Binti wa zamani
Platinum Member
- Nov 19, 2011
- 14,955
- 36,392
- Thread starter
- #61
Hakua mnyonge, kama mnataka wanawake wa kuwaendesha, basi hawa wasomi na wanaijitafutia hela zao wenyewe achaneni nao!RIP Jane! Ila ubabe ulikuwa nao!
Hakua mnyonge, kama mnataka wanawake wa kuwaendesha, basi hawa wasomi na wanaijitafutia hela zao wenyewe achaneni nao!RIP Jane! Ila ubabe ulikuwa nao!
Taasisi inahitaji uvumilvu sana hii, hata tuliomo bado tunajifunza mapya kila uchwao!Nakuwa msomaji zaidi hapa, nipate maarifa zaidi, kuhusu taasisi ya ndoa
Yamemkuta!Hakua mnyonge, kama mnataka wanawake wa kuwaendesha, basi hawa wasomi na wanaijitafutia hela zao wenyewe achaneni nao!
😂😂😂😂😂 😂 Hapo ndiyo inakuwaga kamzozo, nyonyo ziko mkononi bibie anakwambia nina kiwanja basi tujenge, unajikuta umekubali tu. Mapenzi yakipungua akili ikakukaa sawa, tayari ushamwaga milioni 100 nyumba iko kwenye finishing, hapo ndiyo hasira zinapofukuta sasa.
Tutasikia mengi...Hati ya nyumba tayari ilishatoka mkuu ikiwa na majina ya watoto - hata mke hakua mmiliki bali msimamizi tu mpaka mtoto wao wa kwanza atakapofikisha miaka 18.
Hakika 🙏Duh.... TUTUBU na kuiamini injili tu! nimemaliza...
Kama yeye alikuwa mmiliki wa kiwanja, na akajenga Kweka, huoni kuwa ingekuwa jambo la busara angemshirikisha Kweka katika ku process hati ya umiliki? Na kama Kweka anaumwa saratani, ni ingekuwa busara zaidi kumshirikisha yeye kwani at the end of the day, ataaga dunia na kumwachia nyumba, other factors constant.Umesoma uzi?
Hakubadili alitengeneza (kwa sababu yeye ndiye alikua mmiliki wa kiwanja) na akaweka majina ya watoto badala ya jina lake na la mumewe.
Hebu wewe nipe ukweli, na usisahau kuweka vyanzo vyako vya taarifa.Mleta mada unatumia nguvu nyingi kugeuza ukweli kuwa UONGO, hata hivyo haitosaidia
Acha kuwamba ngoma wew, tumeambiwa majina aliyoweka katka hati ni lake na majina ya watoto, mme alitengwa, tena alifanya hvyo kwa kificho!Umesoma uzi?
Hakubadili alitengeneza (kwa sababu yeye ndiye alikua mmiliki wa kiwanja) na akaweka majina ya watoto badala ya jina lake na la mumewe.
Yeah . Kuna namna watu inabidi wafanye background checking... Sema hii inabidi utumie akili (logic) kuliko hisia. Utaujua ukweli wa mtu alivyoIla Kweka.! Nashauri kabla ya kuhusiana na mtu angalia jinsi anavyowatendea watu wengine.
Kuna watu hawatoi heshima kwa wazazi wao, ndugu na jamii inayowazunguka.
Wamejawa viburi na majivuno.
Sasa mtu kama huyu asiyejali kuhusu wazazi wake, vipi awaze kuhusu wewe.
Tukifatilia uhusiano wa Kweka na wazazi wake, kazini, majirani utakuta tu alikua mtu wa matatizo.
Ukatili wa hali ya juu kumuua mama watoto wako.
😂😂😂 utafanya wafuasi wa Jane wapandwe na kichaa bure hapa. Em tulia hata kuzika bado. LolNasimama na kweka pia tupo tunalishughulikia tatizo lake hapa osterbay tukiwa na mawakili mahiri wa sheria aweze kupata haki yake ya kimsingi arudi uraiani mapema sana🙏
Kwenye ndoa au mahusiano,#FACT-CHECKING
Usidanganyike, mambo kwa ground yapo tofauti sana. Kwa ushahidi, tupitie ni yapi ya kweli na yapi si kweli kuhusu kifo cha Jane Maloo Urassa ⚰️ aliyeuawa na Laurence Kweka, mwanaume aliyekosa akili, busara na utashi wa kibinadamu.
View attachment 3686843
- Jane na Bw. Kweka waliishi kwenye ndoa kwa miaka 18 na miezi 8 na wana watoto 4 - KWELI
- Jane alikua mtumishi aliyeajiriwa, mwenye kipato chake binafsi, na elimu ya chuo kikuu (Masters) - KWELI
- Jane alimiliki mali binafsi alizotafuta kabla ya ndoa ikiwemo kiwanja kilichojengwa nyumba iliyoleta mgogoro - KWELI
- Jane alikua ameshaondoka hapo nyumbani kwenye migogoro kwa zaidi ya miezi miwili na kwenda kuishi kwa ndugu zake na alimuachia bwana Kweka nyumba na pamoja na watoto wote aishi nao - KWELI
- Mgogoro mkubwa ulijitokeza miezi kadhaa nyuma baada ya hati ya nyumba kutoka na majina ya watoto na Jane kama msimamizi mpaka pale mtoto wao wa kwanza atakapofikisha miaka 18 - KWELI
- Jane alitaka hati ya nyumba iwe kwa jina lake - SI KWELI
- Jane aliweza kutengeneza hati sababu kiwanja kilikua mali yake na bwana Kweka hakutaka majina ya watoto kwenye hati bali jina lake mwenyewe, sababu aliamini nyumba ameijenga kwa jasho lake - KWELI
- Jane alirudi nyumbani kwao masaa machache kabla ya kuuawa, kuwapelekea watoto wake chakula kwa sababu walikua wameishiwa na baba wa watoto alikua safarini Moshi - KWELI
PS:
Mtoto wao mkubwa aliyempigia simu mama yake ataishi kwa uchungu maisha yake yote, akijua bila ya simu yake, mama yao angekua hai leo.
View attachment 3686846
- Kabla ya mauaji, tayari kulikua na kesi polisi na ustawi wa jamii dhidi ya bwana Kweka kuhusu ukatili wa kijinsia na kumtishia mkewe maisha - KWELI
Vyanzo vya taarifa / Sources: (Ukija kubisha na wewe ulete vyanzao vyako)
Tofauti na mambo yanayoendelea mtandaoni na watu wanavyoleta mizaha kuhusu ukatili wa kijinsia na mauaji, Jane Urassa aliuawa kwa sababu alikua tayari kuachana na mume wake na kuhakikisha mali zao walizochuma pamoja zinabaki kwa watoto wao.
Alifanya vile ambavyo wanaume wanashauri humu kwamba using’ang’anie mali ambayo si yako, akampisha mwanaume kwenye nyumba yao, akaacha watoto bila kuwang'ang'ania na bado akauawa kikatili.
Hitimisho:
Jane alifikia mwisho kwenye maisha ya ndoa ila Mr. Kweka hakuwa tayari kuona mwisho wa ndoa yao pekee, alitaka pia kuhakikisha ni mwisho wa maisha yake pia - kusudi lake limetimia.
R.IP Jane 💔
Tupinge Femicide / mauaji ya wanawake
Alamsiki!
Kwa nini hakutaka iwe na majina ya wote kama alikuwa na nia njema?6. Jane alitaka hati ya nyumba iwe kwa jina lake - SI KWELI
Yaani juzi ndo alijua kuwa kiwanja ni chake? Why ha aje abadilike suddenly kama hakuwa na nia mbaya?7. Jane aliweza kutengeneza hati sababu kiwanja kilikua mali yake na bwana Kweka hakutaka majina ya watoto kwenye hati bali jina lake mwenyewe, sababu aliamini nyumba ameijenga kwa jasho lake - KWELI
8. Jane alirudi nyumbani kwao masaa machache kabla ya kuuawa, kuwapelekea watoto wake chakula kwa sababu walikua wameishiwa na baba wa watoto alikua safarini Moshi - KWELI
Binti wa zamani nakutingisha kote makebo kwa baba mjengo wa yours, siku akizingua unaweza mkazichapa kavu kavu?😎😎Hakua mnyonge, kama mnataka wanawake wa kuwaendesha, basi hawa wasomi na wanaijitafutia hela zao wenyewe achaneni nao!
Unafikiri alitengeneza hati kwa majina ya watoto bila kumshirikisha mumewe? wanaume karibu wote huwa wanataka mali zao ziende kwa watoto wao, haikufikirishi kwanini Kweka yeye alikua anapinga?Kama yeye alikuwa mmiliki wa kiwanja, na akajenga Kweka, huoni kuwa ingekuwa jambo la busara angemshirikisha Kweka katika ku process ya umiliki?
Inaonekena tayari kulikua na migogoro, hata hayo mambo ya kutishana yalisharipotiwa mpaka polisi. Ila, what if umuweke umiliki, afe aache wosia kwamba nusu yake wapewe ndugu zake na si watoto au worse apewe mchepuko wake?Na kama Kweka anaumwa saratani, ni ingekuwa busara zaidi kumshirikisha yeye kwani at the end of the day, ataaga dunia na kumwachia nyumba, other factors constant.