Ukweli kuhusu Jane Urassa - mke aliyeuawa kwa risasi 💔

Ukweli kuhusu Jane Urassa - mke aliyeuawa kwa risasi 💔

#FACT-CHECKING

Usidanganyike, mambo kwa ground yapo tofauti sana. Kwa ushahidi, tupitie ni yapi ya kweli na yapi si kweli kuhusu kifo cha Jane Maloo Urassa ⚰️ aliyeuawa na Laurence Kweka, mwanaume aliyekosa akili, busara na utashi wa kibinadamu.

View attachment 3686843

  1. Jane na Bw. Kweka waliishi kwenye ndoa kwa miaka 18 na miezi 8 na wana watoto 4 - KWELI

  2. Jane alikua mtumishi aliyeajiriwa, mwenye kipato chake binafsi, na elimu ya chuo kikuu (Masters) - KWELI

  3. Jane alimiliki mali binafsi alizotafuta kabla ya ndoa ikiwemo kiwanja kilichojengwa nyumba iliyoleta mgogoro - KWELI

  4. Jane alikua ameshaondoka hapo nyumbani kwenye migogoro kwa zaidi ya miezi miwili na kwenda kuishi kwa ndugu zake na alimuachia bwana Kweka nyumba na pamoja na watoto wote aishi nao - KWELI

  5. Mgogoro mkubwa ulijitokeza miezi kadhaa nyuma baada ya hati ya nyumba kutoka na majina ya watoto na Jane kama msimamizi mpaka pale mtoto wao wa kwanza atakapofikisha miaka 18 - KWELI

  6. Jane alitaka hati ya nyumba iwe kwa jina lake - SI KWELI

  7. Jane aliweza kutengeneza hati sababu kiwanja kilikua mali yake na bwana Kweka hakutaka majina ya watoto kwenye hati bali jina lake mwenyewe, sababu aliamini nyumba ameijenga kwa jasho lake - KWELI

  8. Jane alirudi nyumbani kwao masaa machache kabla ya kuuawa, kuwapelekea watoto wake chakula kwa sababu walikua wameishiwa na baba wa watoto alikua safarini Moshi - KWELI

    PS:
    Mtoto wao aliyempigia simu mama yake ataishi kwa uchungu maisha yake yote, akijua bila ya simu yake, mama yao angekua hai leo.

    View attachment 3686846

  9. Kabla ya mauaji, tayari kulikua na kesi polisi na ustawi wa jamii dhidi ya bwana Kweka kuhusu ukatili wa kijinsia na kumtishia mkewe maisha - KWELI

Vyanzo vya taarifa / Sources: (Ukija kubisha na wewe ulete vyanzao vyako)

Tofauti na mambo yanayoendelea mtandaoni na watu wanavyoleta mizaha kuhusu ukatili wa kijinsia na mauaji, Jane Urassa aliuawa kwa sababu alikua tayari kuachana na mume wake na kuhakikisha mali zao walizochuma pamoja zinabaki kwa watoto wao.

Alifanya vile ambavyo wanaume wanashauri humu jukwaani kwamba, using’ang’anie mali ambayo si yako, akampisha mwanaume kwenye nyumba yao, akaacha watoto bila kuwang'ang'ania na bado akauawa kikatili.

Hitimisho:

Jane alifikia mwisho kwenye maisha ya ndoa ila Mr. Kweka hakuwa tayari kuona mwisho wa ndoa yao pekee, alitaka pia kuhakikisha ni mwisho wa maisha yake pia - kusudi lake limetimia.

R.IP Jane 💔

Tupinge Femicide / mauaji ya wanawake

Alamsiki!
YOTE ULIYOYAANDIKA NI YAUONGO NA UMETUMWA ILI KUSAFISHA UCHAFU ULIOPO
 
YOTE ULIYOYAANDIKA NI YAUONGO NA UMETUMWA ILI KUSAFISHA UCHAFU ULIOPO
Umenituma wewe?

200.gif
 
Wewe bado huna maisha huwezi elewa au we ulipewa urithi, hapa tunaonhea fighters from zero to hero, mi nimetembeza vitumbua Arusha nimepigwa mvua leo hii niambiwe jina langu lisiwepo liwepo la watoto na mke kama msimammizi? Kwanini nae asiniweke mimi kama msimammizi? Tulia kaka hii ngoma huwezi ijua kaka, we fight hard mnatuona usoni tuna furaha kumbe moyoni tuna hudhuni, tunapitia mengi kwenye utafutaji bado nawe unani chezea, basi tafuta refa wa kukubeba
Hustler's Tu Ndo tukaelewana kwenye hili
Muda huo huo ushapoteza vyote mke ana file talaka
 
Ushauri mzuri sana mzee mwenzangu, uzee ni dawa!💪
Tafuta usome kitabu cha Mzee Mengi "I Can, I must , I will"

Kwenye kosa binafsi ambalo mwenzetu alilifanya ni kuongeza watoto na Mama mwingine pamoja na kukubali kugawana Mali na aliyekuwa mkewe Bi Mercy Mengi

Wanasema kidole kimoja hakivunji chawa, kwahiyo mnapokuwa na hisa 100/100 then mkakubali kuzigawanya, hazitakuwa 100/100 tena, bali zinaweza kuwa ni 40/60 ama vinginevyo

All in all, sisi tuliobaki, tunayo nafasi ya kurekebisha na kujenga kwaajili ya kesho ya vizazi vyetu ili kama tulizaliwa masikini, basi kizazi cha 3 na 4 wakute tayari tuliwachongea barabara ya wao kupita

Kama ambavyo Familia ya Mo, na Mengi waliyofanya kwaajili ya vizazi vyao
 
Hata mimi nilivyosimuliwa story nilisema hivi hivi kitendo cha kumuua mkewe akakimbilia polisi kujisalimisha, alipanga kumuua hapo kabla, kwanini asingejipiga risasi na yeye bastola si alikuwa nayo,, na kama alikuwa amechsnganyikiwa kwanini hakummaliza na house aliyekutana nae mlangoni, na je boda aliyempeleka polisi!!!! Na fun enough akaenda kituo ambacho kuna washkaji zake kwaninj asingeenda mabwepande akakimbilia kawe,, alijua akikaa pale raia walikuwa wanammaliza maana majirani wanamuelewa mwanamke kuliko yeye ambae muda wake mwingi alikuwa kwa mama yake moshi,,

Kulikuwa na mvutano wa upande upi uzike, Mr akawa anakigugumizi kutetea upande wa mwanaume nilimwambia kabisa mi ukiniua usinizike acha nizikwe hata na serikali ila sio wewe!!!

Wanaume wa sasa kichefuchefu sana akili fupi kama mboo zenu
So Umempa idea ya kukuua
 
Wewe bado huna maisha huwezi elewa au we ulipewa urithi, hapa tunaonhea fighters from zero to hero, mi nimetembeza vitumbua Arusha nimepigwa mvua leo hii niambiwe jina langu lisiwepo liwepo la watoto na mke kama msimammizi? Kwanini nae asiniweke mimi kama msimammizi? Tulia kaka hii ngoma huwezi ijua kaka, we fight hard mnatuona usoni tuna furaha kumbe moyoni tuna hudhuni, tunapitia mengi kwenye utafutaji bado nawe unani chezea, basi tafuta refa wa kukubeba
Acha ujinga na ujuaji sasa unalilia mali iliyonunuliwa na mwanamke kweli wewe mzima? Wewe acha ujinga nyie ndiyo mnaopenda kulelewa umeitafuta hiyo mali wapi weweeee huna ndiyo maana unaongea kama mvulana
 
Ni sahihi, lakini kwanini hizi changamoto za mali zinatukumba zaidi sisi ngozi nyeusi?

Unajua familia ya Mo, inao utajiri wa vizazi vitatu kama sio vinne sasa

Na tayari Kuna succession plan ya kumrithisha mtoto Mkubwa wa Mo, nadhani anaitwa Abbas kama sijakosea ili aendeleze

Sisi huku ngozi nyeusi tunaweza kuibiana na kudhurumiana tu

Mimi naanza mchakato wa kuweka assets zote chini ya bodi ya Kampuni ikiwemo nyumba tunayoishi

Kila jambo litahitaji uamuzi wa kikao Cha Bodi
Kwa wengine mkakati huo tumeuanza zamani. Ukoo wetu mtoto haruhusiwi kurithi, kazi ya mtoto ni kutunza mali ya mzazi. Ukiwa tumboni tu, baba yako anaanza kukuhubiria.

Pili, tatizo kubwa kwa vijana ni pale unapooa ukaanza kuchanganya mapato. Hilo ndilo kosa kubwa. Mwanamke anakuwa na hela yake na ana invest anavyopenda. Wewe nawe unakuwa na mfuko wako ambao mwanamke hajui una kiasi gani. Ila mnakubaliana majukumu. Mfano, mwanaume lazima ujue kuwa umeoa siyo umeolewa. Hivyo utahakikisha familia yako ina pahala pa kukaa, kula, kuvaa, watoto kwenda shule etc. Kama mke anachangia ni pale anapopenda. Kwa mtindo huo, hakutakuwa na risasi maana hata nyumba ukiwa unajenga, humuulizi contribution, akitoa ni zawadi tu. Hati ni jina la mwanaume tu. Tofautisheni kuoa na kuolewa. Kiafrika hakuna neno TUMEOANA.
 
Kwa wengine mkakati huo tumeuanza zamani. Ukoo wetu mtoto haruhusiwi kurithi, kazi ya mtoto ni kutunza mali ya mzazi. Ukiwa tumboni tu, baba yako anaanza kukuhubiria.

Pili, tatizo kubwa kwa vijana ni pale unapooa ukaanza kuchanganya mapato. Hilo ndilo kosa kubwa. Mwanamke anakuwa na hela yake na ana invest anavyopenda. Wewe nawe unakuwa na mfuko wako ambao mwanamke hajui una kiasi gani. Ila mnakubaliana majukumu. Mfano, mwanaume lazima ujue kuwa umeoa siyo umeolewa. Hivyo utahakikisha familia yako ina pahala pa kukaa, kula, kuvaa, watoto shule etc. Kama mke anachangia ni pale anapopenda. Kwa mtindo huo, hakutakuwa na risasi maana hata nyumba ukiwa unajenga, humuulizi contribution, akitoa ni zawadi tu. Hati ni jina la mwanaume tu. Tofautisheni kuoa na kuolewa. Kiafrika hakuna neno TUMEOANA.
Lazima pawepo na succession plan, kwahiyo miongoni mwa watoto sharti awepo Kiongozi kwaajili ya kuyapokea na kuendeleza maono ya Baba.

Mimi nitakuwa Mzee Mkoloni, watoto wangu wataoa na kukaa kwenye nyumba yangu.

Watafanya kazi kwenye miradi ya familia, na nitawalipa mishahara huku wakiendelea kukua na kujifunza namna bora ya kuendeleza kile Baba yao nimekianzisha

Sio kazi rahisi kuvunja mnyororo wa Umasikini miongoni mwa Jamii zetu

Ni vita inahitaji askari shupavu, na hao askari ni sisi Wazazi ndiyo tunawaandaa

Kama ulivyosema, hakuna kurithi ila watoto wanaweza kuwa sehemu ya bodi ya wakurugenzi kwaajili ya kuwaingiza kwenye maamuzi na kupata uzoefu, ili biashara ziweze kuendeleza hata baada ya Mzee kuaga maisha
 
Kunakuwa na Advisory Board tu. Siyo Governing Board.
 
Kunakuwa na Advisory Board tu. Siyo Governing Board.
Ni sahihi, japo kwenye Governing board ni muhimu kuwa-enject watoto wako kwaajili ya kuchota uzoefu na kujifunza namna sahihi ya kufanya maamuzi
 
Mgogoro mkubwa ulijitokeza miezi kadhaa nyuma baada ya hati ya nyumba kutoka na majina ya watoto na Jane kama msimamizi mpaka pale mtoto wao wa kwanza atakapofikisha miaka 18 - KWELI
I don’t condone the husband’s violence, but I don’t think the wife wasn’t at fault.

Dhamana ya Jane kuwa msimamizi ilipatikanaje?

Tumcheni Mungu wetu. He brought us here empty-handed, and empty-handed we will return to Him!
 
Back
Top Bottom