Ukweli kuhusu Jane Urassa - mke aliyeuawa kwa risasi đź’”

Ukweli kuhusu Jane Urassa - mke aliyeuawa kwa risasi đź’”

Ila Kweka.! Nashauri kabla ya kuhusiana na mtu angalia jinsi anavyowatendea watu wengine.

Kuna watu hawatoi heshima kwa wazazi wao, ndugu na jamii inayowazunguka.
Wamejawa viburi na majivuno.

Sasa mtu kama huyu asiyejali kuhusu wazazi wake, vipi awaze kuhusu wewe.

Tukifatilia uhusiano wa Kweka na wazazi wake, kazini, majirani utakuta tu alikua mtu wa matatizo.

Ukatili wa hali ya juu kumuua mama watoto wako.
Huyo jamaa hilo tukio litamtesa sana. Unamuua mama watoto wako kisa nyumba,, alafu hiyo nyumba sasa mimi ningekuwa mtot hata nyumba yako nakuachia baki nayo
 
NINAVYOWAZA MIMI
1.kiwanja lilikuwa Cha mwanamke

2.mwanaume alikuwa na upendo sana kwa mke wake na hakujua ipo siku wataachana hivyo akajenga kwenye kiwanja cha mke wake ili waendelee kulisongesha.

3.Migogoro ilivyoanza mwanamke akaona mwanaume atafaidi hivyo Bora mali ziandikwe majina ya watoto (Kosa kubwa)

4.Mwanaume akaona anaporwa hakika yake aliyoipambania kwa siku nyingi

5.Yalipotokea mabishano kwa kuwa jamaa moyo ulishachoka ndo akalipuka hasira kama vile na kufanya alichokifanya.(Hakudhamiria kuua ila alishindwa kucontrol hasira,sote hatuijui mke wake alimtamkia maneno gani)

6.ushauri wangu,ndoa inapovunjika sote wanaume kwa Wanawake tusiwe wabinafsi,kila mmoja ana mchango wake,hata kama mmejenga nyumba ya bilioni na mwanamke ni mke wa nyumbani hafanyi kazi ya kuingiza kipato,still ana haki kwani Kuna mchango wake hata wa kimawazo,the same tu mwanaume hata kama kiwanja si chake lakini Kuna mchango wake hadi kufika walipofikia

Hivyo basi ilitakiwa nyumba iuzwe kila mmoja ashike chake na watoto waendelee kutunzwa na baba na mama kwa utaratibu mliokubaliana

N:B wanaume tuache ubabe pia Wanawake punguzeni midomo na maneno ya kukera yanayoamsha hasira za ndani.

Habari zenu wakuu,
 
#FACT-CHECKING

Usidanganyike, mambo kwa ground yapo tofauti sana. Kwa ushahidi, tupitie ni yapi ya kweli na yapi si kweli kuhusu kifo cha Jane Maloo Urassa ⚰️ aliyeuawa na Laurence Kweka, mwanaume aliyekosa akili, busara na utashi wa kibinadamu.


View attachment 3686843

  1. Jane na Bw. Kweka waliishi kwenye ndoa kwa miaka 18 na miezi 8 na wana watoto 4 - KWELI

  2. Jane alikua mtumishi aliyeajiriwa, mwenye kipato chake binafsi, na elimu ya chuo kikuu (Masters) - KWELI

  3. Jane alimiliki mali binafsi alizotafuta kabla ya ndoa ikiwemo kiwanja kilichojengwa nyumba iliyoleta mgogoro - KWELI

  4. Jane alikua ameshaondoka hapo nyumbani kwenye migogoro kwa zaidi ya miezi miwili na kwenda kuishi kwa ndugu zake na alimuachia bwana Kweka nyumba na pamoja na watoto wote aishi nao - KWELI

  5. Mgogoro mkubwa ulijitokeza miezi kadhaa nyuma baada ya hati ya nyumba kutoka na majina ya watoto na Jane kama msimamizi mpaka pale mtoto wao wa kwanza atakapofikisha miaka 18 - KWELI

  6. Jane alitaka hati ya nyumba iwe kwa jina lake - SI KWELI

  7. Jane aliweza kutengeneza hati sababu kiwanja kilikua mali yake na bwana Kweka hakutaka majina ya watoto kwenye hati bali jina lake mwenyewe, sababu aliamini nyumba ameijenga kwa jasho lake - KWELI

  8. Jane alirudi nyumbani kwao masaa machache kabla ya kuuawa, kuwapelekea watoto wake chakula kwa sababu walikua wameishiwa na baba wa watoto alikua safarini Moshi - KWELI

    PS:
    Mtoto wao aliyempigia simu mama yake ataishi kwa uchungu maisha yake yote, akijua bila ya simu yake, mama yao angekua hai leo.

    View attachment 3686846

  9. Kabla ya mauaji, tayari kulikua na kesi polisi na ustawi wa jamii dhidi ya bwana Kweka kuhusu ukatili wa kijinsia na kumtishia mkewe maisha - KWELI

Vyanzo vya taarifa / Sources: (Ukija kubisha na wewe ulete vyanzo vyako)

Tofauti na mambo yanayoendelea mtandaoni na watu wanavyoleta mizaha kuhusu ukatili wa kijinsia na mauaji, Jane Urassa aliuawa kwa sababu alikua tayari kuachana na mume wake na kuhakikisha mali zao walizochuma pamoja zinabaki kwa watoto wao.

Alifanya vile ambavyo wanaume wanashauri humu jukwaani kwamba, using’ang’anie mali ambayo si yako, akampisha mwanaume kwenye nyumba yao, akaacha watoto bila kuwang'ang'ania na bado akauawa kikatili.


Hitimisho:

Jane alifikia mwisho kwenye maisha ya ndoa ila Mr. Kweka hakuwa tayari kuona mwisho wa ndoa yao pekee, alitaka pia kuhakikisha ni mwisho wa maisha yake pia - kusudi lake limetimia.

R.IP Jane đź’”

Tupinge Femicide / mauaji ya wanawake

Alamsiki!
Nilishawahi kusema Kuna mwanaume mengine yanalazimisha wanawake Sasa haya ndio matokeo.

Narudia tena hii ya kuokotana sijui kulazimisha kuolewa haya ndio matokeo yake Sasa.

Wanawake Huwa hawaelewi Hadi yawakute eti kwamba utamshauri aelewe,kenge anasikia Kwa damu.
 
1. Mama kaacha watoto aliowazaa, kwenye kiwanja alichonunua kwa pesa yake? Kuna kitu unaficha ndugu. Nini sababu ya kufukuzwa hapo nyumbani mbona hutaji MZIGO WA MADENI aliyokua nayo Dada yako MANKA? Wadai je?

2. MANKA alikua na mikopo kila kona ya nchi hii na haieleweki alikua anafanyia nini. Wadai walishadai mpaka wakachemsha. Kutimuliwa kulikuja baada ya drama za manka na mikopo na wadai.
 
Sasa Hapo ungekuwa na tofauti gani na Kweka?
Unasema Kweka ana deserve kuuliwa kwakuwa kaua na wewe ukiua uta deserve kuuliwa
Hapo itakuwa wote mmeshindwa Ku handle changamoto katika namna yakutokuongeza changamoto zingine
Ukiua na wewe inahitajika uuliwe...
Mimi sio muuaji... nimelipiza kisasi...
 
Hakuna anayependa kuua bwana labda wanajeshi vitani na polisi wakiwa kwenye mission za majambazi yenye siraha.

Kama waliishi miaka 18 iweje auliwe wakati huu?

Kuna jambo lilipelekea kitendo hicho kufanyika
Jambo lipi?
Jambo lipi huyo dada amefanya astahili kifo? Unaweza kuelezea ni jambo lipi?
Kama ni suala la nyumba si angepeleka kesi kwa kufuata protocol...
 
Jambo lipi?
Jambo lipi huyo dada amefanya astahili kifo? Unaweza kuelezea ni jambo lipi?
Kama ni suala la nyumba si angepeleka kesi kwa kufuata protocol...
Usijifanye unajua sana kushauri mambo ya ndani ya watu na wewe pimbi wewe

Hata wewe ukizingua unakula chuma tu
 
Usijifanye unajua sana kushauri mambo ya ndani ya watu na wewe pimbi wewe

Hata wewe ukizingua unakula chuma tu
hand-showing-the-middle-finger-and-flipping-off-the-camera-cut-out-on-black-background.jpg
 
Jane licha ya kipato chake na kumuachia mmewe watoto na nyumba kwenda kukaa kwingne hakukubali na kuja kuliamsha upya. Uzuri kweka alilea watoto vizuri na bado hakuingiza michepuko.
 
Kufuata protocol mtu ana nia ya kukudhulumu macho makavu.?

Tena huo ni wizi wa wazi kwa kutumia udhaifu
Kwa hivyo ndipo aue? Aue mkewe ambae ameishi nae miaka 18 na wana watoto wanne , kwamba alikuwa anataka kumdhulumu nyumba?
 
Huwezi jua nini kilipelekea. Kwani yeye ni wa kwanza kuua?
Watanzania msiwe mnatetea uovu na mauaji kwa kigezo unapitia au ulishapitia nyakati ngumu kwenye mahusiano/ndoa yako...

Hapo unatetea uovu na mauaji... jibu la ajabu sana kwamba siwezi fahamu nini kilipelekea, ni kweli siwezi fahamu lakini si kwa kumtoa mtu uhai...

Mnaotetea huu ujinga mna tofauti gani na madikteta, wauaji, watoa kafara...

Inawezekana maisha ya mahusiano uliyopitia ukaumizwa ujinga ulikuwa ni wako mwenyewe, sasa isiwe sababu ya kuhalalisha ukatili na mauaji kisa mlitendwa...
 
Back
Top Bottom