Binti wa zamani
Platinum Member
- Nov 19, 2011
- 14,951
- 36,339
#FACT-CHECKING
Usidanganyike, mambo kwa ground yapo tofauti sana. Kwa ushahidi, tupitie ni yapi ya kweli na yapi si kweli kuhusu kifo cha Jane Maloo Urassa ⚰️ aliyeuawa na Laurence Kweka, mwanaume aliyekosa akili, busara na utashi wa kibinadamu.
Vyanzo vya taarifa / Sources: (Ukija kubisha na wewe ulete vyanzo vyako)
Tofauti na mambo yanayoendelea mtandaoni na watu wanavyoleta mizaha kuhusu ukatili wa kijinsia na mauaji, Jane Urassa aliuawa kwa sababu alikua tayari kuachana na mume wake na kuhakikisha mali zao walizochuma pamoja zinabaki kwa watoto wao.
Alifanya vile ambavyo wanaume wanashauri humu jukwaani kwamba, using’ang’anie mali ambayo si yako, akampisha mwanaume kwenye nyumba yao, akaacha watoto bila kuwang'ang'ania na bado akauawa kikatili.
Hitimisho:
Jane alifikia mwisho kwenye maisha ya ndoa ila Mr. Kweka hakuwa tayari kuona mwisho wa ndoa yao pekee, alitaka kuhakikisha ni mwisho wa maisha yake pia - kusudi lake limetimia.
R.IP Jane 💔
Tupinge Femicide / mauaji ya wanawake
Alamsiki!

- Jane na Bw. Kweka waliishi kwenye ndoa kwa miaka 18 na miezi 8 na wana watoto 4 - KWELI
- Jane alikua mtumishi aliyeajiriwa, mwenye kipato chake binafsi, na elimu ya chuo kikuu (Masters) - KWELI
- Jane alimiliki mali binafsi alizotafuta kabla ya ndoa ikiwemo kiwanja kilichojengwa nyumba iliyoleta mgogoro - KWELI
- Jane alikua ameshaondoka hapo nyumbani kwenye migogoro kwa zaidi ya miezi miwili na kwenda kuishi kwa ndugu zake na alimuachia bwana Kweka nyumba na pamoja na watoto wote aishi nao - KWELI
- Mgogoro mkubwa ulijitokeza miezi kadhaa nyuma baada ya hati ya nyumba kutoka na majina ya watoto na Jane kama msimamizi mpaka pale mtoto wao wa kwanza atakapofikisha miaka 18 - KWELI
- Jane alitaka hati ya nyumba iwe kwa jina lake - SI KWELI
- Jane aliweza kutengeneza hati sababu kiwanja kilikua mali yake na bwana Kweka hakutaka majina ya watoto kwenye hati bali jina lake mwenyewe, sababu aliamini nyumba ameijenga kwa jasho lake - KWELI
- Jane alirudi nyumbani kwao masaa machache kabla ya kuuawa, kuwapelekea watoto wake chakula kwa sababu walikua wameishiwa na baba wa watoto alikua safarini Moshi - KWELI
PS:
Mtoto wao aliyempigia simu mama yake ataishi kwa uchungu maisha yake yote, akijua bila ya simu yake, mama yao angekua hai leo.
- Kabla ya mauaji, tayari kulikua na kesi polisi na ustawi wa jamii dhidi ya bwana Kweka kuhusu ukatili wa kijinsia na kumtishia mkewe maisha - KWELI