Updates: Yanayojiri Mtwara - hali bado tete (Mei 23/24, 2013)

Updates: Yanayojiri Mtwara - hali bado tete (Mei 23/24, 2013)

Si mnamwita rais dhaifu sasa akiwashikisha adabu mnasema mkatili.., well done kikwete gesi sio yao peke yao..,
 
Naona umeamua kuyapa sifa ya hayo maandamano kuwa haramu. Hayo maandamano yalikuwa haramu kwa nani? Kwa wale waandamaji au kwa yule maandamano yalikuwa yanamwendea? Na kama ni yule ambaye maandamano yalikuwa yanamwendea ni kwa namna gani umeweza kuamua kuwa yalikuwa haramu?

yalikua haramu kwakua walioandamana hawakupata kibali cha kuandamana! nambie ww usichokielewa kwenye uharamu wa kuandamana bila kibali!

Kwanini udai haki bila kutii mamlaka? usiwe mpumbavu wa kupandikizwa na watu wengine, utajuta kufuata vibendera vya vyama vya siasa, just be yourself!!
 
Jana si ulimsikia amiri jeshi mkuu wao akiwaambia wasiishie kung'oa meno na kucha tu bali wang'oe na mapembe pia.

Badala ya kutafuta ufumbuzi wa kudumu kwa tatizo lililo mbele yao wao wanaongeza chuki, hasira na uhasama ambao hautaisha leo wala kesho.

Hapo ndipo utapojua kwanini DRC (Congo, Somalia, Siera, Sudani kuna vita ya wenyewe kwa wenyewe
 
yalikua haramu kwakua walioandamana hawakupata kibali cha kuandamana! nambie ww usichokielewa kwenye uharamu wa kuandamana bila kibali!

Kwanini udai haki bila kutii mamlaka? usiwe mpumbavu wa kupandikizwa na watu wengine, utajuta kufuata vibendera vya vyama vya siasa, just be yourself!!

Asante sana kwa kuniita mpumbavu, natumaini kuwa wewe una busara sana. Mtu mpumbavu hapaswi kuongea na mtu mwenye busara. Nakutakia siku njema na maisha mema.
 
Rubish! kumbe kuna watanzania wengine ni shetani kuliko freemason, unawezaje kumshawishi mwenzio ale ugali wakati kunawatanzania wenzetu hawana uhakika wa kufika hata saa 7 mchana?! Huo ugali unashukaje? Au wewe ni Mrundi wewe! Hivi unavyoambiwa watu wanakufa unadhani ni movie? Hii nchi sio ya serikali, We are going to fight mpaka kinaeleweka. mimi binafsi tangu jana hata hamu ya kula imekatika hebu wewe chukulia familia yako ingekuwa ipo huko muda huu na wewe upo dar ungekula wewe? Au unabwatuka bwatuka tu! kesho serikali ikitaka mkeo utaipa coz ni serikali? While people are dying talk sencefull.
Haya ni majitaka tuuu mbona hujaenda kuwaunga mkono? Si ungeitisha basi maandamano hapo ulipo ya kuunga mkono tukakujua kazi kutia wenzako ujinga
 
Nyie ndo aina ya watu msioitakia mema nchi hii, tena unastahili kuvishwa tairi shingoni na kutiwa kiberiti.
Wewe unayeitakia mema hii nchi si ndio ungejivisha tairi ujipige kiberiti tujue uko siriaz mbona kule Tunisia walifanya au kubwabwaja tuuuu kwa vile mdomo haulipiwi bili
 
Tukisema ukweli, mnasema CDM chama cha fujo. Hv mwanamke mwenye mimba kupigwa risasi hukumu ya ccm ninini mbele ya mwenyezi mungu.
 
Taarifa zinaonesha kuwa sasa Polisi wa Mtwara ndio wafanyafujo huko.Wanavamia;wanapora;wanakamata;wanapiga mateke,ngumi na risasi;wanachoma samani za majumbani na kunyanyasa raia.Wana kila aina ya kutamba watakavyo.


Polisi wameshika hatamu Mtwara. Huo ndio udhibiti hasa utakiwao na Serikali kuzima vuguvugu ya Mtwara? Majukumu ya Polisi ndiyo hayo? Hii si kumwagia mafuta kwenye moto uwakao sasa Mtwara? Ndiyo zamu kwa zamu?


Vyanzo vya habari: VoA,BBC,DW na wakazi wa Mtwara.
hiyo taarifa ya BBC ,VOA za saa ngapi.

Hizo risasi hao wanaopigwa tangu jana wamefikia mia ngapi?au ni walewale wahanga wawili bado wanaongezewa risasi?
 
Mbona wanasema ni raia wawili tu? ipi ni habari sahihi hapa? Tuambiwe ukweli tujue moja.
"Raia wapatao 7 wameripotiwa kufariki (wengine walipelekwa hospitali ya Ndanda Ndogo na mmoja ameripotiwa kupokelewa Ligula".
Naona taarifa hii nchimbi hakupewa.
 
Media wanaogopa kufungiwa wakisema ukweli mana magamba ndo vile.
si kweli kama ndivyo mbona blogs haziupdate?hata humu jamii update za humu za akina mtwaragesi,maembe mabichi ni update fake za kuchochea kwani tayari misimamo yao kuhusu gas inafahamika nda yawazekana ndo maorganiser wenyewe wa vurugu za mtwara.
 
Mbona wanasema ni raia wawili tu? ipi ni habari sahihi hapa? Tuambiwe ukweli tujue moja.
mkuu habari za humu usichukulie serious kivile..vyombo vingi vya habari viko mtwara,magazeti,blogs,radio,TV etc,kama kuna mauaji zaidi ya hao wawili pangejulikana tu.humu watu wako kishabiki zaidi usiamini update yeyote bila kuicomfirm na media zingine.
 
yalikua haramu kwakua walioandamana hawakupata kibali cha kuandamana! nambie ww usichokielewa kwenye uharamu wa kuandamana bila kibali!

Kwanini udai haki bila kutii mamlaka? usiwe mpumbavu wa kupandikizwa na watu wengine, utajuta kufuata vibendera vya vyama vya siasa, just be yourself!!

haki haiombwi Bali huchukuliwa. ulitegemea serikali hii tuliyonayo ingetoa kibali cha maandamano?. Kamwe
hiyo haiwezi kutokea, hivyo wanamtwara sana kilasababu ya mutants walichokifanya Uli sauti Yao na Madai Yao yaweze kusikilizwa. ukiyaita haramu au vurugu hiyo yote ni tafsiri yako lakini ujumbe umefika na umesikika.
 
Hali ya utulivu bado haijapatikana mkoani mtwara kwani usiku wa kuamkia leo wanakijiji wa kijiji cha Msimbati kilichopo Mtwara vijijini mkoani mtwara sehemu ambayo ugunduzi wa gas ulifanyika.

Wamelipua ofisi za idara ya uhifadhi bahari Marine conservation kwa bomu ambalo linaonekana kuwa na KG nyingi wa kuwa jengo hilo kubwa na la kisasa limesambaratishwa kabisa. Usiku huo huo wanajeshi wa jeshi la wananchi J.W walifanikiwa kufika eneo la tukio,na leo asubuhi cruiser nne za F.F.U zimeelekea eneo hilo la Msimbati kwa ajori ya kurudisha utulivu eneo hilo.

Maeneo ya Magomeni mamia ya watu yamejikusanya kutafakali kitendo cha askari polisi kuchoma nyumba za wananchi na kupora mali za wafanyabiashara wasio kuwa sehemu ya vurugu hizo. Wananchi wanaonekana kutokukubaliana na kilichofanywa na polisi hao na kujipanga kulipiza kisasi. Wilaya ya Newala kumelipotiwa vijana kuingia barabarani na kuchoma moto matairi huku kauli mbiu ikiwa ile ile GAS HAITOKI MTWARA

Kuna uwezekano mkubwa machafuko kuenea sehemu mbalimbali za mikoa ya kusini kama busara hazitatumika.

Ova
 
haki haiombwi Bali huchukuliwa. ulitegemea serikali hii tuliyonayo ingetoa kibali cha maandamano?. Kamwe
hiyo haiwezi kutokea, hivyo wanamtwara sana kilasababu ya mutants walichokifanya Uli sauti Yao na Madai Yao yaweze kusikilizwa. ukiyaita haramu au vurugu hiyo yote ni tafsiri yako lakini ujumbe umefika na umesikika.

hata hivyo me nakosaga kuwaelewa nyie munaoshabikia watu kufa mtwara, utakuta mnasema vurugu ziendelee na watu wakifa mnasema serikali haijatenda haki, wakiachwa bila kupewa kichapo mnasema serikali zaifu, ukipewa nafasi ya kusikiliza malengo ya serikali hutaki kuelewa unataka unachosema ndio kifanyike na unahamasisha vurugu!
me nafikiri kauli ya punda haendi bila mchapo inabidi itumike kwa sasa ndo maana hata wanafunzi wetu wanafeli kwakuendekeza midomo badala ya kusoma! hata adhabu ya viboko mashuleni nadhani inakemewa lakini bado tunaihitaji
 
Nikimfikiria yule mama mjamzito aliyebakwa na kupigwa risasi na polisi............ Naichukia nchi yangu
 
Back
Top Bottom