Ukweli kuhusu Jane Urassa - mke aliyeuawa kwa risasi 💔

Ukweli kuhusu Jane Urassa - mke aliyeuawa kwa risasi 💔

#FACT-CHECKING

Usidanganyike, mambo kwa ground yapo tofauti sana. Kwa ushahidi, tupitie ni yapi ya kweli na yapi si kweli kuhusu kifo cha Jane Maloo Urassa ⚰️ aliyeuawa na Laurence Kweka, mwanaume aliyekosa akili, busara na utashi wa kibinadamu.


View attachment 3686843

  1. Jane na Bw. Kweka waliishi kwenye ndoa kwa miaka 18 na miezi 8 na wana watoto 4 - KWELI

  2. Jane alikua mtumishi aliyeajiriwa, mwenye kipato chake binafsi, na elimu ya chuo kikuu (Masters) - KWELI

  3. Jane alimiliki mali binafsi alizotafuta kabla ya ndoa ikiwemo kiwanja kilichojengwa nyumba iliyoleta mgogoro - KWELI

  4. Jane alikua ameshaondoka hapo nyumbani kwenye migogoro kwa zaidi ya miezi miwili na kwenda kuishi kwa ndugu zake na alimuachia bwana Kweka nyumba na pamoja na watoto wote aishi nao - KWELI

  5. Mgogoro mkubwa ulijitokeza miezi kadhaa nyuma baada ya hati ya nyumba kutoka na majina ya watoto na Jane kama msimamizi mpaka pale mtoto wao wa kwanza atakapofikisha miaka 18 - KWELI

  6. Jane alitaka hati ya nyumba iwe kwa jina lake - SI KWELI

  7. Jane aliweza kutengeneza hati sababu kiwanja kilikua mali yake na bwana Kweka hakutaka majina ya watoto kwenye hati bali jina lake mwenyewe, sababu aliamini nyumba ameijenga kwa jasho lake - KWELI

  8. Jane alirudi nyumbani kwao masaa machache kabla ya kuuawa, kuwapelekea watoto wake chakula kwa sababu walikua wameishiwa na baba wa watoto alikua safarini Moshi - KWELI

    PS:
    Mtoto wao aliyempigia simu mama yake ataishi kwa uchungu maisha yake yote, akijua bila ya simu yake, mama yao angekua hai leo.

    View attachment 3686846

  9. Kabla ya mauaji, tayari kulikua na kesi polisi na ustawi wa jamii dhidi ya bwana Kweka kuhusu ukatili wa kijinsia na kumtishia mkewe maisha - KWELI

Vyanzo vya taarifa / Sources: (Ukija kubisha na wewe ulete vyanzo vyako)

Tofauti na mambo yanayoendelea mtandaoni na watu wanavyoleta mizaha kuhusu ukatili wa kijinsia na mauaji, Jane Urassa aliuawa kwa sababu alikua tayari kuachana na mume wake na kuhakikisha mali zao walizochuma pamoja zinabaki kwa watoto wao.

Alifanya vile ambavyo wanaume wanashauri humu jukwaani kwamba, using’ang’anie mali ambayo si yako, akampisha mwanaume kwenye nyumba yao, akaacha watoto bila kuwang'ang'ania na bado akauawa kikatili.


Hitimisho:

Jane alifikia mwisho kwenye maisha ya ndoa ila Mr. Kweka hakuwa tayari kuona mwisho wa ndoa yao pekee, alitaka pia kuhakikisha ni mwisho wa maisha yake pia - kusudi lake limetimia.

R.IP Jane 💔

Tupinge Femicide / mauaji ya wanawake

Alamsiki!
Rubish .kama kiwanja kilikuwa cha mwanamke kulikuwa na haja gani ya kubadilisha hati.kwa nini huyo mwanamke alikubali nyumba ijengwe kwenye kiwanja hicho?
Kwa nini hakumwambia atafute uwanja mwingine ndo ajenge.huoni huyo mama hakuwa na nia nzuri kubadilisha hati ya uwanja.kwani hati ingekuwa yao wenyewe watoto hawangeirithi.
 
Hayo mawazo yamechangia Jamii nyingi za sisi Weusi kushindwa kuvunja mnyororo wa Umasikini

Umeona "Mo", amekutana na mali za Babu yake na yupo hapo kuziendeleza. Na juzi ameanza kumwingiza kwenye biashara mwanae Abbas ili ajifunze kukuza na kuendesha mali za familia

Ni ushauri wangu, kama una mali (assets) hakikisha unaziwekea mpango wa kuendeleza na familia yako (watoto wako) ili zisaidie kuwapatia mitaji ya biashara ili wajukuu zako kwa watoto wazaliwe na kukuta hiyo chain ya biashara

Ukiwa na mentality hiyo ya kwamba watoto waje watafute zao, mbona watoto wa marehemu Mzee Mengi wanaendeleza biashara na mali za Baba yao

Tujifunze kubadirika, zaa watoto 4/3 na Mama mmoja, kisha wakuze kwa umoja na uwachumie mali ili wao wasije kutumia msuli mkubwa kujitafutia, wewe baba yao unakuwa umewaanzishia njia
Kuna tofauti kati ya kuhamisha umiliki wa majengo na viwanja kwa watoto na kushirikisha watoto kwenye biashara zako.
Angalia tofauti ya kile ulichoandika kwenye post yako ya awali hiki ulichoandika sasa.

Alichofanya Jane ambacho wewe umeridhia ni kuhamisha umiliki wa jengo na sia biashara zake.
Hicho ndicho hasa tunacho shindania.

Hata hiyo biashara huwezi kumkabidhi au kumshirikisha mwanafunzi wa miaka 16 kama walivyo watoto wa Kweka na Jane.

Ni kweli tunatakiwa hasa tuwashirikishe watoto wetu kwenye biashara zetu.
Lakini kuna tofauti kumilikisha majengo na kushirikisha watoto kwenye biashara.

Hata huyo Mzee Ghulam Dewji ameshirikisha watoto wake kwenye shughuli zake baada ya watoto hao kumaliza masomo yao.
 
huu uzi ni wa upande wa k , je upande wa me vipi, hapa kwa vyovyote vile mwanamke alitaka kumzidi speed me,
 
Mimi ni wakike lakini kuna mazingira nakuelewa kweka
Halafu kuna kitu unatakiwa ukijue, binadamu tunatofautiana namna ya Ku handle changamoto, kama hujawahi pitia changamoto yoyote ya kimahusiano huwezi elewa ila kama umepitia utamuelewa kweka then utajiombea wewe na kizazi chako ili yasikukite ya kweka Ila kama unavyosema utachukua maamuzi ya kumchinja kweka basi wewe na Kweka hamna tofauti wote nyie ni Sawa Sawa hamuwezi Ku handle changamoto

Naomba Muangalie kweka
1. Kaoa mke na ana familia for 18yrs ya Ndoa takatifu
2. Kiwanja alinunua Mwanamke ila kujenga Nyumba kajenga mwanaume (kawekeza over 350m
3. Kweka amekutwa na cancer ya utumbo, Kweka Kazi zake hazifanyi vzr kwa sasa plus maradhi mission zikasimama
4. Mke akaomba Hati mume akataka pawe na majina yote mawili mke akafanya kinyume chake (akijua kabisa mume hataki)
5. Mke akaanza Ku file talaka
Hivyo kweka asingetoka hata na tofauti kwasababu Nyumba inasomeka jina la watoto Jane akiwa msimamizi Tu
Hivyo pasingekuwa na Mali ya Ndoa

Kuna namna tuelewe kuchanganyikiwa kwa Kweka Ila tusiunge mkopo reaction
Mimi huwezi kunifananisha na huyo mpuuzi...
Nimetoa mfano , endapo huyo dada angekuwa ndugu yangu kwa namna yeyote ningemmaliza huyo jamaa... maana ana deserve...

Changamoto anazopitia isiwe chanzo cha kuua mtu, tena mkewe ambae wamezaa watoto?

Hata nikiwa katika nafasi ya Kweka siwezi kuua mtu kisa ugomvi wa nyumba... kufanya kisasi haimaanishi sina uwezo wa ku control emotions zangu...

Kweka anyongwe, asiponyongwa ndugu za Jane wamalizane nae...
 
Ukimsikiliza dada yake Jane wa tumbo Moja kaongea kwa busara sana lawama zimedondokea kwa Jane kumbe kesi sio ya leo ni ya muda na alishauriwa na alikua kinacho enda kitokea
Katika familia ya Urassa huyu dada yake Jane peke yake ndio anaonekana ana hofu ya MUNGU , pasipokujali aliyeuwawa ni mdogo wake wa damu lakini kaamua aweke wazi ukweli wa mambo ulivyo...
 
Katika familia ya Urassa huyu dada yake Jane peke yake ndio anaonekana ana hofu ya MUNGU , pasipokujali aliyeuwawa ni mdogo wake wa damu lakini kaamua aweke wazi ukweli wa mambo ulivyo...
Kuna kingine kimejificha zaidi ya umiliki wa hiyo nyumba. Naamini ni uchepukaji na kiburi!
 
Hati ya nyumba tayari ilishatoka mkuu ikiwa na majina ya watoto - hata mke hakua mmiliki bali msimamizi tu mpaka mtoto wao wa kwanza atakapofikisha miaka 18.
Kama ni hivyo, kwamba lengo la Mke ni Nyumba hiyo kumilikiwa na Watoto na sio yeye Wala mume...... mbona Mke hakutumia busara ya kuàndika Majina ya Mume na Mke kama wasimamizi, na Watoto kama Wamiriki mpaka watapofikisha miaka 18...?
 
Jane Urassa alikuwa mjinga, lakini Laurent Kweka naye kaamua kuhitimu ujinga kwa vitendo! 😂🤦🏽‍♂️

Yaani badala ya kutatua matatizo kwa akili, risasi ndiyo imekuwa suluhisho?

Hii siyo hasira tena, ni akili kuchukua likizo ya kudumu! 😅


Ukatili hauna utani, na hakuna ugomvi unaostahili kuishia kwa mauaji.
 
Mimi huwezi kunifananisha na huyo mpuuzi...
Nimetoa mfano , endapo huyo dada angekuwa ndugu yangu kwa namna yeyote ningemmaliza huyo jamaa... maana ana deserve...

Changamoto anazopitia isiwe chanzo cha kuua mtu, tena mkewe ambae wamezaa watoto?

Hata nikiwa katika nafasi ya Kweka siwezi kuua mtu kisa ugomvi wa nyumba... kufanya kisasi haimaanishi sina uwezo wa ku control emotions zangu...

Kweka anyongwe, asiponyongwa ndugu za Jane wamalizane nae...
Sasa Hapo ungekuwa na tofauti gani na Kweka?
Unasema Kweka ana deserve kuuliwa kwakuwa kaua na wewe ukiua uta deserve kuuliwa
Hapo itakuwa wote mmeshindwa Ku handle changamoto katika namna yakutokuongeza changamoto zingine
 
Unafikiri alitengeneza hati kwa majina ya watoto bila kumshirikisha mumewe? wanaume karibu wote huwa wanataka mali zao ziende kwa watoto wao, haikufikirishi kwanini Kweka yeye alikua anapinga?

Inaonekena tayari kulikua na migogoro, hata hayo mambo ya kutishana yalisharipotiwa mpaka polisi. Ila, what if umuweke umiliki, afe aache wosia kwamba nusu yake wapewe ndugu zake na si watoto au worse apewe mchepuko wake?
Ila nyie wanawake ni wabinafsi sana aisee
 
Mimi huwezi kunifananisha na huyo mpuuzi...
Nimetoa mfano , endapo huyo dada angekuwa ndugu yangu kwa namna yeyote ningemmaliza huyo jamaa... maana ana deserve...

Changamoto anazopitia isiwe chanzo cha kuua mtu, tena mkewe ambae wamezaa watoto?

Hata nikiwa katika nafasi ya Kweka siwezi kuua mtu kisa ugomvi wa nyumba... kufanya kisasi haimaanishi sina uwezo wa ku control emotions zangu...

Kweka anyongwe, asiponyongwa ndugu za Jane wamalizane nae...
Hakuna anayependa kuua bwana labda wanajeshi vitani na polisi wakiwa kwenye mission za majambazi yenye siraha.

Kama waliishi miaka 18 iweje auliwe wakati huu?

Kuna jambo lilipelekea kitendo hicho kufanyika
 
Back
Top Bottom