Ulisikia muziki huu kwa mara ya kwanza Ukiwa wapi?

Ulisikia muziki huu kwa mara ya kwanza Ukiwa wapi?



Wimbo huu ulikuwa maarufu sana mwaka 1988 na 1989 kwenye madisko ya Dar es Salaam nikiwa nimemaliza chuko kikuu na kuanza kujitafuta kimaisha. Wakati huo masharia yalikuwa hayana maana yoyote ile ule mdundo wake. Wimbo huu ulifutwa kwenye masikio ya wapenda muziki wakati huo na Judy Boucher kwa nyimbo zake za "Can't Be with You Tonight" na "You Caught My Eye". Nyimbo za Judy Boucher zilechelewa sana kuingia Tanzania ila zilipoingia zikatawala anga. Nyimbo hizo nadhani nimeshazipost huko nyuma hakuna haja ya kuzirudia hapa.
 
Kati ya mwaka 1992 na 1995 Taarabu ya TOT ilipamba moto sana kwa sababu za kkisiasa. Walitoa nyimbo nyiugi sna kipindi hicho kuelekea uchaguzi wa vyama vingi 1995, ila binafsi nilifuahia hizi tatu ambazo sikuzipata Youtube lakini ziko kwenye MP3 collection yangu.
 

Attachments

Niliusikia Radio Free Africa (The sound of Africa) Miaka ile ikiwa bado radio kweli kweli
 
Los del Río ni bendi kutokea Uhispania pembeni kidogo mwa jiji la Seville. Mwaka 1992 walitunga na kutoa wimbo huu wa Macarena kwa siku moja tu wakati wakiwa kwenye tour huko Venezuala. Wimbo huo ulipanda chati sana na mwaka 1995 hadi 1997 ulikuwa haukosekani kweny kumbi za muziki. Remix zake nyingi sana zaid ya 10 zimeshatolewa hadi leo wakati naandika hapa. Wewe uliusikia kwa mara ya kwanza ukiwa wapi? Na je uliupenda?


View: https://www.youtube.com/watch?v=n32mZd5SSlg&list=RDn32mZd5SSlg
 
Mwishoni mwa mwaka 1994 kuna wimbo huu uliojulikama kama "Rhythm of the Night" uliotolewa na bendi ya kiitalianao ikijulikana kama Corona. Wakati huo kwa Tanzania nyimbo za kiingereza zilikuwa siyo maarufu sana kwani ndipo wakati nyimbo za kikongo za akina Koffi Olomide, Papa Wemba, Wenge Muzika na nyinginezo zilikuwa zimepanda chati sana. Hata hivyo wimbo huu wa Rhythm of the Night bado ilikisikika sana redioni na kujipatia umaarufu wenge wakidhani kuwa ni mojawapo ya bendi za Kimarekani bila kujua kuwa ulitokea Itally. Mwimbaji alnaeopnekana kwenye video ni mbrazili aitwaye Olga Souza, na wala hakuwa mwimbaji halisi wa wimbo wenyewe, kwani mwimbaji halisi alikuwa ni Giovanna Bersola au Jenny B; huyu Olga alikuwa ana lip syinc tu. Sijui kwa nini lip syncing ilikuwa ni maarfu sana hasa kwenye bendi za kiitaliano na kijerumani, kwani hata nyimbo nyingi za Black box ambayo nayo ilikuwa bendi ya kiitaliano, video zake zote zilikuwa hazihusishi waimbaji halisi, bali Lip syncers tupu


View: https://www.youtube.com/watch?v=OnT58cIJSpw
 
Kati ya mwaka 1996 na 1997, kuna mwanadada fulani kutokea Atlanta akijulikana kama Toni Braxton alitoa wimbo huu uliojuliakana kama "unbreak my heart". Neno "unbreak" siyo la kiingereza, yaani alijitungia mwenyewe. Wakati huo Toni alikuwa angali dogodogo na mrembo sana, na hivyo kufanya wimbo wake huo kuvuma sana. Kwa bahati mbaya miaka michache baadaye aligundua kuwa alitapeliwa mauzo yote ya wimbo huo na kutangaza kufilisika.


View: https://www.youtube.com/watch?v=O596XpES1rI
 
Sophia George: Girlie Girlie

Wakati huo Sophia alikuwa bado mdogo na anaonekana alikuwa na kiuno kigumu sana. Alikuwa anahangaika kukata kiuno chake kuchochea wimbo ingawa sauti yake ilikuwa nzuri sana.


View: https://www.youtube.com/watch?v=Aql5ywVRMyk

Korogwe Tanga mwaka 1989 mkuu wa WILAYA akiwa magret ndaga tulikuwa tunauimba we mama sigaligeleee au we mama sukari teleeee ha ha ha
 
Kati ya mwaka 1996 na 1997, kuna mwanadada fulani kutokea Atlanta akijulikana kama Toni Braxton alitoa wimbo huu uliojuliakana kama "unbreak my heart". Neno "unbreak" siyo la kiingereza, yaani alijitungia mwenyewe. Wakati huo Toni alikuwa angali dogodogo na mrembo sana, na hivyo kufanya wimbo wake huo kuvuma sana. Kwa bahati mbaya miaka michache baadaye aligundua kuwa alitapeliwa mauzo yote ya wimbo huo na kutangaza kufilisika.


View: https://www.youtube.com/watch?v=O596XpES1rI

Rekebisha hapo she went on to produce massive hits kama he wasn't man enough, another sad song
 
Kool and the Gang - 1981-LP ilikuwa nyumbani na kina Boney M, ABBA, Michael Jackson
Lets go dancing oh la lala, tunaimba mpaka saa hizi hujalala
All Night Long - Lionel Richie tulicheza sana disco sunday boogie
Tam bo li de say de moi ya
Hey Jambo Jumbo
Way to parti o we goin'
Oh, jambali
Tam bo li de say de moi ya
Yeah, Jambo, jumbo
Tuliimba Jambo nipe senti moja, Krismas twende sote

We are the world - 1984, nyimbo yangu ya kwanza kuijua kuimba yote. Niliona lyrics kwenye gazeti za Afrika Events ulipotoka nikacopy kwenye daftari nikiwa darasa la sita


Dont Stop till we get enough ya Michael Jackson-1979
Cheza cheza kwa step usimkanyage mwenzio na ile nyingine kishtobe nipake mafuta

Another Sad Song ndio hit iliyomtoa kabla ya Unbreak My Heart
uko sahihi nili sahau kuweka kama another sad song, ilikuwa reference.
 
Mwaka 1971, Marijani Shaban Marijani akiwa mwanafunzi wa sekondari Tambaza alijiunga na kikukndi cha kupiga muziki pale Ushirika Club ambapo baadaye palikuwa panajulikana kama Magott. Kati ya wimbo uliompa umaarufu sana ni huu wa Georgina ingawa inasemekana kuwa haukuwa utunzi wake original. Je ulikuwa unaufahamu wimbo huo na uliusikia mara ya kwanza wapi? Kikundi hicho kilikuwa kinaitwa Safari Trippers.


View: https://www.youtube.com/watch?v=LiB6M3UL4Zw&list=RDLiB6M3UL4Zw&start_radio=1
 
Pale Kishansa Congo DRC (wakati huo ikiitwa Zaire) kundi la muziki la TP OK Jazz lilikuwa na wanamuziki nyota wengi sana wakiongozwa na "Maitre Franco." Mmoja wa hao nyota alikuwa Lutumba Simaro Massiya ambaye alikuwa ni mtunzi na mwimbaji mzuri sana akijulikana zaidi kwa jina la Poete Simaro. Kama mastaa wengi walivyo, Massiya alikuwa na marafiki wengi sana, na mmoja wao alikuwa ni binti mmoja mrembo sana aliyekuwa akijulikana kwa jina la Bowule ambaye alikuwa biashara za urembo nyingi sana zilozofanikiwa sana hapo Kinshansa. Kwa bahati mbaya mwaka 1986 Bowula alifariki baada ya kuugua muda mrefu kidogo (inawezekana kwa Ukimwi kwani wakati huo ndipo ulikuwa umeingia na watu walikuwa hawajaufahamu);, ndipo Lutumba Simaro Massiya akamutungia wimbo huu wa kumuaga ambao uliimbwa na Malage Lugendo na kutolewa na TP OK Jazz. Wimbo huo uliojulikana kama Testamanet ya Bowule na ulilpata umaarufu sana kwenye anga za muziki Afrika ya Mashariki na ya kati. Ulikuwa wimbo mrefu sana uliokuwa na urefu wa takriban dakika 15. Huu ulioko Youtube umakatwa na hauna mashairi yote original.


View: https://www.youtube.com/watch?v=p8CJRZvREpY&list=RDp8CJRZvREpY&start_radio=1

Nimepata mashairi yake yaliyotasfsiriwa kwa kiingereza ila kwa vile ni wimbo mrefu sana, nami nikayatasiri yale ya kwanza kwa kiswahili kama ifuatavyo


Maneo haya yanaongewa na Franco kabla mashairi hayajaanza

Oh Nzambé (Eh Mungu)
Osala bomowi bwa moto (Ulitengeza uhai)
Moto akoya ko kutana na malade (binadamu wanakuwa wagonja)
Mondelé pe asali kisi po moto abika (Watu weupe wanatengeza madawa ya kuponya biandamu)
Vraiment soki ezalaki po na mbongo ndé Bowulé a kufi té (Kweli kama ilikuwa ni kwa ajili ya pesa, Bowule hakutakiwa kufa)
Po famille asali nioso (Kwa vile ndugu zake walifanya kila linalowezekana)
Nzambé , pona nini liwa? (Mungu, kwa nini kifo?)
Ah somo, na ndimaki té, hum (Ah, inatisha, sikuaminie, mhu)


Mashairi yanaanzia hapa

Testament.. ba ndeko na kotanga na ko zongela eh (Ushuhuda, ndugu, ninausoma na kuusoma tena)
Maloba ya Bowulé baninga na kotanga nako lela eh (Wosia ambao Bowule aliandika, marafiki ninausoma nikilia)
Nazangi na mokili oh ba famille bosali nga mabé (Nilipotea, ndugu zangu mmenikosa)
Massiya na sala fielé wapi oh mokili esilisi nga lolendo lelo na ndimi (Massiya nitaonyesha nini; mimi ndiye wa kuchekwa)


Testatement.. ba ndeko na kotanga na ko zongela eh (Ushuhuda, ndugu, ninausoma na kuusoma tena)
Maloba ya Bowulé baninga na kotanga nako lela eh (Wosia ambao Bowule aliandika, marafiki ninausoma nikilia)
Nazangi na mokili oh binemi bo liesi nga poison(Nilipotea, wapinzani wangu mlipipa sumu)
Luambo na sala fielé wapi oh mokili esilisi nga lolendo lelo na ndimi(Luambo nitaonyesha nini; mimi ndiye wa kuchekwa)


...mashairi yanaendelea
 
Rekebisha hapo she went on to produce massive hits kama he wasn't man enough, another sad song
Siksema kuwa huo ndio ulikuwa wimbo wake wa mwisho ila ndio uliokuwa maarafu sana katika nyimbo zake zote ambao ndio ulimtambulisha kwa anga za muziki na kumwingizia pesa nyingi sana.
 
Back
Top Bottom