UB 40 ilianzishwa na vijan wachache huko Birmingham baada ya kukosa kazi kutokana na recession iliyoikumba Uingereza baada ya kupigana vita dhidi ya Argentina kugombania visiwa vya Falklands mwaka 1981 au 1982 nikiwa high school. Bendi ilianzishwa mwaka 1978 na wanafunzi kadhaa kama hobby kwao ila baada ya kugraduate wakajikuta hawana kazi nyingine kutokana na recession hiyo wakaanza kuishi kwa kupokea dole (unemployment benefit) ambapo walikuwa anatakiwa kujaza form
Unemployment Benefit Form Number 40 (UB40). Wakaamua kugeuza bendi yao kutoka hobby club kuwa biashara na kuiita UB40. Nyimbo nyingi walizotoa mwanzoni zilikuwa siyo tungo zao original bali zilikuwa ni covers za watunzi wengine. Huu wa Red Red Wine ulikuwa ni cover ya wimbo uliotolewa na Neil Diamond nadhani mwaka 1967 au 1968 hivi: nyumbani tulikuwa na santuri yake.
View: https://www.youtube.com/watch?v=tFyNHpNlECI