1, vp na Rwanda kuna festival za matamasha ya kimuziki kama fiesta, ukiondoa the ben ni wasanii gani wengine wanafanya vizuri ktk industry ya music, pia lile kundi la ambassadors of Christ lilifia wapi, na pia kuna lilifuatia nalo pia halikufua dafu ama ndio wanatoa ma song yanaishia nchini mwenu humo humo,
2, Pamoja na hilo Rwanda kuna wana harakati na wakosoaji wa serikali kama akina martin, Maria serungi, Hilda na watu kama hao pamoja na hilo, vp kuhusu wasanii wanaomba harakati kama Roma, nay wa mitego na wengine kama hao nanyi mpo nao pia???
3, Bunge lenu Lina jumla ya wabunge wangapi, wote ni wa chama kimoja tawala ama kuna wa upinzani pia??
4, ligi yenu ina jumla ya team ngapi zinazoshiriki ligi, pia mna derby baina ya team mbili kubwa ama ndio mnayo moja pekee???
5, niliwahi kusikia kuwa kuna baadhi ya wizara miaka ya nyuma kidogo PL aliweka wazungu waziongoze, vp bado wanaziongoza wizara hizo ama alishawatoa??
6, unapokutana na binti wa kinyarwanda/mwenye asili ya ki Tutsi Mara nyingi response Yao huwa kama ya dharau tofauti na wanavyosemeshwa na wanaume wa mfananio wao je, kuna mapandikizi gani ya malezi kutoka kwao kwenda kwa matabaka mengine kuyadharau linapokuja suala zima la kuonyesha kuvutiwa nao, ama ndio ile dhima mlionayo kuwa wa Tutsi mliumbwa na wengine tulichongwa(hii nina evidence nayo kuna binti alinijibu hivi pale kayanga mjini 😁😁)
7, tayari mpo ktk jumuiya ya EA lakini ajabu ni kuwa Mara nyingi nikiwa mipakani huko karibu na Rwanda masaa yanabadilika, kitu ambacho huwa kinanishangaza majira ya jua ni yaleyale yaani jua likiwa linachoma bongo ni sawa na nyie tuu pia hata likiwa linazama japo kuna tofauti kidogo sana… why hamjaamua kuyarudisha masaa ya Rwanda kuendana na yale ya sie wenzenu wa EA??
Dahhh maswali marefu kama shida za wakimbizi jamani: Ila ntakujibu tu
1. Zipo. Lakini haziwezi kuwa na shamla shamla kama za kwenu, kwa sababu huko hawana hela za kuchezea kama Bongo. Ka nchi kao kadogo, na vyanzo vya mapato kwa watu wa kawaida, si vingi kama kwenu, hivyo wanakula kwa mahesabu, huku nyie mnajua yote uliyo nayo ukiitumia, kesho unapata nyingine
😉 😉 😉
Kuhusu wasanii, wapo, na wanafanya vizuri kwa lugha yao, na wanaowaelewa. Kikubwa tu mdundo. Unadhani wangapi wanaelewa anachoimba Daimondi? mdundo upo, fresh. Ambassador of Christ ipo. Ila, haiwezi kuwa na nguvu kivile, kwa sababu waanzilishi wa miaka ile, sasa hivi wengine wana majukumu ya kifamilia, makazi ya mbali mbali, uwezo tofauti tofauti, hivyo si rahisi kutamba kama miaka ile.
Hilo lingine unalolisema, lipo ni la wanachuo(Chuo kikuu cha Kigali, ULK). Na wao ndo kama hivo, walipoanza wote walikua chuo, na sasa wamemaliza, na wametengana kimaisha kutokana na majukumu. Ila wao, kuna wakati wanakutana na kutumbuiza. Wakristo wanapata raha duniani(sio ile ya Kingwendu lakini).
2. Rwanda ni nchi changa ujue! Ukiachana na jina, ujue mwaka 1994, ilianzia zero,haikuwa na kitu. Ukisikia watu wanadai kwamba wakimbizi walirudishwa kwao kwa nguvu, nahisi haikuwa na watu zaidi ya milioni 4 kipindi hicho. Wasomi wengi waliuliwa, wengine walikimbia, kila sekta ilikuwa ni kuanza upya. Mpaka wa leo, ni nchi inayopiga hatua, lakini haiwezi kufika mlipo nyie kwa kila jambo.
Hao watu sasa, ukiweka kwenye mzani, utaona hakuna jipya wanaloliongelea, mbali na kutaka kujaza matumbo yao tu. Japo pia hata hao ni watu waliopo nje ya nchi, wala siyo watu wanaojua uhalisia wa maisha ya Rwanda kwa sasa. Na ndio maana, hata vinavyojiita vyama vya upinzani, vina misingi ya chama tawala, na wanachokifanya ni kuelekeza serikali wapi wanaona mapungufu. Sasa, kwa kuwa havina uwezo wa kufanya chochote, ikiwa kuna jambo kweli haliko sawa na lina tija, bunge linajadiliana kama la Rwanda, si kama la vyama tofauti. Bajeti ya jambo furani inapitishwa,inatafutwa, na jambo linatekelezwa.
Kuhusu wasanii, kumbuka wengi ni watoto wa juzi hata yaliyotokea hawayajui, hivyo, wanajitafutia tu cha kuwaendeleza kimaisha, basi.
Watu kama kina Maria Sarungi wapo. Japo pia kama ilivyo kwake, hata wa Rwanda wapo nje. Yupo mmoja yupo Ulaya huko, yeye ana serikali yake kabisa, ila ni yale tu ya kwamba mi ni mtoto wa furani, na mimi natakiwa nipate mgao kwa nchi yangu.
Mara, zamani tulikuwa na vitu hivi na hivi, laima tuendelee kwa mfumo huo. Sasa basi, mtu akiona ni tofauti, lazima atakuwa kama hao.
3. Bunge la serikali ya Rwanda, lina Jumla ya wabunge 80. Hapana, siyo wa chama kimoja, hata wa vyama vingine wapo.
4. Hapa ndo nimepotea, mambo ya mpira kwa kweli mi ni zero brain. Nachojua kuna timu mbili(APR na Rayon Sport), zikicheza, ujinga ujinga unaofanyika ni kama wa Simba na Yanga.
Kama kuna mtu humu anaeelewa(Najua wapo sema tu hawataki wajulikane), anisaidie akupe majibu ya hili kwa mapana.
5. Hawajawahi.
Kinachokuwagepo, ni kwamba kama inaoneka nchi haina watu wenye uwezo(hasa washauli), wanaajiri watu kutoka nje.
Japo pia, baada ya kuliona hilo, serikali mpaka leo inasomesha watu katika kila idara kuondoa kesi kama hizo za ukosefu wa watendaji wazawa, maana kutumia wageni, gharama zinakuwa kubwa.
Lakini pia, wapo ambao ni raia wa Rwanda, na wenyewe bila kujali rangi ya ngozi, wanaajiliwa kama raia. Nahisi miaka ya nyuma Rwanda ilikuwa na mwanajeshi mzungu.
6. Hili lipo aina mbili: Wanyarwanda, si wazinzi kama watanzania. Ile umekutana nae kwenye gari, mkishuka mnaenda Guest, sahau. Labda Bar, na penyewe ukute ni yule anaetaka hela. Hivyo, majibu utapewa kulingana na approach yako. Nachojua mimi, ni kwamba wengi wa wanawake hao, hufanya uzinzi tu kama sehemu ya maisha, wengine, idadi ndogo, ni yale makulumbembe yaliyoshindikana(yanayojua kuna mwanaume alieumbwa kuyahudumia), hayo na yenyewe yapo.
Kuhusu kwenda kwa matabaka mengine, mifano ni mingi ya familia za kitusi,zinazooana na familia za kihutu zilizohusika na mauaji ya familia za watutsi hao. Kwa hiyo, kuhusu kuangukia kwa tabaka lako, ni asilimia ndogo sana, na yenyewe hutoka kwa wazazi wao kuliko inavyoweza kuwa kwa watoto wao wenyewe. Kuhusu huyo wa Kayanga, pole kwa kuyatimba.
Mwanamke wa kinyarwanda,japo wengine mnawaita wanyarwanda kisa maumbile na sura zao, pengine ni wenu. Kama anajielewa, kumpata utasumbuka sana. Hata kwa kumdinya tu. Wengine bado wana heshima ya familia(malezi), wengine wanaridhika na maisha yao, sio yale madude yanayolilia Iphone huku kwao hata choo hawana. Hawaigizi, wanaishi maisha yao halisi.
Labda umpate anaejiuza, hapo sawa. Japo pia, unaweza mpata anaejiuza na akawa mstaarabu.
7. Hili swali, naomba urudi shule ukasome. kwa kaujuzi kidogo niliko nako, kupishana masaa kwa nchi, kunatokana na mistari wakoloni waliyochora, ambayo wengi hujua kwama GMT. Mfano hai, nchi ya Russia, najua inapishana masaa 11. Hivyo, kuna sehemu Russia huko, wakati jua linachomoza,wengine wanajiandaa kulala.
Congo, jirani, ina masaa matatu . Kama Goma ni saa tatu, Basi Kinshasa utakuta ni saa moja. Hivyo basi, wazo lako, haliwezekani kutokana na majira tunayotumia ni hayo ya wakoloni, na EAC ni jumuia sio nchi. So, ukiiweka pamoja, bado itakuwa na majira tofauti.