Ciril
JF-Expert Member
- Jan 10, 2011
- 8,558
- 7,168
Wakuu leo Mtwara hali nI mbaya zaidi kuliko jana kwa vitendo viovu VINAVYOFANYWA na askari wa jeshi la polisi.
Iko hivi;
-Polisi wanafyatua risai za moto kwa raia
-wanavunja mabanda ya biashara ya raia na kupora mali, fedha na chochote kilichopo KISHA KUYACHOMA MOTO
-Wanasachi na kunyang'anya fedha, simu na chochote alichonacho mfukoni kisha wanamjeruhi vibaya yeyote wanayekutana naye bila kujuwa kuwa ni nani
-wanavunja nyumba za raia na kubeba wanachoona kinawafaa
NB: Vijana wengi hasa wa mitaa ya Majengo, Mdenga na Magomeni wameyakimbia makazi yao wako mafichoni nje kdogo ya mji
Nnaiunga mkono taarifa hii ni ya kweli kabisa,kazi ya polisi ni kuvunja mabanda(maduka)ya biashara na kuiba kila kilichomo humo ila polisi wanapowaona JWTZ huwa wanakimbia.Taarifa sahihi niliyopewa na rafiki yangu ninaefanya nae biashara ni kuwa wananchi wengi(hasa kina mama/watoto/na wazee)wengi wao wanakimbilia kuelekea katika kambi ya jeshi la wananchi wa Tanzania iliyopo Nalindele kwa usalama zaidi.Polisi wanamkamata kila kijana watakaemwona sehemu yeyote wanampiga vibaya na kuondoka nae,polisi pia wamemuua mama mjamzito kama mleta uzi alivyosema na ni kweli sio uongo.
Nnasikitishwa na baadhi ya kauli za viongozi wa Serikali wanosema Mtwara hali imetulia wakati polisi bado wanatekeleza unyama wa hali ya juu dhidi ya raia.Kama nchi tumefikia mahali pabaya sana,kwa kauli ya jana ya raisi wa nchi hii ni kama amewabariki polisi wakafanye mauaji/kupora mali za wananchi,sababu wanajua hakuna watakachofanywa.