Ukweli kuhusu Jane Urassa - mke aliyeuawa kwa risasi 💔

Ukweli kuhusu Jane Urassa - mke aliyeuawa kwa risasi 💔

Ila kuna wanaume wananyanyasika sana katka ndoa zao, sema machoz na maumiv yao hakuna anayeyajali!
Kilio cha mwanaume ni kama cha samaki.
Machozi yanaliwa na maji.
Wachangiaji wote wanamuona bro Kweka mzembe kujenga nyumba ya familia kwenye kiwanja cha mkewe.
Binafsi sijaona kosa, tatizo ni tamaa ya mali iliyopitiliza ya bibie.
 
Ni kweli hatuwezi kuujua ukweli wote, Laurence na Jane ndiyo wanajua.

Jane si mmiliki bali msimamizi mpaka mtoto wao wa kwanza (15 years old) atakapofikisha miaka 18.
Wote yeye na mumewe hawakuwa wamiliki, na Lawrence ndiyo alikua anapinga hilo.
Ni kwa nini mke alikuwa analazimisha hati ya kiwanja iwe kwa majina ya watoto na sio wao wawili wenye mali mume na mke?
 
SWALI (hasa kwa wanaume walioreply wakiunga mkono mauaji na huyu mama kwenye nyuzi zilizopita)
  • JANE ALIKOSEA NINI?
  • NI NINI KIFANYIKE ILI MAUAJI NA UKATILI KAMA HUU USIENDELEE KUTOKEA?
Alikosea kudai Mali ya mwanaume iandikwe kwa jina la mtoto na ambapo unajua watoto ni dhaifu kwa mama namana huyo mama angetafuta mubaba ale naye pesa na watoto jamaa kafanya sawa
 
😂 😂 Hapo ndiyo inakuwaga kamzozo, nyonyo ziko mkononi bibie anakwambia nina kiwanja basi tujenge, unajikuta umekubali tu. Mapenzi yakipungua akili ikakukaa sawa, tayari ushamwaga milioni 100 nyumba iko kwenye finishing, hapo ndiyo hasira zinapofukuta sasa.
Ndo maana mnachapwa risasi

Mnapenda huduma ila mna sahau mmekula jasho la mtu, ni kheri kabisa mchapwe risasi maana eti kisa umezingua na leo uniambie mimi niliye jenga nyumba sina changu kisa kiwanja ni cha kwako...

Mwanaume gani anaweza kuacha tu hilo lipite? Sasa tukutane na mchaga mwenye njaa, anakukera mpaka unatamani ardhi ipasuke
 
#FACT-CHECKING

Usidanganyike, mambo kwa ground yapo tofauti sana. Kwa ushahidi, tupitie ni yapi ya kweli na yapi si kweli kuhusu kifo cha Jane Maloo Urassa ⚰️ aliyeuawa na Laurence Kweka, mwanaume aliyekosa akili, busara na utashi wa kibinadamu.

View attachment 3686843

  1. Jane na Bw. Kweka waliishi kwenye ndoa kwa miaka 18 na miezi 8 na wana watoto 4 - KWELI

  2. Jane alikua mtumishi aliyeajiriwa, mwenye kipato chake binafsi, na elimu ya chuo kikuu (Masters) - KWELI

  3. Jane alimiliki mali binafsi alizotafuta kabla ya ndoa ikiwemo kiwanja kilichojengwa nyumba iliyoleta mgogoro - KWELI

  4. Jane alikua ameshaondoka hapo nyumbani kwenye migogoro kwa zaidi ya miezi miwili na kwenda kuishi kwa ndugu zake na alimuachia bwana Kweka nyumba na pamoja na watoto wote aishi nao - KWELI

  5. Mgogoro mkubwa ulijitokeza miezi kadhaa nyuma baada ya hati ya nyumba kutoka na majina ya watoto na Jane kama msimamizi mpaka pale mtoto wao wa kwanza atakapofikisha miaka 18 - KWELI

  6. Jane alitaka hati ya nyumba iwe kwa jina lake - SI KWELI

  7. Jane aliweza kutengeneza hati sababu kiwanja kilikua mali yake na bwana Kweka hakutaka majina ya watoto kwenye hati bali jina lake mwenyewe, sababu aliamini nyumba ameijenga kwa jasho lake - KWELI

  8. Jane alirudi nyumbani kwao masaa machache kabla ya kuuawa, kuwapelekea watoto wake chakula kwa sababu walikua wameishiwa na baba wa watoto alikua safarini Moshi - KWELI

    PS:
    Mtoto wao mkubwa aliyempigia simu mama yake ataishi kwa uchungu maisha yake yote, akijua bila ya simu yake, mama yao angekua hai leo.

    View attachment 3686846

  9. Kabla ya mauaji, tayari kulikua na kesi polisi na ustawi wa jamii dhidi ya bwana Kweka kuhusu ukatili wa kijinsia na kumtishia mkewe maisha - KWELI

Vyanzo vya taarifa / Sources: (Ukija kubisha na wewe ulete vyanzao vyako)

Tofauti na mambo yanayoendelea mtandaoni na watu wanavyoleta mizaha kuhusu ukatili wa kijinsia na mauaji, Jane Urassa aliuawa kwa sababu alikua tayari kuachana na mume wake na kuhakikisha mali zao walizochuma pamoja zinabaki kwa watoto wao.

Alifanya vile ambavyo wanaume wanashauri humu jukwaani kwamba, using’ang’anie mali ambayo si yako, akampisha mwanaume kwenye nyumba yao, akaacha watoto bila kuwang'ang'ania na bado akauawa kikatili.

Hitimisho:

Jane alifikia mwisho kwenye maisha ya ndoa ila Mr. Kweka hakuwa tayari kuona mwisho wa ndoa yao pekee, alitaka pia kuhakikisha ni mwisho wa maisha yake pia - kusudi lake limetimia.

R.IP Jane 💔

Tupinge Femicide / mauaji ya wanawake

Alamsiki!
Cha msingi leo hii mwanaume kajiongeza mapema kaua kabla ya kuuliwa yeye soo bhita ni bhita muraa
Mara zote huwa nasema huku ndani, mwanaume kukosa akili ndio chanzo cha matatizo mengi kwenye ndoa sababu kuanzia kwenye uchaguzi wa mwanamke wa kuishi nae mwanaume unatakiwa kumsoma huyu mtu atakuja kubadilika au la

Hapa bwana Kweka alikosa akili tokea mwanzo kwa kukubali kujenga kwenye kiwanja cha mwanamke maana ndio makosa yalipoanzia
 
WANAWAKE wa kichaga na ni makatili sana HASA warombo na machame... Wachawi, roho mbaya ...wabinafsi. niliwahi kumiliki kinguchiro cha kirombo maniner zake... Miaka hiyo nasoma pale ushirika. Kidem hakijakwapua vijisalia vya boom langu!, nilikipga futi za maana toka hapo nikakiambia wewe Paula kimario sepa. From there sitaki kusikia mwanamke kutoka kaskazini!.
 
Siku hizi kuna hati ya pamoja kwa assets na mali mlizochuma pamoja

Hata hivyo kwa mujibu wa sheria, mali ambazo mke/mume alichuma kabla ya ndoa ni hiyali yake kuifanya ya pamoja ama yake pekee, japo inashauriwa itengwe na zile zilizochumwa ndoani/kwa pamoja

Hata hivyo, sioni haja ya assets hizo kuandikwa jina la baba ama Mama pekee wakati mnao watoto pamoja

Ni maoni yangu, Mali/assets ziwe zinaandikwa majina ya watoto chini ya uangalizi wa wazazi wote mume/mke

Ikitokea mkaachana/kutengana ni vyema Baba aondoke amwachie nyumba mke ili alee watoto

NB: Mtaka vyote kwa pupa, hukosa vyote ✍️
Vipi kama watot ni wahuni au mateja waue wazazi?
Vipi kama hao wazazi hawataki kuacha urithi kwa hao Watoto?
 
Pamoja na elimu yangu, sikutaka kabisa kujipa stress ya kuoa mwanamke aliyesoma. Mtasema sijiamini, lakini kama ni kutojiamini, basi bora niendelee kutojiamini ili nijue nimekaa sehemu salama na yenye amani kwangu.

Ukitaka kuamini hili, angalia hata historia ya wake wa baadhi ya viongozi wetu. Mama Janeth Magufuli alikuwa mwalimu wa shule ya msingi, Salma Kikwete alikuwa na elimu ya ualimu, na hata wake wa viongozi kama Nyerere na Mwinyi hawakuwa na hizo elimu kubwa tunazoziona leo.

Kwa hiyo, kwangu mimi elimu kubwa kwa mwanamke si lazima iwe kipimo cha kumfanya awe chaguo bora la ndoa. Muhimu zaidi ni tabia, heshima, busara, utulivu na namna anavyoijenga familia.
Mwanamke aliyesoma huwa anakuwa na ego na pride za kishamba sana, anakuwa manipulated na mavyeti kudhani anaweza ku control physical reality. Kumbe hakuna chochote, hao ndo huwa wanaishia kuwa toxic tu, angalia limtu kama li Chura kiziwi
 
Kwa nini mwanamke aliamua kuanza kugawa urithi mapema kinyume cha matakwa ya mume wake?
Ni kwa nini mke alikuwa analazimisha hati ya kiwanja iwe kwa majina ya watoto na sio wao wawili wenye mali mume na mke?
Kwenye hili sijui, naweza kuspeculate tu kwamba labda kulikua na kutoaminiana au intentions za kuhamisha mali za familia kwenda kwa watu wa nje ambao si watoto ila ukweli wanaujua wenyewe wanandoa.
 
Hivi mmejiuliza kama ugomvi wote huu na kisa cha kuua ni kwa sababu watoto hawakuwa wa Kweka? Hasira yote hiyo hadi kuua si rahisi iwe kwa ajili tu ya hati ya kiwanja au nyumba. Labda Kweka alijua watto wao sio wake na bado wanapewa nyumba aliyojenga. Hiyo atafanya wanaume wengi sana wapige mke risasi
 
#FACT-CHECKING

Usidanganyike, mambo kwa ground yapo tofauti sana. Kwa ushahidi, tupitie ni yapi ya kweli na yapi si kweli kuhusu kifo cha Jane Maloo Urassa ⚰️ aliyeuawa na Laurence Kweka, mwanaume aliyekosa akili, busara na utashi wa kibinadamu.

View attachment 3686843

  1. Jane na Bw. Kweka waliishi kwenye ndoa kwa miaka 18 na miezi 8 na wana watoto 4 - KWELI

  2. Jane alikua mtumishi aliyeajiriwa, mwenye kipato chake binafsi, na elimu ya chuo kikuu (Masters) - KWELI

  3. Jane alimiliki mali binafsi alizotafuta kabla ya ndoa ikiwemo kiwanja kilichojengwa nyumba iliyoleta mgogoro - KWELI

  4. Jane alikua ameshaondoka hapo nyumbani kwenye migogoro kwa zaidi ya miezi miwili na kwenda kuishi kwa ndugu zake na alimuachia bwana Kweka nyumba na pamoja na watoto wote aishi nao - KWELI

  5. Mgogoro mkubwa ulijitokeza miezi kadhaa nyuma baada ya hati ya nyumba kutoka na majina ya watoto na Jane kama msimamizi mpaka pale mtoto wao wa kwanza atakapofikisha miaka 18 - KWELI

  6. Jane alitaka hati ya nyumba iwe kwa jina lake - SI KWELI

  7. Jane aliweza kutengeneza hati sababu kiwanja kilikua mali yake na bwana Kweka hakutaka majina ya watoto kwenye hati bali jina lake mwenyewe, sababu aliamini nyumba ameijenga kwa jasho lake - KWELI

  8. Jane alirudi nyumbani kwao masaa machache kabla ya kuuawa, kuwapelekea watoto wake chakula kwa sababu walikua wameishiwa na baba wa watoto alikua safarini Moshi - KWELI

    PS:
    Mtoto wao mkubwa aliyempigia simu mama yake ataishi kwa uchungu maisha yake yote, akijua bila ya simu yake, mama yao angekua hai leo.

    View attachment 3686846

  9. Kabla ya mauaji, tayari kulikua na kesi polisi na ustawi wa jamii dhidi ya bwana Kweka kuhusu ukatili wa kijinsia na kumtishia mkewe maisha - KWELI

Vyanzo vya taarifa / Sources: (Ukija kubisha na wewe ulete vyanzao vyako)

Tofauti na mambo yanayoendelea mtandaoni na watu wanavyoleta mizaha kuhusu ukatili wa kijinsia na mauaji, Jane Urassa aliuawa kwa sababu alikua tayari kuachana na mume wake na kuhakikisha mali zao walizochuma pamoja zinabaki kwa watoto wao.

Alifanya vile ambavyo wanaume wanashauri humu jukwaani kwamba, using’ang’anie mali ambayo si yako, akampisha mwanaume kwenye nyumba yao, akaacha watoto bila kuwang'ang'ania na bado akauawa kikatili.

Hitimisho:

Jane alifikia mwisho kwenye maisha ya ndoa ila Mr. Kweka hakuwa tayari kuona mwisho wa ndoa yao pekee, alitaka pia kuhakikisha ni mwisho wa maisha yake pia - kusudi lake limetimia.

R.IP Jane 💔

Tupinge Femicide / mauaji ya wanawake

Alamsiki!
Yaani Taarifa ya kiwanja kilinunuliwa na mke kabla ni crucial kweli kwa wanawake. Utadhani ipo kwenye DNA zao kuwa kiwanja alichonunua mwanamke hakihusiki na mume. Wataivalia njuga hiyo point ya ulimkuta na kiwanja bila kujali mwanaume amewekeza au la.

Igeuze sasa iwe mwanaume alinunua kiwanja na akajenga, ikitokea wanatakiwa kuachana hutasikia wanawake wakitumia hoja ya kukutwa na kiwanja kumtetea mwanaume, utakachosikia ni alimfulia, alimpikia na ujinga ujinga mwingine ili apate hiyo 50/50.
 
Ni sahihi, lakini kwanini hizi changamoto za mali zinatukumba zaidi sisi ngozi nyeusi?

Unajua familia ya Mo, inao utajiri wa vizazi vitatu kama sio vinne sasa

Na tayari Kuna succession plan ya kumrithisha mtoto Mkubwa wa Mo, nadhani anaitwa Abbas kama sijakosea ili aendeleze

Sisi huku ngozi nyeusi tunaweza kuibiana na kudhurumiana tu

Mimi naanza mchakato wa kuweka assets zote chini ya bodi ya Kampuni ikiwemo nyumba tunayoishi

Kila jambo litahitaji uamuzi wa kikao Cha Bodi
Hiyo bodi nayo inaweza kuingiliwa na baadhi ya decision makers mambo yakaharibika tu, kama unavyosema sisi ngozi nyeusi tuna changamoto kubwa sana. Kama tu watoto uliowazaa ukawapa assets wanaweza kukugeuka, kukufilisi na hata kukuuwa kwa sababu ya mali, usitegemee wa pembeni awe na huruma na mali zako.
 
Back
Top Bottom