Uliza chochote kuhusu Rwanda

Uliza chochote kuhusu Rwanda

Kuna ukweli gani kuhusu binti wa PK kuzuiliwa kuolewa na chaguo la mtima wake ambae ni kijana wa kimaskini kisha kulazimishwa kuolewa na mwanaume mwingine ambae ni mtoto wa kigogo , hii inaonyesha ni kwa namna gani serikali chini ya Rais wenu haiheshimu watu wa tabaka la chini na pia kutoheshimu faragha za watu, hili lina ukweli wowote ama niache kuhudhuria vikao uchwara za vijiweni???
 
Pia huko Rwanda kuna wazee wa kusifia kama huku kwetu, na pia zikiwepo shughuli za kichama au kiserikali wasanii na watu mashuhuri hujutokeza kusifia na kutoa pambio za kingese, mzee PK huwa ana react vp anaposifiwa sifa za kindezi kama huku kwetu akisifiwa na mtu, mtu huyo huramba teuzi???
 
Kitu gani cha kawaida kujadiliwa na raia lakin serikali haipendi kuona likijadiliwa?
Mambo gani matatu ambayo serikali ya rwanda ni dhaifu kwayo?
Tabia gani mbaya ambayo wanyarwanda wamezifanya kama tamadun, kama watz walivyo machawa chawa, waongo waongo na wapenda rushwa???
Maswali magumu kama nondo wangu.

-Kuhusu kitu serikali haipendi kuona kikijadiliwa na raia na serikali haipendi, kukaa na kubweteka kwamba kuna mashirika yatatoa misaada, kwamba kisa umesoma lazima upate ajira, kwa ujumla haipendi kuona raia wakipoteza muda kwa mambo yasiyo na manufaa kwao binafsi na kwa taifa kwa ujumla.

-Mambo matatu ambapo serikali ni dhaifu:
a. Wala rushwa wakubwa wakubwa hawashughulikiwi kama wadogo,

b. Kuna kitu kinaitwa targets. Bila kujali huyu ana hali gani, michango ni lazima. Binafsi nakubaliana na serikali kuchangisha fedha hizo, lakini angalau raia wakalishwe, waelezwe kwa nini michango hiyo. Katika vita vinavyoendelea huko mashariki mwa DRC, wanyarwanda, hasa wakazi wa Rubavu(Gisenyi), ndo mashahidi wa ushuru na tozo hizo, japo lilikuwa jambo la siri. Ila, nadhani kwa sasa kila mtu anapeleka ushuru wa watu bila hata kukumbushwa, na wa kuchangia anachangia bila shurti.

c. Udhaifu mwingine naouona, ni kuhusu miundo mbinu. Hasa kama mijini, utakuta ujenzi wa barabara, wahusika hawawazii miaka hata 100 mbere, jambo linalosababisha tena kuhamisha watu mara kwa mara. Kwa kifupi niseme kama ni mipango miji.

d. Udhaifu mwingine nijiongezee wa nne, ni swala la fidia kwa raia ambao mari zao zimeharibiwa wakati wa ujenzi na utekelezaji wa miundo mbinu. Taratibu nyingine zinawaumiza raia, mpaka miaka zaidi ya 10 unakuta kuna mtu hajalipwa fidia yake.

e. Kuhusu tabia ambazo watu wamezifanya kuwa kama tamaduni, uhuru uliopitiliza unasababisha watu kujisahau. Mfano ni kama raia na vyombo vya usalama. Wananchi wapo karibu sana,tena sana na vyombo hivyo, lakini utakuta wengine wameleta dhalau za kijinga. Mambo ya uchawa, Rwanda haina. Kwa sababu bado ni nchi changa, ambayo bado inajijenga katika nyanja zote, hivyo haijafikia ile hatua ya watu kushiba na kuanza kujigamba. Pia, historia yake, hakuna anaetaka ijirudie, hivyo kila mtu yuko makini sana na maisha ya nchi. Si viongozi tu, hata raia wenyewe.
 
Kuna ukweli gani kuhusu binti wa PK kuzuiliwa kuolewa na chaguo la mtima wake ambae ni kijana wa kimaskini kisha kulazimishwa kuolewa na mwanaume mwingine ambae ni mtoto wa kigogo , hii inaonyesha ni kwa namna gani serikali chini ya Rais wenu haiheshimu watu wa tabaka la chini na pia kutoheshimu faragha za watu, hili lina ukweli wowote ama niache kuhudhuria vikao uchwara za vijiweni???
Ingekuwa hivyo, pengine angekuwa ameolewa na watu wengine kutoka familia za juu au wanajeshi.

Kagame hana mamlaka ya kumchagulia mtoto wake wa kumuoa.

Unachokiongelea, ni stori ya kijiweni
 
Pia huko Rwanda kuna wazee wa kusifia kama huku kwetu, na pia zikiwepo shughuli za kichama au kiserikali wasanii na watu mashuhuri hujutokeza kusifia na kutoa pambio za kingese, mzee PK huwa ana react vp anaposifiwa sifa za kindezi kama huku kwetu akisifiwa na mtu, mtu huyo huramba teuzi???
Hahahahahaha, asante sana kwa swali zuri.

PK, ni mwanajeshi, maisha yake yote, ni ya miti kasi, kwa hiyo, yeye anaamini bado hajafika anakotaka. Kumsifia sifia, wewe pia unatakiwa uoneshe hizo shangwe unazoleta, mchango wako ni upi. kama hakuna, kazi unayo. Na ndo maana, kuanzia viongozi wa ngazi za juu,za jeshi, ukienda ndivyo sivyo, na ikaonekana ulikusudia, hana namna. Unapata unachostahili. Wasanii watajitokeza ndio,ila mambo ya furani ni mwandani wa chama, atakuja kusifia sifia, hakuna.
Watu hujaa kusikiliza hotuba zake na maneno ya kutia moyo. Ndo alivyo, hakubali kushindwa. Anaamini ukithubutu, unaweza.
 
Nimesoma maandiko yako unaandika kiweledi sana hadi nikasema unatumia msaada wa AI au Co Pilot Labda
Any way vichwa vya watu vinatofautiana sio wote wanajibu kwa msaada wa computer 🖥️ huenda ni brain yako kweli
Sasa nisaidie kitu I'm serious nataka Kuja fungua duka rwanda je eneo la mjini kama kariakoo linaitwaje na bei za fremu zipoje kwa mwezi, na pia mzunguka wa duka la nguo special za watoto, au za kike na kiume ni zipi zinauzika zaidi
Na pia procedure gani unapaswa kufuata na mgeni awe na mtaji wa kiasi gani kufungua biashara huko
Na Regulation za Huko zipoje
 
ungeanza wewe kujiheshimu sio unakuja hapa na stress za maisha unaleta mdomo mrefu kama mwaka wa njaa
Jamani eh, uzi wangu unamruhusu kila mtu kutoa maoni yake, hivyo nisingependa kuona kuna ugomvi baina ya watu hata wasiofahamiana. Najua wazi, kuna wengine wanapoteza muda tu bando wanalo la uhakika, na wenyewe majibu yao ninayo karibu.
 
Unaenda mbali Sana. Weka akiba ya maneno.
Ukweli unauma Jeshi tulikuwa nalo zamani. Sisi ndio tuliwapa mbinu za kivita wapigania uhuru wa Afrika Kusini,Msumbiji, Angola na Namibia. Lakini leo hii tumeshindwa kuwapiga magaidi walioua raia wa Tanzania Msumbiji. Tumeshindwa kuweka amani (sio vita) Goma mpaka kanali anakimbia vita mpaka wa Rwanda. Mnaotetea JWTZ ndio wale wale mnaotetea UDSM. Najua kuna watanzania wanafikiria kuwa UDSM ndio chuo bora East and Central Africa. Na kuna. Watanzania waliolala wanadhani JWTZ ndio ina Infantry bora duniani. 😂😂😂😂😂😂 Nchi yetu imeshuka kiwango sana. Tukiendelea hivi ndani ya miaka 30 tutakuwa kama Congo.
 
Nimesoma maandiko yako unaandika kiweledi sana hadi nikasema unatumia msaada wa AI au Co Pilot Labda
Any way vichwa vya watu vinatofautiana sio wote wanajibu kwa msaada wa computer 🖥️ huenda ni brain yako kweli
Sasa nisaidie kitu I'm serious nataka Kuja fungua duka rwanda je eneo la mjini kama kariakoo linaitwaje na bei za fremu zipoje kwa mwezi, na pia mzunguka wa duka la nguo special za watoto, au za kike na kiume ni zipi zinauzika zaidi
Na pia procedure gani unapaswa kufuata na mgeni awe na mtaji wa kiasi gani kufungua biashara huko
Na Regulation za Huko zipoje
Asante sana.

Mimi situmii chochote tofauti na tikiti langu(kichwa). Na nimeanzisha huu uzi baada ya kuona watu wengi wanaijua Rwanda tofauti na ilivyo. Ulikua muda wangu wa kuwapa ukweli(na vidonge pia 😀 😀 😀 😀 ).

Eneo la mjini, linaitwa Quartier Matheus (Soma Karitsie MATEUSI).

Maduka ya nguo, hasa ya jumla, utayapata humo. Ya rejaleja, Nyamirambo ndo mahali pake.

Bei za fremu, mpaka niulizie, najua hapo mjini kati, wanakodi kwa square meta. Kumkuta mtu ana fremu peke yake, mkuu, sijui umejipangaje, lakini huyo zipo. Nguo zozote zinauzika. Japo kwa ushauri wangu, kama una uwezo wa kufuata mzigo na kushusha mwenyewe, ni rahisi hata ukiwa na stoo. Kama unavyojua, wasioweza kwenda China, mizigo nguo hufuata Kariakoo. hata wa Congo pia huja Kariakoo.

Procedure si nyingi kwa sababu ni vitu vipo online, si mambo ya leo upo ofisi hii, kesho ile. Na gharama za kufungua biashara, ni 0. Labda kama utahitaji msaada kama stationary.

Raia wa EAC hawana masharti,unaona panakufaa, kaa. Kuna chochote unachoweza kufanya, uko huru.

Regulations, naomba unieleze unamaanisha nini
 
Vipi kuhusu mfumo wa elimu nchi Rwanda upoje, maana sisi huku tia maji tia maji mara tunaambiwa wahitimu wa vyuo vikuu waende VETA
 
Nimeelewa ufafanuzi wako, Nikisema regulations namaanisha napswa kwenda ofisi gani kuomba kufungua biashara Mfano.
Tanzania ukitaka fungua redio station inabidi Uende Tcra ndipo Uende brela
 
Nachohisi mmemuelewa vibaya aliewambia hivo.
Tatizo la mifumo ya elimu ya hizi nchi zetu, watu wanasoma ili waajiliwe.
Hawasomi kujiajili. Na nahisi lengo la aliyesema kwenda VETA, ni kutafuta fani inayoweza kukusaidia pale unapokwama kuajiliwa.
Ukipitia VETA, kuna kitu utajifunza na utaweza kuthubutu, lakini uwe na vyeti tu, af Division zenu za failure, utaishia wapi ndugu! Kwetu, kuna mfumo huo, na wanaobahatika kufika, wapo vizuri, iwe kwenye soko la ajira.

Natamani serikali yenu ingeruhusu tulete vijana wetu wakapate hizo nafasi mnazochezea.
 
Ok. Kwetu huendi popote. Internet inatosha. Registration zote ni online. Taasisi husika zimeunganishwa. Masaa 6, toka umeanza process, umeshapata kila kinachohitajika kuanza biashara.
 
Nachohisi mmemuelewa vibaya aliewambia hivo.
Tatizo la mifumo ya elimu ya hizi nchi zetu, watu wanasoma ili waajiliwe.
Hawasomi kujiajili. Na nahisi lengo la aliyesema kwenda VETA, ni kutafuta fani inayoweza kukusaidia pale unapokwama kuajiliwa.
Ukipitia VETA, kuna kitu utajifunza na utaweza kuthubutu, lakini uwe na vyeti tu, af Division zenu za failure, utaishia wapi ndugu! Kwetu, kuna mfumo huo, na wanaobahatika kufika, wapo vizuri, iwe kwenye soko la ajira.

Natamani serikali yenu ingeruhusu tulete vijana wetu wakapate hizo nafasi mnazochezea.
Asante sana mkuu, vipi Kuna ukweli wowote juu ya unafuu wa Internet Kutoka Starlink ukilinganisha na Hawa makampuni ya simu kama MTN maana tunaona tunapigwa sana na Hawa wenye Bando za wiki halafu ukifungua data Bando linakata ndani ya nusu saa
 
StarLink ni habari nyingine mkuu.

Japo, ukiachana na hiyo pia, kuna KTRN, ambayo inaprovide 4G. Ukilinganisha na kwenu, ni kitu kingine. 4G, GB30 ni kama elfu 15 kwenu. Na Ni 4G yenyewe hakuna cha mara ikakata, mara ikawa hivi.

Kwa upande wa Internet, bado Tanzania mpo mbali sana.
 
Kikubwa unikumbushe, kama kweli una nia. Maana kichwa changu mtandaoni ni kama kalakana la TAZARA
Nia ipo Ila lazma nipime upepo kwanza je inafanya kazi
Biashara ni All about profit so huo uwiano wa bei za fremu, mzunguka wa kazi,
Aina ya nguo zinazopendwa huko
Finally
Hali iliyojengeka vichwani kwa baadhi ya watu ni kuwa.. Rwanda ni kama North Korea yaan ukiwa Huko unahisiwa kama mpelelez, hivyo ukifanya mistake kidogo tu polisi unao maana walikutilia shaka Tangu siku unaingia.. Yaan upo monitored bila ww kujua.
Kuhusu hilo.
 
Rwanda kwenye swala la usalama inaanza na inajifuata. Utakumbana na changamoto nyingine za kimaisha,ila usalama wako na mali zako,sahau. unapeleleza kitu gani labda! Ukifanya kosa,utaadhibiwa kwa kosa lako,kama ilivyo kwa raia wengine. Na ukiwa mgeni, una thamani kuliko mzawa. Watadili na wewe tu pale unapoonekana kuhatalisha usalama, basi. Umelewa,utajua mwenyewe. Ni sawa na mnyarwanda aje kwenu, aanze kuchambua serikali isiyomhusu. Ila, wewe ni mtanzania, inajulikana, nani atakufatilia? Hayupo
 
Back
Top Bottom