Ulishawahi jiuliza ni kwanini wakristo waliokoka wengi wana hali ngumu za kiuchumi japokua biblia imewahidi baraka nyingi sana

Gibbethon bible code

JF-Expert Member
Oct 9, 2023
441
677
Kama kinavyosema kichwa cha habari hili ni swali ambalo watu wengi wamekua wakijiuliza kwanini walokole wengi sio wote hali zao za kipato sio nzuri japokua kwenye biblia wameahidiwa baraka nyingi sana na Mungu na huku watu wanaoishi maisha yasiyompendeza Mungu wanamaisha mazuri na familia zao zinaishi vizuri

Unatakiwa uwe jasiri ili urithi ahadi za Mungu
Walokole wengi sana wanataka Mungu awaletee baraka mezani kwenye sahani huku kiuhalisia unatakiwa upiganie kisawa-sawa, baraka yeyote ile Mungu anayotaka kukupa inakipimo cha ujasiri ndani yake hutaipata kirahis rahisi lazima uwe jasiri ili uipate

Mungu hajibu maombi kama unavyotaka wewe
Wengi tunamuomba Mungu mahitaji mengi ukweli ni kwamba alishajibu kitambo ila sisi tunafeli sababu tunataka atujibu tunavyotaka ndo hapo tunafeli mfano unamuomba Mungu kuhusu ajira baada ya mda inatokea kazi ila mshahara ni laki 2 wengi wetu tunakataa ila Mungu anakua ameshakujibu tayari we unaona laki 2 ila Mungu anaona mamilioni na kutokujua hili wengi wetu tunafeli sana

Mungu anataka ufanikiwe kati-kati ya vurugu, kupingwa na kuchukiwa
Wengi wetu tunataka kufanikiwa kwenye comfort zote hiyo ndo changamoto kubwa inayotusumbua
Jambo la wewe kujua baraka ya Mungu kuja inaambatana na vurugu nyingi na magumu mfano Mungu anaweza kupa uongozi kwenye ngazi yeyote ile ila kuwa na uhakika utaibuka upinzani mkali ambao hukuutegemea kosa la wengi wetu tuna-quit ndo tunapokosea

Baraka yeyote ya ki-Mungu lazima iambatane na uchungu mkali sana mwanzoni
Mungu alimwambia eva utazaa kwa uchungu na akamwambia adamu utakula kwa uchungu; ukiangalia keyword hapo ni uchungu
Baraka yeyote kwa asilimia 99 lazima itaambatana kwa uchungu mwanzoni ndo uipate ni baraka chache sana zinaambatana na furaha mwanzoni

Unapokutana na changamoto yeyote usikimbilie kuitoa bali muombe Mungu iwe irrelevant (tafuta namna ya kuishi nayo) na baada ya hapa muombe tena Mungu akuonyeshe utajiri, heshima na utukufu wa Mungu uliopo ndani ya hiyo changamoto

Kosa kubwa sana wanalofanya watu ni kutumia nguvu kubwa kuondoa changamoto zinazowakabili jambo la wewe kufahamu changamoto yeyote ndani yake kuna utajiri, heshima na tukufu wa Mungu
Sasa unapokimbilia kuiondoa changamoto inayokukubali unapoteza hivyo vitu vitatu utajiri, heshima, na utukufu kwa Mungu

Ndo maana unaweza omba Mungu hitaji flani akakuletea changamoto au tatizo kumbe pasipokujua ndani ya hilo tatizo au changamoto kuna utajiri, heshima, na utukufu kwa Mungu
Na changamoto unayoiweza kuihimili hio sio changamoto

Kwako ni changamoto mpaka pale wewe binafsi imekushinda hio ndo changamoto ninayoongolea
 
Mfano nikiwa na changamoto ya Hofu inamaana hcho kinachonipa hofu nikikikabili ndipo kwenye ustawi wangu si ndio?
Unapokutana na changamoto yeyote usikimbilie kuitoa bali Muombe Mungu iwe irrelevant na akuonyeshe utajiri, heshima na utukufu wa Mungu uliopo ndani ya hiyo changamoto
Kosa kubwa sana wanalofanya watu ni kutumia nguvu kubwa kuondoa changamoto zinazowakabili jambo la wewe kufahamu changamoto yeyote ndani yake kuna utajiri, heshima na tukufu wa Mungu
Sasa unapokimbilia kuiondoa changamoto inayokukubali unapoteza hivyo vitu vitatu utajiri, heshima, na utukufu kwa Mungu
Ndo maana unaweza omba Mungu hitaji flani akakuletea changamoto au tatizo kumbe pasipokujua ndani ya hilo tatizo au changamoto kuna utajiri, heshima, na utukufu kwa Mungu
 
Je, hii ni hoja binafsi au ni msimamo wa biblia? Wanaofanikiwa wameweza kuzishika kanuni za kiuchumi
*Wanazalisha /kuuza /kuongeza thamani hivyo kupata kipato
*Wanadhibiti matumizi ipasavyo hivyo, wanakuwa na ziada (surplus)
*Ukifanikiwa hapo utaweza kuona tofauti

Mungu kaumba wote, Rostam Aziz, Harmorapa, Aziz Ki, msukuma mkokoteni, Abood,Mo Dewji, kila mmoja kwa mfano wake na sura yake

UJINGA ni kufikiri kuwa utapata utajiri, kwa sababu tu "umeokoka ".UTAPATA UTAJIRI KWA KUFANYA KAZI KWA JUHUDI NA MAARIFA, na Mungu ATABARIKI KAZI YA MIKONO YAKO
 
Kwani ni wapi nimesema ukiokoka tu ndo unapata utajiri ujinga ni mzigo
 
Back
Top Bottom