Je, unajua kwamba William Tyndale alichomwa moto na Kanisa kwa kosa la kutafsiri na kuchapisha Biblia?

mchawi wa kusini

JF-Expert Member
Apr 18, 2018
805
810
Habari Ya asubuhi Leo Ya tarehe 11/03/2024 Nawaletea Ufunuo huu WanaJF twende Na Mimi ili mpate mambo mzuri

WILLIAM TYNDALE,MTU ALIYECHOMWA MOTO NA KANISA KWA KOSA LA KUTAFASIRI NA KUCHAPISHA BIBLIA:

Mambo mengine ni magumu mno kuandika, lakini hata hivyo nitaandika!

Kila Mkristo amesoma kitabu kitakatifu cha Biblia,lakini pia naamini watu wachache sana wamesikia au kujua hili jina “William Tyndale”, na sidhani kama ni muhimu kwa watu wengi, ingawa Biblia ndiyo kitabu maarufu kuliko zote duniani. Kuna sababu kubwa ya jina hilo maarufu kulazimishwa ipotee kwenye kimbukumbu za kihistoria!

Ebu tupate maarifa kidogo, tusome kuhusu mtu huyu aliyeteswa na watu waliojiita wakristo ambao hawakutaka watu wengine wamiliki wala kusoma Biblia na kufahamu ukweli kuhusu neno la Mungu. Walijiita wakristo lakini walikuwa wapinga "Maarifa" ya Kikristo na Mungu.

Kutafasiriwa kwa Biblia kwenye lugha zetu haikuwa kazi rahisi. Kuna watu waliumia sana, waliteswa na kuuliwa kikatili walipojaribu kutafasiri Biblia kutoka kwenye lugha za Kiibrania (Agano la kale) na Kigriki (Agani jipya)-Ingawa pia kuna aya chache kwenye vitabu vya Yeremia, Ezra na Daniel ambayo yaliandikwa kwa lugha ya Kiaramu (Aramic).

William Tyndale alizaliwa kati ya mwaka 1490 na 1494, huko England (Uingereza). Ingawa kanisa limemsahau mtu huyu kabisa,na kuwatukuza watu ambao hawana mchango kama wa William, hakuweza kuishi maisha huru baada ya kupinga jitihada za kanisa kujaribu kuficha neno la Mungu.

Nia ya wenye mamlaka ilikuwa ni kuhakikisha watu wachache tu wamepata maarifa, ili sisi wengine tuangamie kwa kuikosa. Watu hao wachache walifundishwa ujuzi na namna ya kutufikishia ujumbe, ambao ulitungwa kutupumbaza na kutupoteza kabisa. Walitaka Biblia ifanywe kuwa kitabu ambacho kingetufanya sisi watumwa wa watu wachache!

Huyu mwamba alikuwa msomi si haba,alikuwa na uwezo wa kuongea na kuandika lugha takriban 7 maarufu duniani, tena kwa ufasaha mkubwa (Kiebrania, Kigriki, Kilatino, Kiitaliano, Kiispania, Kifaransa na Kiingereza).

Tyndale alikuwa padre wa kanisa katoliki. Alikuwa padre msomi sana na mtu anayejiuliza maswali mengi kichwani mwake na kuvitafutia majibu kwa namna yoyote ile. Pia alikuwa mtu mjasiri wa kuzungumza ukweli, lakini pia alikuwa mtu mpole na mnyenyekevu sana.

Yaani ningekulia kipindi hicho huko Uingereza,ningekuwa mwanafunzi mtiifu sana wa Tyndale!

Moja kati ya mambo aliyoamini ni kuwezesha watu wengi iwezekanavyo kupata nakala za Biblia kwenye lugha zao,ikianzia kwenye lugha mama ya kiingereza.

Naamini hii ndiyo ilikuwa kichocheo kwake au sababu kubwa ya kusoma na kuelewa lugha nyingi, ili atumie uwezo huo kutafasiri Biblia kwa lugha nyingi iwezekanavyo. Hii ilikuwa ni kinyume kabisa na imani ya kanisa na ufalme wa kirumi kipindi hicho.

Kwa sababu lengo kuu ya kanisa katoliki ilikuwa ni kueneza injili kwa lugha ya kiitaliano tu-Hii ikiwa inakwenda sambamba na ndoto ya kumiliki na kuitawala dunia yote chini ya lugha moja, imani moja na falme moja. Hii ilimsababishia ugomvi, chuki na uhasama mkubwa na wakuu wake wa kanisa pamoja na mfalme wa Uingereza ambaye kipindi hicho alikuwa akifanya kazi chini ya utawala wa kiroma(Roman Empire).

Tyndale alifanya maamuzi magumu ya kutafasiri vitabu vya agano jipya kwa lugha ya kiingereza kutoka kwenye lugha ya Ugiriki mnamo mwaka wa 1523,kinyume na amri ya kanisa.

Wakuu wake waliposikia anafanya hivyo, walifanya mpango wa kumuangamiza, na kutokana na presha alizopata alitoroka nchini kwao akakimbilia nchini Ujerumani mwaka 1524. Kwa bahati nzuri alipata ufadhili mkubwa wa kifedha kutoka kwa jamii ya wafanya biashara matajiri wa mjini London(Uingereza).

Alimalizia tafasiri ya kwanza ya Agani jipya mwaka 1525 na kuichapisha mjini Cologne (Ujerumani), lakini hata hivyo presha baado zilimuandama huko mjini Cologne na alilazimika tena kukimbilia mjini Worms, ambapo alifanikiwa kutoa tena matoleo (Editions) mawili mwaka huohuo wa 1525.

Nakala za mwanzoni kabisa zilisafirishwa kwa siri hadi nchini Uingereza mwaka 1526, ambako ziligundulika na zikakataliwa kabisa na utawala wa kiroma nchini humo. Biblia hizo zilipigwa marufuku kutumika popote pale nchini humo!

Hakuchoka,alipomaliza tafasiri ya Agano jipya, alianza tafasiri ya Agano la kale akianzia vitabu vitano vya Taurati (Pentateuch) vya ‘Mwanzo’, ‘Kutoka’, ‘Mambo ya Walawi’, ‘Hesabu’ na ‘Kumbukumbu la Torati’. Alitafasiri na kuchapisha nakala kadhaa ya vitabu hivi mwaka 1530, mjini Marburg.

Alifanikiwa kutoa nakala ya kila kitabu kimoja kimoja. Aliendelea na kazi ya kutafasiri Agano la kale baada ya kutorokea nchini Ubelgiji (mjini Antwerp) wakati maisha yake yalizidi kuwa hatarini huko Ujerumani. Kwa bahati mbaya, Tyndale alikamatwa mjini Antwerp kabla hajamaliza kazi yake ya kutafasiri.

Alisalitiwa na marafiki zake wa karibu,akakamatwa na kuwekwa ndani kwa miezi 18 kabla hajahukumiwa kunyongwa kwa kufungwa kwenye nguzo hadi kufa tarehe 6/10/1536. Hii ilifanyika katikati ya mji wa Vilvoorde, jirani na mji mkuu wa Brussels nchini Ubegiji.

Kama hilo halitoshi, walichoma mwili wake kwa moto huku watu wakiangalia hadi ilipogeuka kuwa majivu. Kwa nini? Alikwenda kinyume na kanisa pamoja na mamlaka za Warumi. Hii hali ilitishia watu wengi lakini haikusitisha kazi ya Mungu.

Wakati anakufa William Tyndale, kulikuwa na nakala 18,000 zilizochapishwa, lakini hadi leo kuna nakala 2 tu kwenye jumba la maktaba kuu la “British Library”. Naamini hata leo hii Biblia tunayosoma ilichezewa na ukweli fulani kuondolewa humo!Inanisikitisha sana!

KWA NINI KANISA LILIKATAZA UMILIKI WA BIBLIA?
Kulingana na William Tyndale na Martin Luther, Kanisa lilikuwa chini ya mamlaka ya serikali ya waroma, walitaka kuthibiti na kutawala imani ya watu. Hawakutaka watu wapate maarifa, elimu na uelewa wa Biblia.

Kanisa ilikataza kabisa waumini na watu wa kawaida kumiliki na kusoma Biblia. Ilikuwa kinyume na sheria na mtu yoyote aliyepatikana na Biblia aliteswa, na kunyongwa hadi kufa,kisha mwili wake kuchomwa moto.

Hii pia ndo sababu hata kuitafasiri ilikuwa ni kosa kubwa la jinai. Hii sheria kali ilianza mwaka 410 na iliendela mpaka mwaka 1600. Kwa huku kwetu Afrika, kumiliki Biblia katika kanisa Katoliki ilikuwa ngumu sana mpaka miaka ya hivi karibuni.

Kama ukifikiri hili halina ukweli angalia sheria hizi walizotunga kipindi hicho:

Amri ya baraza lililokusanyika mjini Toulouse, nchini Ufaransa, mwaka 1229: “Tunakataza pia walei kukubaliwa kumiliki vitabu vya agano la kale na agano jipya, lakini tunakataza kabisa wao kumiliki tafasiri ya vitabu hivi.”

Amri ya baraza lilikusanyika mjini Tarragona, nchini Spain, mwaka 1234: “Hakuna mtu atamiliki vitabu vya Agano la kale na Agano jipya kwenye lugha za kiromansi (Uspania, Kireno, Kifaransa, Kiitaliano au Kiromana), na endapo mtu amemilikishwa, lazima avirudishe kwa askofu wa eneo hilo ndani ya siku nane baada ya kutangazwa kwa amri hii,ili vichomwe moto.”

Hii hali iliwaacha waumini kwenye giza totoro la ujinga,ili watawaliwe kiurahisi na wanyimwe uwezo wa kupata maarifa, waangamie na wasiweze kuurithi ufalme wa Mungu.

Na mpaka leo, ni waumini wachache sana ndani ya kanisa wenye ujuzi au uwezo wa kutafasiri au kutafakari Biblia ingawa ni Wakristo, na yapo baadhi ya maparokia ambapo waumini wanakatazwa kubeba Biblia (ni rahisi sana kutawala watu wajinga).

Kutokana na hili,hadi leo hii, ni wachache sana wameweza kupata injili sahihi ya Kristo,ya Ufalme wa mbinguni. Maana Yesu aliagiza hivi: “Na mnapokwenda, hubirini mkisema, ufalme wa mbinguni umekaribia, waponyeni wagonjwa, wafufueni wafu, watakaseni wenye ukoma, wafukuzeni pepo. Mmepokea bure, toeni bure. Msichukue dhahabu, wala fedha wala sarafu za shaba katika mikanda yenu” (Mathayo 10:7-9).

Na mtume Paulo anasisitiza hivi: “Najua kwamba nikishaondoka, mbwa mwitu wakali watakuja kati yenu nao hawatakuwa na huruma yo yote juu ya kundi lenu. Na hata kati yenu ninyi patatokea watu watakaosema maneno ya kupotosha ili wawavute baadhi ya wanafunzi wawafuate” (Matendo ya Mitume 20:29-30). Ukweli ni kwamba baada ya Paulo kuondoka, kanisa ilinyakuliwa na mbwa mwitu,neno lilikanyagwa na watu kutekwa kimawazo.

Badala ya kujifunza na kujua ukweli ili wawe huru, wamejifunza uwongo na kuwa watumwa kwenye wongo. Watu wanaabudu mali, pesa na siyo Mungu aliyehai. Kwa sasa ukikosa pesa ya kutoa kanisani, umekua mpinga imani na mzigo kwa kanisa.

Wanahubiri mali na utajiri, wamekusanya watu kwenye makundi mbalimbali na kutunga sikukuu mbalimbali ili wawe bize, wasije kuwaza Mungu wao hata siku moja. Wamewamiliki na kuwafanya watumwa kwa kutumia mbinu nyingi za kijanja janja, ili wasijue wala kuona ukweli, na waendelee kuwa watumwa wa kanisa badala ya kuwa wafuasi na waumini wa Kristo. Maskini, wajane, wagane, walemavu wananyang’anywa hata kile kidogo walichopata kwa mateso, kwa kisingizio cha kutoa zaka!

Luka 11:52, “Ole wenu, ninyi wanasheria, mmechukua ufunguo wa kujifunza kuhusu Mungu. Ninyi wenyewe hamtaki kujifunza na mmewazuia wengine wasijifunze pia.”

Mathayo 23:13-24 na Marko 12:40, “Ole wenu waalimu wa sheria na Mafarisayo, wanafiki! Mnaufunga mlango wa ufalme wa mbinguni mbele ya macho ya watu. Nyinyi wenyewe hamwingii ndani, wala hamwaruhusu wanaotaka kuingia waingie. Ole wenu waalimu wa sheria na Mafarisayo, wanafiki Mnawanyonya wajane na kujisingizia kuwa watu wema kwa kusali sala ndefu.

Kwa sababu hiyo mtapata adhabu kali. Ole wenu waalimu wa sheria na Mafarisayo, wanafiki! Mnasafiri baharini na nchi kavu ili kumpata mtu mmoja afuate dini yenu. Mnapompata, mnamfanya astahili maradufu kwenda katika moto wa Jehanamu kuliko nyinyi wenyewe.

“Ole wenu viongozi vipofu! Nyinyi mwasema ati mtu akiapa kwa hekalu, kiapo hicho si kitu; lakini akiapa kwa dhahabu ya hekalu, kiapo hicho kinamshika. Enyi vipofu wapumbavu! Kipi kilicho cha maana zaidi: Dhahabu au hekalu linalofanya hiyo dhahabu kuwa takatifu?

Tena mwasema ati mtu akiapa kwa madhabahu si kitu; lakini akiapa kwa zawadi iliyowekwa juu ya madhabahu, kiapo hicho humshika. Enyi vipofu! Ni kipi kilicho cha maana zaidi: Ile zawadi, au madhabahu ambayo hufanya hiyo zawadi kuwa takatifu? Anayeapa kwa madhabahu ameapa kwa hiyo madhabahu, na kwa chochote kilichowekwa juu yake.

Na anayeapa kwa hekalu ameapa kwa hilo hekalu na pia kwa yule akaaye ndani yake. Na anayeapa kwa mbingu ameapa kwa kiti cha enzi cha Mungu, na kwa huyo aketiye juu yake. Ole wenu waalimu wa sheria na Mafarisayo, wanafiki! Mnatoza watu sehemu moja ya kumi, hata juu ya majani yenye harufu nzuri, bizari na jira, na huku mnaacha mambo muhimu ya sheria kama vile haki, huruma na imani. Haya ndio hasa mliyopaswa kuyazingatia bila kusahau yale mengine. Viongozi vipofu! Mnatoa nzi katika kinywaji, lakini mnameza ngamia!

JINA YEHOVAH-NANI ALILIANZISHA?
Jina Yehovah lilitafasiriwa kutoka kwenye jina Yahweh/YHWH na kuandikwa na mwandishi huyu huyu William Tyndale kwenye kitabu cha Kutoka 6:3, kwa lugha ya kiingereza(JEHOVAH). Leo hii tunatumia hili jina maarufu, jina kuu, jina lenye baraka na neema. Jina la Mungu wetu, lakini ni wachache sana wanajua lilitokea au kuanzia wapi.‬ ‭

Pia tutambue kwamba baada ya kutoweka kwa Tyndale, jina hilo liliondolewa sehem nyingi ndani ya Biblia na kupachikwa jina "BWANA!".

Badala ya kutumia jina "Bwana", tumia sana jina halisi la Mungu, tumia jina Yehova!

Si vibaya kufahamu, si vibaya kuwa na maarifa, naamini hatutaki kuhangamia kwa kukosa maarifa, sanasana tunapoelekea miaka ya Mbeleni Kutoka mwaka Huu tulipo 2024

Hii ni 'special dedication' kwa watu wanaotaka kujua ukweli.
 
HAPANA YESU KRISTO NDIO KANISA NA KRISTO YUPO NDANI YA WATU WALIO MPOKEA NA KUMKILI KUWA NI BWANA NA MWOKOZI WA MAISHA YAO

HAO WATU NI WAHUNI TU WALIO MCHOMA UKISEMA KANISA UNAMAANISHA KRISTO KAMCHOMA WAKATI KRISTO NI MUNGU MWENYE UPENDO MPAKA AKAUTOA UHAI WAKE

(AMRI KUU YA YESU KRISTO NI UPENDO)

MARAN ATHA - BWANA WETU ANAKUJA
 
Kanisa lina tafsiri zaidi ya moja.
Na kwa sasa kanisa lahitaji uamsho.
 
Mungu atulinde.
 
UKATOLIKI NA HISTORIA YA KANISA NA UANZISHWAJI WA UISLAMU DUNIANI KARNE YA 6 ref ufunuo 9
 
Back
Top Bottom