Sababu ya umaskini na ufukara ni nini?

bongo dili

JF-Expert Member
Feb 13, 2015
12,371
24,591
Namna ambavyo kanisa linapaswa kuwajibu waumini ambao ni maskini na wanaoteseka kwa magumu wanayopitia.

Ninachotaka kushughulikia katika makala hii ni mafundisho ya uongo yanayoenezwa na wale wanaofikiri kuwa eti wanazijua SABABU ZA UMASIKINI uliopo kati ya waumini – kati ya ndugu zao katika Kristo! Mafundisho hayo ya uongo hayamsaidii yeyote na isipokuwa ni watumishi vifungoni na katika kuhukumiwa. Sitaongea juu ya wenye dhambi, wala juu ya wavivu, wala juu ya wale wanaodanganywa wadhani kuwekewa mikono na mchungaji ndipo watakuwa matajiri, wala sitaongea juu ya wale wanaopatwa na uchoyo kwa kuambiwa ‘panda mbegu utapata dabo dabo’!

Siongei juu ya fikra au kauli zako kuhusu UMASKINI, bali kuhusu UHUSIANO WETU na ndugu zetu maskini kweli kweli. Katika makala hiyo ninaongelea tu kuhusu wale masikini waliopo KATI YA WAUMINI, NA WAJIBU WETU kama wakristo kwa jambo hilo yanapaswa yaweje kwa shida hii inayowapata NDUGU ZETU KWA MUJIBU WA NENO LA MUNGU. Siendi kugusia sababu nyingi zilizopo kuhusu kwa nini umasikini unaendelea kuwepo katika jamii kwa ujumla wake. Pia kile kilichoandikwa hapa kwa namna yoyote ile hakitafuti kufariji au kuhalalisha waumini wawe wavivu au waache kuzitumia fursa au hatua ili kuboresha mazingira yao ili kuwawezesha kupata kazi. Biblia inaliweka jambo hili wazi kabisa, “…tulipokuwapo kwenu tuliwaagiza neno hili, kwamba ikiwa mtu hataki kufanya kazi, basi, asile chakula. Maana twasikia kwamba wako watu kwenu waendao bila utaratibu, hawana shughuli zao wenyewe, lakini wanajishughulisha na mambo ya wengine. Basi twawaagiza hao, na kuwaonya katika Bwana Yesu Kristo, watende kazi kwa utulivu na kula chakula chao wenyewe.” (2 Wathes.3:10-12), na tena, “Mwibaji asiibe tena; bali afadhali afanye juhudi, akitenda kazi iliyo nzuri kwa mikono yake mwenyewe, APATE KUWA NA KITU CHA KUMGAWIA MHITAJI.” (Waefeso 4:28). Katika ule mstari wa mwisho, ebu tugundue pia sababu kuu ambayo kufanya kazi sio tu kukusaidia wewe katika mahitaji ya nyumbani mwako pekee (“Lakini mtu ye yote asiyewatunza walio wake, yaani, wale wa nyumbani mwake hasa, ameikana Imani, tena ni mbaya kuliko mtu asiyeamini.” 1 Tim.5:8), bali ili kukuwezesha wewe upate pesa ili UKUTANE NA MAHITAJI YA WAUMINI WENGINE. Kwa hiyo neno la Mungu liko wazi kabisa na ni imara katika jambo hili.

Hata hivyo, hii sio sura yote ya jambo hili! Mistari ya hapo juu inakisia kwamba sababu inayowafanya waumini asiwe wanafanya kazi ni kwa sababu tu ni wavivu wa kufanya kazi ,au hawazichukui fursa. Lakini sawasawa na neno la Mungu, kuna mazingira mengineyo ambapo waumini HAIWAPASI KULAUMIWA kwa ufukara wao, na tutaliangalia jambo hili kwa umakini na ukaribu zaidi.

Kwa miaka ishirini nimekuwa ninatembelea makanisa mengi vijijini. Nimeona shida na matatizo ya wakristo. Hata hivyo wengi wanaishi wakimsifa na kumshukuru Mungu mioyoni mwao! Huo ndio ushuhuda wa ajabu mbele ya watu, mbele ya mapepo na hata mbele ya malaika! Ingawa watu hao wanayo shida na upungufu wa mambo, lakini wao wanaendelea kumtumikia Bwana Yesu katika maisha yao kwa furaha! Kwa hiyo neno la Mungu linatangaza:

“Ndugu zangu, sikilizeni: Je, Mungu hakuwachagua wale walio maskini machoni pa ulimwengu kuwa matajiri katika imani na kuurithi Ufalme aliowaahidi wale wampendao?” (Yak.2:5).

Katika nyakati za leo kuna mafundisho mengi ya uongo yawahusuyo watu maskini. Mtume Paulo alisema kulikuwa na wengi waliolipotosha neno la Mungu, na ni vivyo hivyo siku hizi. Hebu turidhie kuwa Biblia ndyio neno la Mungu na kwamba tunapaswa kuongozwa na kile ambacho Mungu anavyoelekeza, na wala tusifuate kile ambacho mwanadamu anakianzisha wale namna anavyopindisha.

Tunawezaje kuyazua mafundisho haya ya uwongo? Ni rahisi. Kama mmoja anafundisha wazo fulani, jiulize mwenyewe, je wazo hilo lipo popote katika Biblia? Je, linafundishwa wapi katika Biblia namna ile ile huyo muhubiri anawakilisha kwako?

Kwa mfano, nilikuwa naongea na kiongozi wa kanisa kubwa katika mji mkubwa nchini Tanzania kuhusu wakristo masikini walioko huko vijijini, na mara moja akaniambia, “Wanayo Injili, sasa kwa nini wawe masikini!” Maneno yake yalionekana kwangu kama ni mtu anayewalalamikia wakristo hao wanaobaki kuwa ni masikini hali wanayo Injili huko vijijini. Kwa hakika sikuamini masikio yangu. Kiongozi huyo alikuwa ni mtu msomi mzuri, kwa hiyo nilishangaa alivyoweza kusema maneno hayo akijua Biblia!

Sasa ningependa tutumie kanuni nyepesi ili kuzuia kasoro katika mfano nilioutoa hapo juu. Ujiulize, ni mahali gani ambapo mitume wanawaambia wale waumini masikini kwamba wanapaswa kuamini Injili kwa umakini tu na kisha umasikini wao utawaishia? Je, mitume wanafundisha wapi mafundisho ya aina hii? Hakuna mahala popote pale! Kwa MATENDO YAO na kwa MAFUNDISHO YAO wanafunua wazi kuwa fundisho la hapo juu ni la uwongo kamili. Katika Matendo ile sura ya 2 Roho Mtakatifu alipomwagwa, waumini waliuza mali zao na wazigawanya mali hizo kulingana na HITAJI LA KILA MMOJA (Mtd 2:45,4:35). Paulo anawaagiza Wakorinto kutenga pesa siku za jumapili KWA AJILI YA WAUMINI MASKINI waishio Yerusalem ili kwamba wampe atakapokuja huko bila kuanza kukusanya pesa hizo atakapokuwepo (1Wakorintho 16:1-3). Kukusanya pesa kwa ajili ya kuwapa waumini waliokuwa wakiishi maisha ya dhiki au wale walio kuwa ni masikini lilikuwa ni JAMBO LA KAWAIDA katika nyakati za Agano Jipa. Katika Rumi 15:26, tunasoma kuwa Wakristo kutoka huko Mekodonia walituma pesa kwa watakatifu maskini waishio Yerusalem. Nabii Agabus alipoambiwa kuwa kutakuwa na njaa kubwa, waumini waishio huko Antiokia walifanya makusanyo ya fedha hizo za msaada na wakatuma kwa hao watakatifu waishio Judea. (Mtd. 11:27-30.)

Inapotokea mvua au ukama ukaharibu mazao katika mikoa ya huko Tanzania, je yale makanisa yaliyokwisha kufanikiwa zaidi katika miji mikubwa hukusanya matoleo au fedha ili kuwasaidia ndugu zao kaka na dada za masikini, wakulima kule vijijini? Au basi watakuwa wanasahauliwa! Kanisa la nyakati zile pia liliwasaidia waumini ambao hawakuweza kujisaidia wenyewe kutokana na hali yao ya kimaisha – kwa mfano yatima na wajane. Tunasoma katika Matendo 6 kwamba lilikuwa ni jambo la kawaida kanisa liwasaidie wajane waishio kati yao. Na jambo hili liliendelea kufanyika nyakati zote za Agano Jipya kama tunavyoweza kuona katika 1Tim 5:3-4 na Yakobo 1:27.

Hata hivyo, hii haikuwa tu kwamba ni TENDO LA KAWAIDA kwa waumini wa Agano Jipya ila lilikuwa pia ni FUNDISHO la mitume ya kwamba TUWAKUMBUKE NDUGU ZETU WANAUME NA WANAWAKE WALIO MASIKINI na wale waliopo katika hali ya hatari, hivyo wakawahudumia kwa msaada wa kifedha. Mtume Petro alipokuwa anajadiliana kuhusu fundisho la Injili na mtume Paulo, Petro alimwambia kuwa AWAKUMBUKE MASIKINI, na Paulo mara moja alionyesha wazi kuwa hiyo ndiyo ilikuwa ni desturi yake (Gal. 2:10). Hivyo tunayaona mahusia yake katika Warumi 12:13, “Kwa mahitaji ya watakatifu mkifuata ukarimu”, na kwa Wakorinto anasema kuhusiana na kutoa msaada wa fedha kwa waumini waliokuwa wakiteseka kwa ugumu wa maisha, “Lakini kama mlivyo na wingi wa mambo yote; imani, na usemi, na elimu, na bidii yote, na upendo wenu kwetu sisi; basi vivyo HIVYO MPATE WINGI WA NEEMA HII pia.” (2 Wakor.8:7).

Hali ya hapo juu inaelezea juu ya waumini masikini. Kwa hiyo mitume wanapowahamasisha waumini kwamba iwapo wataamini na kuitumia Injili ipasavyo katika maisha yao kwamba kwa tendo la aina hii, basi umasikini wao utafikia mwisho? Ni eneo gani anaposhauri jambo hilo kuwa ni ondoleo la umasikini wao? Ni wapi ambapo Paulo au Petro au Yakobo au Yohana wanasema, “Ndugu, mnayo Injili! Kwa hiyo shida ni nini? Amini Injili kama inapasavyo tu, na umaskini wenu utaishia!” Wazo hili, fundisho hili halipatikani popote! Je, unaweza kuupata mstari mmoja wapo katika vitabu vya mitume unaosema na kufundisha hivyo? Haupo. Na hii ndiyo sababu inayokuwezesha wewe KUPINGA FUNDISHO LA AINA HIYO!

Siamini kama hili ndilo lilikuwa kusudi la mitume kuwafanya waumini wabakie katika umasikini. Hapana kabisa, halikuwa kusudi la mitume, na wala chochote kilichoandikwa katika makala hii hakiungi mkono na wazo hilo wala kusudi hilo. Lakini kile tunachokiona kwa uwazi hapa ni kuwaona mitume walikubali kuwa masikini ni tendo la UKWELI WA MAISHA, ambayo kwa nyakati fulani fulani inakuwa juu ya uwezo wa mtu kuidhibiti. Kwa maneno mengine, ni kwamba mazingira ya baadhi ya waumini wanajikuta katika hali ya kupambana na mambo ya lazima katika maisha. Wala mitume nao HAWAKUWASHUTUMU WAUMINI wa aina hiyo katika Agano Jipya. Hapana! Hawakufanya hivyo, BADALA YAKE waliwasihi waumini wengine WASAIDIE NDUGU ZAO wanaokuwa na mahitaji halisia. Hakuna mahala popote katika Biblia ambapo waumini maskini waliweza kushutumiwa kwa upungufu wa imani katika Agano lote la Jipya. Badala yake sikiliza ukiri huu wa Yakobo, “Ndugu zangu wapenzi, sikilizeni, Je! Mungu hakuwachagua maskini wa dunia wawe matajiri wa imani na warithi wa ufalme aliowaahidia wampendao?” (Yakobo 2:5). Watu wengine nyakati za leo WANAUPINDUA UKWELI JUU CHINI, kuhusiana na jambo hili.

Bwana wetu Yesu Kristo yeye mwenyewe alisema kwamba mnao masikini kila siku pamoja nanyi (Yoh. 12:8, na Mungu alisema vile vile kwenye Kumbuk.15:11) na wanfunzi wake WALIBEBA MFUKO ambao walichukulia FEDHA KWA AJILI YA WATU MASIKINI! Je wahubiri wa hapo juu wanaamini kwamba KILE ALICHOKIFANYA YESU alikosea? MAAGANO YOTE LA KALE NA JIPYA yanaonyesha wazi kuwa wapo ambao wanaweza kuwa ni masikini kati ya watu wa Mungu. Na katika maagano yote mawili Mungu anaunganisha watu wake kuwasaidia ndugu zao waliopo katika mahitaji hayo. Wengine wenu wanaweza kusema, “Imeandikwa kuwa ‘Utafuteni kwanza ufalme wa Mungu na haki yake, na hayo yote mtazidishiwa.’” Ndiyo hiyo ni kweli. Nawafahamu watu wengi masikini wanaoishi kwa namna hiyo, na wanapata wema wa Mungu, na njia mojawapo ambayo Mungu hutoa kwa watu wanaoteseka na kupungukiwa ni KUPITIA WEWE NA MIMI. Na ukumbuke kuwa katika Agano Jipya mitume hawakuwaambia ndugu zao kuwa ‘Tafuteni kwanza ufalme wa Mungu na kisha umaskini wenu utakwisha.’ Hapana, bali wao mara zote walikusanya pesa kwa waumini waliokuwa ni masikini, ili kuwasaidia katika maumivu yao. Hebu msikilize mtume Yohana, “Katika hili tumelifahamu pendo, kwa kuwa yeye aliutoa uhai wake kwa ajili yetu; imetupasa na sisi kuutoa uhai wetu kwa ajili ya hao ndugu. Lakini mtu akiwa na riziki ya dunia, kisha akamwona ndugu yake ni mhitaji, akamzuilia huruma zake, je! Upendo wa Mungu wakaaje ndani yake huyo?” (Yoh.3:6,17). Ni sehemu ya lazima ya pendo la Mungu kwamba tunayaweka chini maisha yetu na kuwasaidia ndugu zetu katika Kristo wanaoteseka kwa ugumu wa maisha.

Mungu alisema vile vile katika Agano la Kale, “Kama akiwapo mtu maskini pamoja nawe, NDUGUZO MMOJAWAPO, ndani ya malango yako mojawapo, katika nchi yako akupayo Bwana, Mungu wako, USIFANYE MOYO WAKO KUWA MGUMU, wala USIMFUMBIE MKONO WAKO NDUGUYO MASKINI; lakini MFUMBULIE MKONO WAKO KWA KWELI, umkopeshe kwa kweli yatoshayo haja yake katika ahitajiayo.” (Kumbuk.15:7,8). Na katika Agano la Kale tunaona ukweli ule ule juu ya maskini ambao Bwana Yesu aliutaja, yaani, “Kwa maana maskini hawatakoma katika nchi milele; ndipo ninakuamuru na kukuambia, Mfumbulie kwa kweli mkono wako nduguyo, mhitaji wako, maskini wako, katika nchi yako.” (Kumbuk.15:11). Kwa hiyo, huwezi kutumia Agano la Kale wala Agano Jipya kuwalaumu au kuwashutumu ndugu zako wakristo kwa sababu tu wao ni maskini! Mungu hakufanya hivyo (katika Agano la Kale); Bwana Yesu hakufanya hivyo, na mitume hawakufanya hivyo (katika Agano Jipya)!

Ebu sikiliza maneno ya Mungu kutoka katika kitabu cha Mithali, “Amhurumiaye maskini humkopesha Bwana; …Mwenye jicho la ukarimu atabarikiwa; Maana huwapa maskini chakula chake… Mwenye haki huyaangalia madai ya maskini; Bali mtu mbaya hana ufahamu hata ayajue. (Mithali 19:17; 22:9; 29:7).

Ikiwa tunaishi katika miji na makanisa yetu hayateseki kwa zaidi kwa jinsi hii, basi tufuate kielelezo cha Agano Jipya na tukusanye pesa kuwasaidia wajane na yatima pamoja na ndugu zetu wa vijijini ambao watakuwa wanateseka kwa ugumu wa maisha kwa sababu ukame na mvua zimeharibu mazao ya musimu. Namfahamu kiongozi wa kanisa katika jiji la Dar Es Salaam ambaye pia yeye ni mwangalizi wa makanisa mengi huko vijijini. Kwa sababu ya kujitoa kwake na huduma yake kwa ajili ya makanisa yake yote, washirika waliamua kwa kujitoa kufanya makusanyo ili kwamba aweze kununua gari kwa ajili ya huduma yake kwao. Pesa zilipomfikia, alikataa kutumia pesa zile ili kununua gari, badala yake aliaagiza kuwa pesa hizo ZIKANUNUE MABATI KWA AJILI YA MAKANISA YALIYOPO VIJIJINI, ili kwamba waweze kujenga maeneo bora ya kukutania kuabudu. Huo ndio moyo mzuri wa Mchungaji!

————-

Inanihuzunisha sana kuona kwamba siku hizi watu wanataka kutoa sababu ya umaskini lakini wanafanya hivyo kwa kutumia mawazo ya watu, yaani, ya ulimwengu, badala ya kusoma neno la Mungu na kutoa maelezo kutoka katika Biblia. Sasa tutaangalia fundisho lingine la siku hizi ambalo linatokana kabisa na fikra za wasioamini ulimwenguni, lakini wahubiri wengine wanakariri mawazo yale yale bila kujua wanalofanya – kwa sababu hawajali neno la Mungu lisemalo. Wanafuata mafundisho ya ulimwengu, yaani, ‘Nguvu ya Fikra au Mtazamo Bora’ (‘The Power of Positive Thinking’). Kwa mfano wanasema, “UMASKINI maana yake ni hali ya KUKOSA MAARIFA pamoja na kuwa na FIKRA / MTAZAMO MBOVU akilini mwako! (POVERTY simply means; Lack of knowledge and having bad attitude! The state of having negative mentality).”

Haipo rahisi namna hiyo! (It is NOT as simple at that!). Kwa kweli, kwa wakristo maskini wengi walioishi Tanzania wazo hili siyo kweli! Wanajitahidi sana wapate maendeleo au kazi nzuri. Hawana ‘mtazamo mbovu’! Kusema “kama ukipata maarifa na ukiwa na mtazamo mzuri basi ndiyo utaachana na hali ya umaskini”, hiyo nidiyo kutokutumia akili yako! Ina maana unafunga macho yako ili usione yale yaliyo wazi mbele ya macho yako! Mawazo haya hayatokani na Biblia. Yanatokana na ‘Self-help’ vitabu – ‘How to be successful’, ‘Have the right attitude’, ‘Three Steps to Success’, n.k.d! (“Namna ya kuwa na Mafanikio”, “Uwe na Mtazamo ulio Sahihi”, “Hatua Tatu za Mafanikio”). Haya ni mafundihso ya ulimwengu, ya watu wasioamini juu ya ‘mafanikio’! Na mafundisho haya kwa kiasi yameingia makanisa, lakini hayana uwezo kuwasaidia ndugu zetu maskini kweli kweli!

Wengi sio wavivu. Wengi hawayachukii maarifa! Wanayo hamu sana kushughulisha akili zao! Lakini wengi wapo maskini na hawana hata uwezo wa kuwapeleka watoto wao kwenda shule ya sekondari nzuri, au wakienda pengine walimu hawapendi kwenda madarasani kuwafundisha kwa sababu wanalalamika juu ya mapato yao! Hali ya umaskini sio kwa sababu ya kosa lao! Nilikutana na vijana wengi ambao wanayo shauku kubwa sana waendelee na elimu lakini wanashindwa kwa sababu ya kukosa pesa au kwa sababu ya kutokufundishwa vizuri kwenye shule ya sekondari. Wengine lazima wanabaki vijijini kulima au kutafuta kazi nyingine lakini siyo rahisi. Sio kosa lao! Siyo laana! Ni maisha! Kwa maskini wengi (Wakristo) hapo Tanzania hali hiyo inatokana na mazingira tu! Na tumeshaona neno la Mungu linakubaliana na ukweli huo!

Jiulize mwenyewe! Ni eneo gani katika Agano Jipya ambapo Bwana Yesu au mitume wanawaonya waumini maskini ni lazima wabadilishe mtazamo wao ili kuachana na hali ya umaskini? Ni mahali gani ambapo Bwana Yesu au mitume kuwakemea au kuwalaumu waumini maskini juu ya mtazamo mbovu? Fundisho hili halipatikani popote! (Tayari tumeshaona Biblia inatufundisha dhidi ya uvivu, na lazima tuchukue kila nafasi kupata kazi tuwezavyo. Lakini kwenye somo hili tunaongelea juu ya waumini maskini, na neno la Mungu lisemalo juu ya ndugu hao!)

Kwa kweli, ni maneno makali sana na bila huruma dhidi ya wakristo maskini walioishi kwa shida kuwaambia, “Sababu ya umaskini wako ni kwamba unadharau maarifa na unao mtazamo mbovu.” Kwa wakristo wengi hiyo siyo kweli! Kusema mambo haya juu ya wakristo maskini bila kutaja au kutoa maelezo ya neno la Mungu ni kuwatenda dhambi ndugu zetu! Ukitaka, naweza kukupeleka vijijni na unaweza kuongea na ndugu hao. Utaona, maneno yako na mafundisho yako hayatagusa hali ya umaskini wao na hayana uwezo wo wote kubadilisha maisha yao!

Neno la Mungu linatufundisha kwa wazi: “Ndugu zangu, yafaa nini ikiwa mtu atadai kuwa anayo imani lakini hana matendo? Je, imani kama hiyo yaweza kumwokoa? Ikiwa ndugu yako au dada hana mavazi wala chakula, mmoja wenu akamwambia, ‘Enenda zako kwa amani, ukaote moto na kushiba,’ pasipo kumpatia yale mahitaji ya mwili aliyopungukiwa, yafaa nini?” (Yak.2:14-16).

Mafundisho ya ‘mafanikio’ au ‘badalisha mtazamo yako tu’ ni yale yale. Kwa msingi yanasema, “Je, huna mavazi wala chakula? Jifunze kitu! Umaskini wako unatokana na mtazamo wako mbaya. Enenda zako kwa amani na badilisha mtazamo wako tu na ukaote moto na kushiba.” Haya ni mafundisho makali na bila huruma, na mafundisho haya hayana msingi katika neno la Mungu.

Biblia inafundisha dhidi ya uvivu. (2 Wathes.3:6,10-12). Hiyo ni wazi. Lakini katika Agano Jipya walikuwepo waumini maskini na katika somo hili tunaangalia mitume walilofanya na walilofundisha juu ya ndugu zao maskini. Tunaona hawakufundisha umaskini wao ulitokana na laana wala kutokana na ‘mtazamo mbaya’! Hawataji mawazo hili hata mara moja! Waliwasaidia ndugu zao maskini na wanafundisha tufanye vile vile.

Nimeongea na vijana waumini vijijini. Hawafikiri, “Wazazi wangu ni maskini, lazima niwe maskini, siwezi kufanya cho chote.” Hapana! Wengi wanatafuta njia, wanajitahidi na wanayo hamu kubwa sana kutoka katika hali ya umaskini, lakini wanapungukiwa na nafasi kufanya hivyo – hali ya mazingira na upungufu wa fursa na umaskini wa wazazi wao zinawazuia wengi. Wao wasemao vijana hawa waliopo vijijini wanabaki katika hali ya umaskini kwa sababu wanakataa kubadilisha mtazamo au fikra zao, wanaongea kama hawaishi katika Tanzania. Inawezekana watu wengine ni wavivu lakini kusema msingi wa umaskini ni mtazamo mbovu sio kweli kwa vijana wengi waliookoka.

NDIYO MTAZAMO NI MUHIMU SANA, lakini tunapaswa kupata taarifa zetu KUTOKA KATIKA BIBLIA, kwamba ni mtazamo upi tuuendeleze pia tutoe ushauri ambao unatekelezeka kwa wale waliomo katika uhitaji – sio tu kuwapatia mawazo ambayo hayagusi wala kubadili hali yao. Ndiyo, yawezekana baadhi ya waumini huko vijijini wakahitaji kutiwa moyo – lakini kutiwa moyo huko kuna hitaji kitu mbadala labda kwa msaada halisia au kwa ushauri maalum. Kutokana na nilichokiona na kukisoma, watu wale wafundishao kuwa unaweza kuuacha umasikini nyuma yako kwa kupata mtazamo halisia, kila mara ni wale waishio katika majiji na miji ambako FURSA za kuboresha maisha NI KUBWA ZAIDI na pengine familia zao zimewasaidia kufanyika kuwa bora kimaisha. Watu kama hao wanapojaribu kuwasaidia watu wengine vijijini kwa kawaida huwa hawajui kuhusiana na uhalisia wa kimaisha. Wanafikiri kuwa kwa vile walihamasishwa vya kutosha kujiboreshea maisha yao, basi wanafikiri kuwa watu wengine pia wanahitaji kuhamasishwa na kuwa na mitazamo / mwelekeo halisi ili kuboresha maisha yao! Wanashindwa kuelewa kuwa fursa walizo nazo na historia ya nyuma walikotoka ni vitu muhimu, ni tofauti kabisa na zile za wale waishio katika vijiji. Ndiyo mtazamo ni muhimu ili kufanyia matumizi mazuri ya fursa zilizopo hapo, lakini ni ULE UWEPO WA FURSA HIZO NDIYO INAYOWAKILISHA TATIZO HALISI LA MASIKINI WENGI, hapa sio kuhamasisha wala mtazamo. Tafadhali kumbuka kuwa naongelea kwa ujumla; hapa sisemi kuwa watu masikini huko jijijini hawawezi kuboresha maisha yao, hapana, sisemi hivyo, kwa vyovyote wapo wale ambao wanajitahidi kufanya hivyo. Ninachokipinga hapa ni kile kuwa unahitaji TU kuwa na mtazamo halisia ili uukwepe umasikini.

——————-

Sasa napenda kulishughulikia wazo kuwa eti wale walio masikini wametumbukia katika hali hiyo kwa sababu ya mambo fulanifulani katika ULIMWENGU WA KIROHO, na kwamba inawapasa watu hao kugundua hali zao hizo za kiroho na “kuzifunga” kabla hata hujaleta “kufunguliwa” kwao kutoka kwenye ufukara wao. Tena wengine wanakosa sana kwa kusema hali ya umaskini inatokana na dhambi za maskini wenyewe au eti hawaishi karibu na Mungu! Mawazo kama haya ni ushirikina na udanganyifu, na siyo ya kibiblia. Watu wengine huenda mbali zaidi hata kusema kuwa maeneo ya Africa yanateseka kwa ufukara kwa sababu eti ya ‘laana’ zilizotajwa katika Biblia. Hiyo siyo kweli nami nashughulikia sana na habari ya mafundisho ya uongo haya kwenye nyaraka zangu (“Vita Vya kiroho / Roho Zitawalazo Maeneo”, na “Laana”). Hapa nakwenda kushughulikia wazo la hapo juu tu.

Jambo hili linaonyeshwa kwa urahisi tu katika mistari mingi ya neno la Mungu. Hata katika Agano la Kale Mungu alieleza kuwa kutakuwepo na watu masikini halisi au wa dhati KATI YA WATU WAKE (taifa la Israel), na akawapa Israel maelekezo na namna ya KUWATUNZA NA KUWASAIDIA kwa HURUMA. Kwa mfano, “Ikiwa mmoja wa ndugu wa nchi yako amekuwa maskini naye akashindwa kujitegemeza mwenyewe katikati yako, msaidie…ili aweze kuendelea kuishi…”, na tena, “Ikiwa kuna mtu maskini miongoni mwa ndugu zenu, katika mji wo wote wa hiyo nchi ambayo BWANA wenu anawapa, MSIWE NA MOYO MGUMU wala usimfumbie mkono ndugu yako aliye masikini. Afadhali fungua mikono yako na umkopeshe kwa hiari cho chote anachohitaji.” (Walawi 19:10, 23:22, 25:35; Kumbu.15:7,8). Neno la Mungu pia lilitoa maagizo yaliyo wazi katika Agano la Kale kuwaagiza watu wake kuwafikiria masikini kwa huruma (Mith.14:21,31; 21:13). Neno la Mungu linathibitisha kuwa kwa sababu hali hubadilika kutokana na mazingira tofauti tofauti ya maisha, basi kimsingi mara zote watakuwepo watu walio masikini (Kumb.15:11; Mat. 26:11) na HAWA MASIKINI WAPOKEE KUFIKIRIWA KWA HURUMA TOKA KWA NDUGU ZAO. Mungu apewe sifa kwa neema na rehema zake na kwamba anakumbuka maskini na anachochea mioyo ya watu wake kuwahurumia ndugu zao maskini!

Tumeshaona kwamba mitume walibeba mfuko wenye pesa, ambao ulijazwa pesa zilizokusanywa kwa ajili ya watu masikini (Yoh.12:5,6). Iwapo sasa masikini walikuwa ni masikini kutokana na baadhi sababu za maroho hayo mabaya, kwa nini basi Bwana Yesu au mitume hawakugundua sababu hizo za kiroho na “wazifunge” na hivyo “kufungulia” mafanikio kwa watu hao masikini? Hapa tunaweza kuona wazi jinsi mafundisho hayo yalivyo ya kipuuzi. Bwana Yesu alifundisha kuwa tunapaswa kutoa kwa watu masikini (Matt.19:21; Lk.14:13).

Jiulize mwenyewe! Ni eneo gani katika Agano Jipya ambapo Bwana Yesu au mitume wanawaambia watu kwamba umaskini wao unatokana na ‘laana’ au na ‘ulimwengu wa kiroho’? Wapi Yesu au mitume wanasema, ‘Ninyi ni maskini kwa sababu ya dhambi zenu au kwa sababu hamishi karibu na Mungu’? Je, unaweza kuupata mstari mmojawapo katika vitabu vya mitume unaosema na kufundisha hivyo? Haupo! Kumbuka, tunaongea juu ya neno la Mungu LINALOHUSU WAUMINI MASKINI MOJA KWA MOJA. Mistari kama Yakobo 4:2 na Mtt.6:33 na maneno kwa wote. MUKTADHA NI MUHIMU SANA!

Mafundisho ya uongo nyingi ni matokeo ya watu kuunyofoa mstari mmoja au miwili kutoka katika Agano la Lale na kisha hujengea mifumo yao wenyewe wanayoitaka juu yake. Bila shaka yoyote wengine huchanganya mambo ambayo jinsi Mungu alivyoshughulikia taifa la Israel na kweli ya Agano Jipya. Wahubiri wengine wangetaka kutupelekea nyuma tuishi chini ya Agano la Kale. Wanapenda sana kunukulu Kumbukumbu 28 (juu ya ‘baraka’ na ‘laana’) kana kwamba inahusu maisha ya mkristo binafsi siku hizi katika Agano Jipya. Kwenye sehemu ile Mungu aliongea na Israel kama TAIFA LAKE, naye aliwaambia yatakalotokea kama wakimtii na yatakalotokea kama wasipomtii – kama wakimwacha Mungu kuabudu sanamu. Lakini ni wazi kwamba Bwana Yesu katika mafundisho yake hakuyatumia wala kuyakariri mawazo hayo juu ya maisha binafsi ya mtu, wala mitume hawakufanya hivyo! Wahubiri wale huchanganya kabisa uhusiano kati ya Mungu na Taifa la Israel kwa upande moja, na huruma ya Mungu kwa maskini kwelikweli wote katika Agano la Kale na Agano Jipya!

Jiulize mwenyewe, ni mstari upi katika Agano Jipya unaosema ‘Kama ukiwa katika hali ya umaskini, ina maana umelaaniwa na Mungu.’? Haupo. Na nijalie kusema kitu hapa. Wahubiri kadhaa – kupitia mafundisho na machanganyiko yao – wanakaribia wamfanye Mungu afanane na mchawi. Wanafikiri na kufundisha kama unabarikiwa na mambo ya nje, ya kimwili, ina maana unampendeza Mungu; na kama unapungukiwa na mambo ya nje, ya kimwili, ina maana humpendezi Mungu. Yeye afikiriye kwa namna hiyo, yeye ni mtu wa kimwili na siyo wa kiroho. Kwa sababu ya yale Mungu aliyoyafanya kupitia Mwanawe kwenye Kalvari kwa ajili yetu, mafundisho na mawazo yale yanakaribia ulimwengu wa uchawi au ushirikina – hayawakilishi Injili, hayawakilishi Agano Jipya; hayawakilishi Mungu! Soma Agano Jipya, soma Luka 2:13, soma 1 Wakor.4:11, soma 2 Wakor.8:2, soma Wafilipi 4:11,12, soma 1 Tim.6:6-11, soma Yakobo 2:5,15,16; soma Warumi 8:28-39! Na soma Ufunuo 2:9,10 ili uone jinsi wao wanavyokosea kabisa ambao wanasema kuwa maskini ina maana unalaaniwa au huishi karibu na Mungu! Kusema hayo juu ya wamaskini wote ni ushirikina tu, na zaidi ya hayo yanakaribia fikra za uchawi.

Kama tulivyoona, makanisa katika Agano Jipya, sio tu wao waliwatunza na kuwasaidia washirika masikini bali waliwafundisha jinsi gani wakristo watatakiwa kufanya hivyo. (Wagal. 2:10; Matendo11:29; Warumi 15:26; 1 Wakor.16:1,2; 2 Wakor. 9:1; 1 Yoh 3:17). Mistari hii ya neno la Mungu inaonyesha wazi kwamba Yesu pamoja na mitume walikubali kuwa katika maisha watakuwepo masikini na kwamba sisi kama wakristo tunapaswa kuwahurumia ndugu zetu masikini na kwamba kama hatutafanya hivyo basi “upendo wa Mungu unakaaje ndani yetu?” (1 Yoh.3:17).

Wale wanaofundisha kwamba umaskini inatokana na hali ya kutokuishi karibu na Mungu, au kwamba inatokana na upungufu wa maarifa na mtazamo mbovu, je, hawajasoma neno la Mungu lisemalo, “Ndugu zangu, sikilizeni: Je, Mungu hakuwachagua wale walio maskini machoni pa ulimwengu kuwa matajiri katika imani na kuurithi Ufalme aliowaahidi wale wampendao? Lakini ninyi mmemdharau yule aliye maskini.” (Yak.2:5,6). Bwana asifiwe kwa neno lake!

Mafundisho haya hayana huruma na ni ya kikatili. Kwa nini? Kwa sababu mafundisho haya yanawaachia watu masikini mawazo kuwa matatizo wayapatayo yanatokana na sababu za siri fulani ya kiroho lakini hayana uwezo wa kuwasaidia. Wahubiri hao hawaji kwa watu masikini na wala hawawatembelei masikini ili kuwahudumia na kisha kuwaondoa kutoka katika ufukara wao ili kuwaingiza katika mafanikio kwa kugundua ni nguvu zipi za kiroho zinazowakalia ambazo huwaweka katika hali ya ufukara na kisha wazifunge! Masikini wanaosikiliza mafundisho hayo yao huachiwa mawazo mabaya na ya kuhuzunishwa tu kwamba nguvu za kutisha za madude ya kiroho ndizo zinazowaweka katika hali ya ufukara. Wanakatisha moyo wa washirika maskini kwa mafundisho yao na waliwaacha bila kuwasaidia chochote! Fundisho hilo ni la kikatili na dhidi ya mafundisho ya Biblia!

Mafundisho ya ‘Self-help’ and ‘Success’ books (vitabu vya ‘Jisaidie’ na ‘Mafanikio’) hayana uwezo kuwasaidia wakristo maskini kweli kweli kwa sababu hayatokana na Biblia. Najua kitabu cha Mithali na hata Agano Jipya zinafundisha juu ya uvivu lakini sijaandika juu ya watu wavivu. KOSA LA MAFUNDISHO YALE HAPO JUU NI KWMABA WANATAKA KUZINGATIA WATU MASKINI WOTE KATIKA MAFUNDISHO YAO, YANADAI KUTOA ‘THE SOLUTION’ (KUTATUA) KWA UMASKINI, LAKINI YANAKOSA KABISA!

“Ikiwa mtu anavyo vitu vya ulimwengu huu na akamwona ndugu yake ni mhitaji lakini asimhurumie, upendo wa Mungu wakaaje ndani ya mtu huyo? Watoto wangu wadogo, tusipende kwa maneno au kwa ulimi bali kwa tendo na katika kweli.”

© David Stamen 2016

""""""""""""""*********"""""''"""
Sijaelewa ni nini katika hili unachopinga na unachokubali kwa habari ya sababu za umaskini na ufukara. Naamini mtu akipata maarifa atafanikiwa. Huo mstari wa Yakobo unahitaji kujua zaidi aliposema hivyo alikuwa na maana gani/katika context gani. Na kwetu sasa inaapply vipi? Mungu hapendi umaskini. Kama mtu mwenyewe atakuabliana na huo ni sawa tu, atakufa maskini

Ni wazi kabisa, Lukundo, hujaelewa somo langu hapo juu. Umeandika kama hujasoma somo lile hapo juu! Niliweka muktadha wazi kabisa. Uliandika, ‘Naamini mut akipata maarifa atafanikiwa.’ Je, hujasoma nilyoyaandika juu ya wazo hili?

Sioni ubunifu wa fikra chanya kwenye fundisho hili. Nachokiona ni huruma binafsi isiyo na suluhisho.yawezekana ni utafiti mwepesi unaomridhisha mwandishi na hauna msingi imara wa kuwa fundisho.

Mungu Akubariki Sana Mtumishi Wa Mungu; Hii Ndiyo Injili Ya Kweli Uweza Uletao Wokovu

Naamini Mungu hakusudia tuwe wote maskini na naamini umaskini sio utakatifu naamini ni mzigo wa laumu na fedheha kwa mtu..ningependa nitimize ibada iliyo kamili ya kuweza kutoa zaka na sadaka iliyo kamili.na sipend niwe sababu ya kushabikia umaskini

Sijui kama umeisoma makala. Ni wazi hujaelewa niliyoyaandiaka. Wapi niliandika Mungu alikusudia tuwe wote maskini? Hiyo ni masingizo tu. Ya pili, wapi mitume ya Bwana waliandika ‘umaskini ni mzigo wa laumu na fedheha kwa mtu…’. Je, Petro alikosa alipoandika, “Ndugu zangu wapenzi, sikilizeni, Je! Mungu hakuwachagua maskini wa dunia wawe matajiri wa imani na warithi wa ufalme aliowaahidia wampendao?”

Mmm, Ninaogopa ku-comment lakini niseme tu, sikubaliani na hoja zilizotolewa na mtoa mada kuhusu Baraka na Laana na kurejea hicho kifungu cha Yak.2:5 kwa maana ya mwandishi ni kuwa watu waliofanikiwa katika dunia hii hawataurithi ufalme isipokuwa tu maskini waliochaguliwa na kwa maana hiyo ndiyo hao wenye dhiki huko vijijijini. Kwa ufahamu wangu tu niseme kuwa watu wote tangu Adamu tuko chini ya laana kwa Adamu kutenda dhambi ya kwanza na kufukuzwa Edeni na pili Kaini alipomuua ndugu yake Abeli na sisi tukiwa ni kizazi cha Kaini hatujakwepa hiyo laana kumbuka ardhi tunayo kaa dunia hii ili laaniwa pia. Ndiyo maana ukisoma Rumi 3:23-24 ina sema watu wote wametenda dhambi na hivyo kupungukiwa na utukufu wa Mungu, wanahesabiwa haki bure kwa neema Yake kwa njia ya ukombozi ulio katika Kristo Yesu. Galatia 3.13 imeandikwa aangikwaye msalabani amelaaniwa. Tujiulize, kwanini Yesu alikubali kuangikwa msalabani na huku akijua kwa kufanya hiyo ni laana? Kwa ninavyoelewa Yesu alijua kabisa kuwa watu wa dunia hii wako chini ya laana kama Rum3.13, hivyo ili kuondoa laana ilimpasa kuigongomelea msalabani.

Kwa Kuja kwake Yesu duniani kwa ukombozi wa mwadamu haimanishi watu wote wamekombolewa katika laana hiyo hapana, Yohana 3.16-18,ukisoma vizuri utagundua wale tu waliomwamini ndio watakaokolewa na kinyume cha hivyo ni hukumu.

Pia nafikiri tusipime Baraka na Laana kwa vipimo vya utajiri wa fedha, mali, elimu (material things)pekee yake, tukasema hawa wenye maendeleo ya dunia hii wamebarikiwa na ambao hawajaendelea wamelaaniwa. Si kweli. Kumbuka Mungu anasema watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa Hosea 4:6, soma kwa umakini ,(Mungu anasema watu wangu)… ina maana watu wa Mungu kwa kosa maarifa ndiyo inayopelekea kuwa katika hali duni, maarifa ndiyo yanayoleta tofauti ya haya maendeleo tunayoyaona na si swala la laana na baraka pekee. Tuchukulie mfano wa nchi kama Uingereza kama utapima baraka kwa vigezo vya maendeleo kuwa imebarikiwa na Tanzania kwa umasikini wake kuwa imelaaniwa tutakuwa tunakosea. Kumbuka nchi zote zipo chini ya laana isipokuwa tu kwa ukombozi wa Yesu. Kama ni mfuatiliaji mzuri wa dunia hii Uingereza sehemu kubwa ya utajiri wake ilipata kwa uporaji wa wazi kabisa achilia mbali ule kwa kikoloni uliokuwa unaonekana kama halali. Utawala wa uingereza wakati fulani ulikuwa ukiwatuma raia wake na meli kwenda kupora mali kutoka nchi zingine, ukichanganya na mali zilizotoka katika makoloni yao, na za kwao wenyewe pamoja na maarifa waliyokuwanayo ndiyo matokeo ya maendeleo tunayoyaona leo, je tutasema hizo ni baraka za Mungu ama za miungu?

Kama utakuwa mtafiti mzuri ni kwa jinsi gani miji yetu hii yenye majengo makubwa ya kifahari, fedha zinazomilikiwa na watu, na mali mbalimbali ukiondoa zile za serikali, kwa asilimia ngapi zimepatikana kwa njia za halali? Kama utaupata ukweli basi utakubaliana na mimi kuwa si kila mafanikio ni baraka kutoka kwa Mungu isipokuwa ni maarifa ya mwanadamu akisaidiwa na miungu yake. Wale wa kijijini unaosema kuwa hawako katika laana ni kuwa wanaweza kuwa wamekombolewa na Yesu lakini bado wakawa wamekosa maarifa wanahitaji kusaidiwa kwa kupatiwa maarifa kutoka hapo walipo na wala haimanishi kwa kuwa katika hali yao ya umasikini ndiyo wataurithi ufalme wa Mungu kama mwandishi anavyotaka kutusadikisha ni wachawi wangapi wako huko na ni maskini je kwa kuwa ni maskini ndiyo ticket ya kuurithi ufame wa Mungu. Kabla ya Yesu kuja kuna watu walipewa Baraka kwa Neema ya Mungu Mwenyewe na walikuwa matajiri, Ibrahimu, Isaka, Yakobo, Ayubu, Daudi wote hawa walikuwa ni matajiri na bado walimpendeza Mungu. TAFUTA MAARIFA UFANIKIWE.

Ya kwanza, kwa nini hukuweka jina lako? Wakati wa Mitume walikuwepo waumini maskini. Sasa, wapi mitume wa Bwana walisema au kuandika au kufundisha kuhusu maskini hao, “Tafuta maarifa ufanikiwe.” Hamna. Toa mistari, hasa kutoka Agano Jipya, kuthibitisha wazo yako. Lakini huwezi – kwa sababu wazo hili siyo mafundisho tupatayo katika Agano Jipya juu ya ndugu maskini. Ni kama hujasoma makala hapo juu.

Nashukuru kwa mafundisho mazuri sana, ubarikiwe sana mtumishi wa Mungu, wengi wetu hatupendi kukumbushwa kufanya matendo ya huruma kabisa. na hii inaleta umasikini sana katika taifa. wengi wetu wakiwa na uwezo wanasadia ndugu zao. lakini leo umetufumbua macho. barikiwa sana

So Nashukuru Kwa Kunifundisha Kwamba Nitafute Maarifa Ujumbe Wangu Nasema Bwana Azidi Kutupa Neema?

fundisho ni zuri ,lakini kitu ninacho kiona ni kwamba ule unabi uliotolewa kuwa siku za mwisho watu watakuwa ni wenye kujipenda wenyewe,wabinafs ,wenye kupenda pesa,wasio wapenda wa kwao.Kama ulivo sema kuwa wanafunzi wa yesu walikuwa na umoja bible inasema vitu vyao walivifanya kwa ushirika.Hakika hapakupaswa kuwa na maskini lakini kwa sasa unabii umetimia tufanyaje?kuna mchungaji anadai kuwa mtu maskini halifai kanisa wala selikali wala family kwakuwa hawezi kutoa sadaka ,hatoi kodi selikalini kwahiyo hafai unasemaje kuhusu hili.?

una mchungaji anadai kuwa mtu maskini halifai kanisa wala selikali wala family kwakuwa hawezi kutoa sadaka, hatoi kodi selikalini kwahiyo hafai unasemaje kuhusu hili?”
Ni rahisi! Atoe mstari mmoja ambao unathibitisha mawazo yake. Haupo! Na wewe umesoma somo langu, basi, tayari unalijua jibu, yaani, waumini walikusanya pesa kwa ajili ya ndugu zao maskini – hawakuwalaumu eti kwa sababu hawawezi kutoa sadaka! Je, na yule mchungaji hajasoma sehemu hiyo, “Akamwona mjane mmoja maskini akitia mle senti mbili. Akasema, Hakika nawaambia, huyu mjane maskini AMETIA ZAIDI KULIKO WOTE.” Katika mambo yote, jiulize mwenyewe, ‘Napata fundisho hili wapi katika Biblia?’ Usipopata, usipokee fundisho lile au mawazo yale.
Juu ya unabii sikukuelewa kwa sababu ya kukosa kwa Kiswahili changu! Lazima ueleze zaidi kwa maneno wazi na rahisi ili nielewe.

Haleluya haleluya nimebarikiwa nanazidi kusema neno la Mungu ni upanga nani moto ulao hugawanya nafsi nakukatakata nakuiondoa mafuta yaliopo ndani yake

Mtumishi umejaribu kuelezea kwa mapana sana na ukatumia NENO LA UZIMA ambalo ndio kiongozi wetu MUNGU akubariki sana kuhusu

Jambo la kwanza YESU KRISTO alikuwa anatenda kimafumbo hakuna siku mikutano ilimwelewa mbaka hata wanafunzi wake walikuwa hawamwelewi ktk mafumbo yake mbaka mdaa wa ibada ikiisha waingiapo ktk chumba chao cha mapumziko au faragha wanaenda kumuuliza nakumuhoji ulimaanisha nini pale utufundishe ipo mifano nyingi ambayo inaonyesha kabisa hawakumuelewa nayeye akawafunulia je wewe kwakuwa unahitaji kuleta mabadiko chanya ndani ya makani umejipangaje kufundisha masomo yako ktk makanisa ili watu waifahamu ukweli?

Pili tutafanyaje tupate tumaini jipya kuhusu baraka za Mungu na wokovu kiujumla ili tugeuze fikra zetu tuondokane na elimu ya kibinadamu ili neno la UZIMA lipate nafasi ndani ya jamii zetu kiujumla??

Tatu kuna mpendwa mmoja amekuuliza hapa maswali kadhaa ukakwepa kuyajibu nami narudisha tu kwa njia moja au nyingine Biblia inatuambia tutarithi pamoja na BWANA YESU inamaana baraka zetu sinayeye na ukiangalia hawa maskini wa vijijini unaowasungumzia asilimia 98% wanavitumikia miungu kuhusu umaskini wao watu wanaenda makanisani kumuomba Mungu usiku wanakesha kwa waganga wakiwaloga wengine wakiitisha mafanikio kwanza tutofautishe baraka na mafanikio BAZAKA IPO KWA MUNGU NA MAFANIKIO IPO KATIKA DUNUA HUWEZI KUFANIKIWA HALAFU UJIITE MBARIKIWA NI VITU VIWILI TOFAUTI HUWEZI KWENDA KWA MGANGA KUTAFUTA BARAKA HALAFU UENDE KWA MUNGU KUTAFUTA MAFANIKIO NANDIO SHIDA ILIOPO SAA ZINGINE KANISA HALINA NGUZO WALA UWIMARA KWA SABABU WATU WAPO KANISA KIMWILITU NJIA ZOTE SIPO KWA MIUNGU YAO SASA HAO WAKIWA MASKINI WATAITWA MASKINI WAMUNGU AU MASKINI WA DUNIA? neno maarifa linahitajika sana napia tusitumie kauli za watu kuhubiria INJILI tutumie HAKI kama BWANA YESU hatuwezi kumsaidia MUNGU AU YESU KAZI YAKE yeye anajua mwanzo na mwisho wa kazi yake mawazo ya watu haileti uhalali ndani ya neno la MUNGU NIKWAMBA WATU WAMEJIFUNGA FIKRA NASEMA TENA WATU WAMEJIFINGA FIKRA WALIO NA YESU SIO MASKINI NANDIO MAANA NASEMA NENO MAARIFA NI LA MUHIMU SANA UNGESEMA TUONGEZE ELIMU YA NENO VIJIJINI LAKINI SIO KUHUKUMU MAWAZO YA MTU KWAKUTUMIA NENO LA MUNGIU MTUPE PAULO ANASEMA Atukuzwe Mungu Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo aliyetubariki kwa baraka zote za rohoni katika ulimwengu wa roho ndani yake Kristo (WAEFESO 1:3) BIBLIA IKO WAZI KAMA UNAYE YESU UMEBARIMIWA KWASABABU IMANI YAKO IMEKUUNISHA NA VITU VYOTE ALIVYONAVYO YESU KRISTO BABA YETU IBRAHIMU aliambiwa na MUNGU katika kubariki nitakubariki nitakubariki na katika kuzidisha nitauzidisha uzao wako kama nyota za mbinguni na kama mchanga ulioko pwani na uzao wako utamiliki mlango wa adui zao (MWANZO 22:17) MUNGU anasema katika kitabu cha (ZABURI 24:5-6) ATAPOKEA BARAKA KWA BWANA NA HAKI KWA MUNGU WA WOKOVU WAKE HIKI NDICHO KIZAZI CHA WAMTAFUTAO WAKUTAFUTAO USO WAKO EE MUNGU WA YAKOBO

Nimechanganya kidogo ili nieleweke niachosema utajiri na umaskini wa dunia hii haina nafasi kwa Mungu endapo hauna haki kwa Mungu huwezi niambia tuwaonee maskini huruma wakati hawamtafuti Mungu wanachanganya miungu na MUNGU aliye hai jumapili kanisani jumatatu mbaka ijumaa ni kwa waganga hawataki shauri la Mungu kwa hali wa sasa wimbi la watumishi limejaa na wote hawana maarifa ya ROHO wanayo ya akili ya kidunia wanajaribu kuingiza kwenye NENO la UZAMA ukweli ni kwamba maskini wa KIROHO na MASKINI wa kimwili tunashindwa kutofautisha tunapoambiwa na YESU KRISTO tuutafute kwanza UFALME WA MUNGU HAMAANISHI MAFANIKIO ANAMAANISHA ROHO YAKO KWANZA IUNGANISHWENA UUNGU WA MUNGU MAANA UTAJIRI UPO NDANI YETU PESA NI MAKATASI TUELEWE NANDIO miungu WATU LEO WANAVITUMIKIA ALIYE NAMAFANIKIO YA KIMWILI ANAITWA MBARIKIWA NAMASKINI WA KIROHO TUTAMWITAJE?? Vitu vyote tunapatiwa tuvitumie kwa furaha (1TIMOTHEO 6:17-19) haimaniishi kila tajiri ni wa Mungu aliye juu haimaanishi kila maskini ni wa Mungu aliye juu roho ya huruma siku zote hutazama hali ya nje tu haitazami ya ndani Mimi ni maskini wa dunia lakini sikazi mwendo nipate ya dinia nakaza mwendo ili nipate kulishika lile ambalo kwa ajili yake nimeshikwa na Kristo Yesu Ndugu sijidhanii nafsi yangukwamba nimekwisha kushika ila natenda neno moja tu nikiyasahau yalio nyuma nikiyachumilia yalio mbele (WAFILIPI 3:12-13) PAULO TENA ANASEMA MAANA UFALME WA MUNGU SI KULA WALA KUNYWA BALI NI HAKI NA AMANI NA FURAHA KATIKA ROHO MTAKATIFU (warumi 14:17) utofauti moja hatuelewi tusiwatazame maskini kimwili bali tuwatazame KIROHO ili tupate namna yakuwapa maarifa wapate elimu ya NURU hiyo ndio hurumanamba moja okoa nafsi yake (1WAKORINTO 5:5)

Reply
sans on June 11, 2016 at 7:56 pm
Natamani kukujibu

Reply

Nimekuwa nikisoma makala nyingi za huyu Mtumishi na nyingi zina ukweli ndani yake lakini kitu kimoja ambacho nimejifunza ni kama wale wanasiasa wa upinzani ambao mara zote wao ni kukosoa bila kutoa majibu ya nini kifanyike ili kutoka hapo ambapo watu wame kwama. Kwa maana nyingine hana mafundisho aliyoyaandaa yeye mwenyewe anasubiri tu mafundisho ya waliokosea ili aweze kukosoa kuwa hapa wamekosea sidhani kama hii tawasaidia Wakristo. Kwa mfano makala hii kwa mtizamo wake ni kuwa masikini waendelee kuwa masikini kwasababu imeandikwa masikini hatakosekana katika nchi na wale wenye uwezo wanapaswa kuwasaidia na waendelee kuwasaidi ambao ndio mtizamo wa nchi zilizoendelea kwa nchi masikini. Huwezi kumkomboa masikini kwa kumpa unga au mahindi au tumeseme mkate wa siku, hii ni sawa tu na kumfurahisha kwa dakika na baadae anabaki katika dhiki zake. Ndio maana kuna msemo usemao mtu akikuomba samaki mpe nyavu na umfundishe jinsi ya kuvua kwani ukimpa samaki kesho atakuja tena kukuomba lakini ukimpa nyavu na umkafundisha hatakuomba tena.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom