Cha kukuongezea hapa, kwenye vita kuna udalali. Haijawahi kutokea,na haitawahi kutokea,amili jeshi apaishe ndege zilizojaa wanajeshi na vifaa bila faida.
Jambo la pili,hata uwanjani kati ya timu za mpira, mchezaji huumia,wengine tumewaona wakikata upepo kabisa. Hivyo,unaeenda kupambana nae, bunduki zake hazitoi njegere.
Kuna nchi kifo cha mwanajeshi mmoja,nje ya ncho yake,kinahitaji maelezo ya kujitosheleza. Kasoro tu pale ambapo kiongozi ana sababu zake.
South Africa umeiona (SAMIDRC)kwa ujumla. M23 wasingekuwa waungwana,jiulize wanajeshi waliotekwa leo hii wangekuwa wapi.
Tanzania haijawahi kuchokozwa,toka enzi za Idd Amin,na sidhani kama kuna mtu atawahi. Hakuna jirani mwenye ubavu huo.
Hivyo,pamoja na kukosa experience hiyo ardhini, angani hakika mpo vizuri. Miaka ya nyuma kuna FastJet kama 4 niliona zikifukuzana Mwanza🤣🤣🤣,hakika na mpya zipo. Zikitumika vizuri, zinafanya kazi.
Ila sasa, mtu unaanzisha vita,kuua raia ili iweje?
Mwisho na nikumbushie, kila upande unaoingia vitani, ujue kwamba kuna uharibifu mkubwa utatokea.