Kituo cha televisheni cha ITV kimerusha habari usiku huu kuhusu vurugu zilizojitokeza kwa takribani siku mbili huko Mtwara. Taarifa hiyo imelitaja waziwazi jeshi la Polisi kuhusika na uchomaji wa nyumba za raia na kufanya uharibifu wa mali katika kile kile kilichoelezwa kusaka wahalifu.
Mwandishi wa ITV aliyeripoti habari hiyo kutoka Mtwara amesema "...kwa upande mwingine askari Polisi wameonekana wakichoma nyumba katika kusaka wahalifu waliochochea vurugu hizo..."
Nimejaribu kuploud voice clip ya mwandishi huyo lakini naona network inasumbua. Naendelea kujaribu ikikubali nitaweka wakati mjadala unaendelea.
NB: Jeshi la Polisi limeshutumiwa kuendeleza ghasia za Mtwara badala ya kuzituliza. Imeripotiwa katika vyombo mbalimbali kuwa Polisi wameongeza maafa Mtwara.
mtandao wa GUMZO LA JIJI umeripoti mwanamke mmoja aliyefariki leo mchana na kufanya idadi ya vifo kuwa viwili, kuwa alibakwa na askari kadhaa (licha ya kuwa mjamzito) na baada ya kutimiza haja zao wakampiga risasi, kisa tu mumewe alidaiwa kuhusika kwenye vurugu hizo, na walimtafuta wakamkosa hivyo wakaamua kuelekeza hasira zao kwa mkewe na kiumbe kisicho na hatia kilichokua tumboni.