha ya busara na hekima kuliko kuhamasiusha mapolisiCCM waharibu mali na vitu vya watu!!!

 
Back
Top Bottom