Tuhuma za Waafrika hasa wenye hali ya chini kuwa wavivu ni dhana potofu

Masikio Masikio

JF-Expert Member
Apr 12, 2023
1,840
3,375
Kumekua na hii dhana kwa mda mrefu sana kwamba waafrika ni wavivu ni uongo kwa sababu zifuatazo;
  • Waafrika wengi wamekatishwa sana tamaa mfano mzuri kuna wazee wengi sana wamestaafu wako katika majuto makuu wamefanya kazi kwa uamunifu mkubwa sana lakini wanastaafu hawana kitu wanajuta wengi wanaishia kusema ninge ninge.
  • Kuna miaka fulani ya nyuma nilifanya kazi kwenye kiwanda flani sitakitaja jina wale vibarua walikuwa wanapewa laki na nusu kuna watu wamefanya kazi kwa miaka hadi nane mshahara ni ule ule piga picha mtu kama huyu utamwambia tena afanye kazi kwa bidii ndo apate mafanikio hawezi kukuelewa lazima aamue kutafuta short-cut.
  • Nenda kariakoo kuna wale matajiri wana magodown na store nyingine zipo kariakoo na sehemu tofauti wale vibarua wa kuchukua mizigo store na store nyingine zilizopo gorofa ya tano nyingine mpaka ya tisa na nyingi hazina lift mtu anashusha kila siku mizigo alafu mwisho wa mwezi anapewa hadi laki mtu kama huyu baadae akichukia kazi na kuwa mvivu huwezi mlaumu sababu alisha-apply rule ya kufanya kazi kwa bidii na akafeli.
  • Kuna mtu namjua ni tajiri aliniambia miaka ya nyuma alikuwa anafanya magendo ambayo kwa usiku mmoja alikua anauwezo wa kuingiza hadi million 70 na alikua anauwezo wa kufanya kazi bila kuchoka au kusikia njaa sababu alikua anaingiza mamilion ya fedha; kazi yeyote yenye maslai lazima utaifanya kwa moyo.
KUFANYA KAZI KWA BIDII SIO TIKETI YA WEWE KUWA NA MAISHA MAZURI AU TAJIRI. Ili uwe na maisha mazuri na tajiri unahitaji mambo yafuatayo na sio tu kufanya kazi kwa bidii-kumbuka sehemu yeyote yenye fedha automatic utafanya kazi kwa bidii na moyo wote.
  • Connection
Bila connection ni ngumu sana kufanikiwa, nimesema ni ngumu ila inawezekana kwa mbinde sana kama huna connection, unapokua huna connection changamoto kubwa ni watu hawakuamini Mfano kwanini wahindi na warabu ni matajiri wakubwa wale wana-connection kabla hata nchi haijapata uhuru hawako pale kwa bahati mbaya na mtu wa kawaida kamwe hio connection hawawezi kukupa ina-pass kwa watoto, wajukuu mpaka vitukuu.
  • Bahati/luck
Kama huna bahati utatumia nguvu kubwa sana kufanikiwa hata kama una-qualification zote na unafanya kazi kwa bidiii, kuna watu hawana bahati yaani jambo lolote hata la kawaida wakitaka kufanya lazima watumie nguvu kubwa sana lakin wengine hawatumii nguvu.
  • Monopoly ya baadhi ya bidhaa
Kuna watu wamepewa monopoly kwenye baadhi ya bidhaa na owner ambao wanaishi abroad hii imewapelekea kuvuna utajiri mkubwa sana sababu wamehakikishiwa soko tayari
  • Fluke
Matajiri wengi na watu waliofanikiwa walipitia kipindi cha fluke ndio maana wapo hapo walipo hawawezi kukuambia bali ndo iko hivyo. Wengi wa watu waliofanikiwa kwa kigezo cha self made bila kusaidiwa na mtu wengi wao wamepitia hiki kipindi cha fluke kwenye maisha yao
  • Biashara haramu
Matajiri wengi sana wamefanikiwa kwa kufanya biashara haramu, wengi wao biashara haramu ndo mitaji ambayo wanatumia kufanya biashara halali.

Mfano kuna kada kindakindaki wa ccm anamiliki viwanda vya pombe feki na vipa fedha sana ila ukimuona kwenye media ni kuwasakama vijana ni wa vivu.

HITIMISHO

Usio watu wa hali ya chini ukasema ni wavivu wengi wao sio wote wameshakata tamaa na maisha sababu walishawahi kufanya kazi kwa bidii sana na hakuna cha maana walichopata.

Watoto wengine wamekua wakiona wazazi wao wanafanya kazi kwa bidii alafu hakuna output yeyote mtoto kama huyu huwezi mwambia utafanikiwa kwa kufanya kazi kwa bidii ni ngumu kukuelewa.
 

Mhubiri 9:11​

Nikarudi, na kuona chini ya jua, ya kwamba si wenye mbio washindao katika michezo, wala si walio hodari washindao vitani, wala si wenye hekima wapatao chakula, wala si watu wa ufahamu wapatao mali, wala wenye ustadi wapatao upendeleo; lakini wakati na bahati huwapata wote.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom